Kumbe Ripoti ya CAG ni Barking Dog Only! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe Ripoti ya CAG ni Barking Dog Only!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Jun 23, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,328
  Trophy Points: 280
  Kumbe ile Ripoti Maarufu ya GAG, ya ukaguzi wa hesabu za serikali, ni barking dog only, seldom bite! baada ya kubainika kuwa baadhi ya Wizara, Mashirika, Halmashauri na Idara zinazojitegemea, zimekuwa zikifanya matumizi mabaya ya fedha za serikali hadi kupelekea nyingine kupata hati chafu ama zisizo ridhisha mwaka hadi mwaka, kufuata uwezo wa mdhibiti kuishia kwenye kufanya ukaguzi tuu na kutoa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu lakini ufuatiliaji wa ripoti hizo ni jukumu la Idara nyingine za serikali.

  Hayo yamebainishwa na Mkaguzi Mwandamizi wa Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, Bw. Doegratias Kilama, wakati akielezea shughuli mbalimbali za Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, kwenye maonyesho ya Wiki ya Utumishi, yanayoendelea kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

  Bwana Kilama aliyasema hayo, alipokuwa akijibu swali toka kwa wananchi, walitaka kujua, kwa nini kila mwaka Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha baadhi ya taasisi kuwa na matumizi mabaya ya fedha za serikali na hakuna kinachofanyika, kwa ofisi zile zile kupata ripoti chafu huku zikiendelea kupatiwa migao mingine na kuendeleza matumizi mabaya.

  Bwana Kilama alifafanua kuwa majukumu ya Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, yanaishia kwenye kufanya ukaguzi tuu na kutoa ripoti yenye mapendekezo yake. Jukumu la nini kinafuatia baada ya hapo, sio la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, jukumu hili linabaki kuwa la serikali kupitia vyombo vyake vinginevyo.

  Hata hivyo, wananchi walio wengi, walitoa maoni kuwa Ofisi ya CAG, ipewe meno zaidi, ikiwemo uwezo wa kuziwajibisha zile taasisi zenye ripoti chafu zinazijirudia rudia kwa kutofuata maoni ya Mdhibiti na Mkaguzi, ukiwemo uwezo wa kuzua mgawo wa fedha za serikali kwenda kwenye taasisi zenye matumizi mabaya ya fedha za Umma.

  Kwenye Banda la Ofisi ya Ukazi ya Taifa, wananchi wamekuwa wakigawiwa bure, vitabu vyenye taarifa mbali mbali za ukaguzi, ikiwa ni pamoja na jupatiwa nakala pepe ya Ripoti za Ukaguzi, zilizohifadhiwa kwenye CD kwa matumizi rahisi ya compyuta.

  Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, ni miongoni mwa taasisi zilizoainishwa kwa kifungu namba 143 cha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na kuanzishwa kwa Sheria ya Bunge, ya Fedha za Umma, Namba 6 ya Mwaka 2001, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jun 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,392
  Trophy Points: 280
  mzee mbona hili tumelipigia kelele muda mrefu tu? Hata leo kwenye mojawapo ya makala zangu nagusia hili tena. Tunapouita huu ni "MUK" tuna maana yake ndugu yangu..
   
Loading...