Tungekuwa na barabara nzuri, tukafika kazini mapema, tungeweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi; hiyo peke yake kwa namna nyingi ingeweza kutuongezea kipato, au tungetoka kazini na kufika nyumbani mapema, tungeweza kupata muda wa kupumzika na hivyo bongo zetu kufanya kazi vizuri zaidi, hapo tungepata fursa ya kuweza kufikiri nje ya kasha.
Kama umewahi kupanda daladala au kupita karibu na vituo vya daladala hasa asubuhi na jioni, utakubaliana na mimi kwamba kwa aina ile ya usafiri ukifika huko unakokwenda, lazima uwe umeshachanganyikiwa... hebu angalia wanafunzi wanavyopata shida, wengine wanapanda mpaka malori...
Hatukaki msaada kujengewa choo, tunataka mazingira bora yatakayotuwezesha kufanya shughuli zetu kwa ufanisi zaidi ili tupate pesa nyingi zaidi hata tukila zinabakia kidogo tunajengea choo. Kama hiyo ingewezekana nina hakika tunaotumia hivi vyoo tungekuwa wachache sana.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.