Kumbe Serikali yanunua shule ya CCM halafu tunaambiwa imetaifishwa'

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
21,684
2,000
Kwa ufupi
Novemba mwaka jana, Meya wa Manispaa ya Bukoba, Adronicus Karumuna alilalamikia zaidi ya Sh70 milioni za tetemeko hilo lililotokea Septemba 10 mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 17 na kuharibu miundombinu mbalimbali, kutumika kukarabati shule hiyo ya Jumuiya ya Wazazi huku waathirika wakiwa hawajapata msaada wa maana.

======

Hatimaye Rais John Magufuli amehitimisha mjadala wa matumizi ya fedha za msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kwa kukarabati Shule ya Sekondari ya Omumwani inayomilikiwa na CCM kisha Serikali kuinunua.

Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1966 ikiwa ya kwanza ya Wazazi nchini, ilikarabatiwa na Serikali ili kuiwezesha kupokea wanafunzi wa Sekondari ya Ihungo baada ya shule yao kuharibika kwa tetemeko.

Chanzo: Mwananchi
 
Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
5,249
2,000
Anadanganya kaitaifisha kumbe kainunua bila hata kufuata sheria ya manunuzi ya umma
 
Mzee wa hat-trick

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
1,737
2,000
Waaafwa....!!! Kauli mbovu kbs kuwahi kutokea kwa mtu wa hadhi yake, kwenda kwa wananchi wake wenye matatizo
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
76,219
2,000
Kwa ufupi
Novemba mwaka jana, Meya wa Manispaa ya Bukoba, Adronicus Karumuna alilalamikia zaidi ya Sh70 milioni za tetemeko hilo lililotokea Septemba 10 mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 17 na kuharibu miundombinu mbalimbali, kutumika kukarabati shule hiyo ya Jumuiya ya Wazazi huku waathirika wakiwa hawajapata msaada wa maana.

======

Hatimaye Rais John Magufuli amehitimisha mjadala wa matumizi ya fedha za msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kwa kukarabati Shule ya Sekondari ya Omumwani inayomilikiwa na CCM kisha Serikali kuinunua.

Novemba mwaka jana, Meya wa Manispaa ya Bukoba, Adronicus Karumuna alilalamikia zaidi ya Sh70 milioni za tetemeko hilo lililotokea Septemba 10 mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 17 na kuharibu miundombinu mbalimbali, kutumika kukarabati shule hiyo ya Jumuiya ya Wazazi huku waathirika wakiwa hawajapata msaada wa maana.

Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1966 ikiwa ya kwanza ya Wazazi nchini, ilikarabatiwa na Serikali ili kuiwezesha kupokea wanafunzi wa Sekondari ya Ihungo baada ya shule yao kuharibika kwa tetemeko.

Chanzo: Mwananchi
Moderator ipeleke hii kwenye jukwaa lake la siasa .
 
sir longo

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
1,065
2,000
hata mwl nyerere alipokuwa anataifisha viwanda na vitu vingine hakuwa ananyang'anya, alikuwa ananunua. labda hujui majui maana ya neno kutaifisha. ni kubadilisha umiliki kuwa wa TAIFA, kwa kurudisha gharama za mmiliki wa awali. ni bora kujielimisha kuliko kushutum tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom