Kumbe Rais wa Muungano akiwa Zanzibar yuko chini kwa Rais wa Zanzibar

Huu ni muungano wa mazingaombwe, kiini macho.

Hakuna anayeweza kuueleza ukaelezeka, ukafahamika. Ndio sababu wenye Muungano huu wanaishia kusema Muungano wetu ni unique!

Nilipitia chapisho moja linaitwa shirikisho ndani ya shirikisho linapatikana hapa https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/100638-shirikisho-ndani-ya-shirikisho.html

Humo waandishi wanasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Muungano wa baadhi ya mambo na si muungano kwa baadhi ya mambo.

Kwa dhana hii inamaanisha kuwa Serikali ya Muungano ya Tanzania sio serikali kuu kama vile mfumo wa US au UK. Hapa ndipo jamaa wa mazingaombwe wanapopata hoja ya uniqueness ya Muungano huu wa mazingaombwe, usanii.

Lakini serikali ya Muungano inafanya kazi za serikali ya Tanganyika vilevile kama vile serikali ya UK inavyofanya kazi za serikali ya England.

Kwa kufupisha, Muungano huu ni kama zile hekaya ya nusu mtu,nusu samaki. This Muungano is a myth!

https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/123054-je-tanzania-ni-nchi-moja.html
Teh teh teh! Kaka umeponda na kuchana kabisa, i've got your feeling, it is a really myth, because hawa wenzetu inapotakiwa ku-share resources za Tanganyika they like it a lot, lakini pamoja na kukataa ku-share zile za kule Zbr, ambazo hata hivy hazina uhakika bado, wakiambiwa kwa mfano sasa hivi kama nchi basi waanze ku-contribute kwenye muungano the always fall to their knees! tunawasubiri kwenye tume ya katiba yetu; ingawa ya kwao kungekuwa vita tungejaribu hata kutoa mawazo kuwasaidia; na madudu yao mnayaona, Watahitajika kuchangia gharama za uendeshaji wa tume kama nchi inayojidai katika muungano, i hope tutawabana hapo and show them the door! my ribs again fella!!!
 
ukifikiria kwa makini JK hana nchi anayotawala. yeye sio rais wa Zanzibar na wala sio rais wa Tanganyika.
Ni kweli kabisa mkuu, he's in the river between! President of no-country, Tanganyika ameikana kabisa, halafu Zanzibar kule ni mzushi fulani hivi! this is not the first time, hata mwaka jana it was the same scenario, tena even worse, waziri mkuu alikuwa deep down kwenye hiyo protokali! Nataka niulize kaswali kamoja, hivi katiba ya Zbr inasemaje kuhusu Seriksli ya muungano????
 
Katika kuwasili uwanjani kwenye sherehe za muungano aman stadium zanzibar Rais wa muungano ameingia uwanjani kabla ya Rais wa Zanzibar. Kwa maana hii Rais wa muungano anatangulia uwanjani ili awe tiyari kumkaribisha "mdogo" wake atakapowasili uwanjani. Kwa wenye kuulewa huu muungano nielemisheni.

Hii ni kukujulisha kuwa Zanzibar ni nchi kamili yenye mamlaka kamili na imetimia.

 
wadau nisaidieni, katiba ya zanzibar ina sema zanzibar ni nchi, je katiba ya muungano yasemaje katika jambo hili?

Katiba ya Muungano inamtambua Rais wa Zanzibar kawa waziri asiye na wizara maalumu kwenye serikali ya JMT.
 
wadau nisaidieni, katiba ya zanzibar ina sema zanzibar ni nchi, je katiba ya muungano yasemaje katika jambo hili?

Wakati wa Sakata la Pinda na Zanzibar ni nchi au sio nchi

JK, current Tanzanian citizen number one alisema hivi nina quote. " Hili suala (ZNZ ni nchi au sio nchi) linategemea unalizungumzia ukiwa wapi. Ukiwa katika mipaka ya JMT, Zanzibar ni nchi, ukiwa nje ya mipaka ya JMT, Zanzibar sio nchi" Mwisho wa kunukuu. Hapa ndipo ninaungana na jamaa aliyesema huu muungano wetu ni sawa na hadithi za folklore za samaki mtu (Nguva/Mermaid).


Mahakama kuu ya Tanzania iliwaachia watuhumiwa wa uhaini Zanzibar (Rashid Hamad and Co) Kwa maelezo kwamba, Uhaini hauwezi kufanywa Zanzibar. kwasababu Zanzibar sio nchi. Hiyo ruling bado ina stand. Kwa mjibu wa katiba chombo chenye mandate ya kutafisili sheria katika JMT ni mahakama.

Swali Je, kati ya mahakama na JK tumwamini nani? Because hao watuhumiwa wa uhaini ilidaiwa walitenda kosa hilo wakiwa katika mipaka ya JMT.
 
Labda tusimlaumu sana Dk. J.M.Kikwete, kwani kumbukumbu ya uhuru wa Zanzibar imeanza jana tu!? La hasha, imeanza zamani. Kama ukweli ndio huo, basi tujikumbushe marais wote wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliomtamgulia Dk. Kikwete, wao walikuwa wanafuata protokali/itifika ipi katika sherehe za kumbukumbu ya uhuru wa Zanzibar?
 
..lakini Raisi wa ZNZ ni Waziri asiye na Wizara Maalum ktk serikali ya muungano.

..huu muungano tabu tupu. bora tuuvunje tu na kuanzisha mashirikiano kupitia EAC au SADC.
 
Zanzibar ni sehemu ya JMT, na rais wa JMT ana mamlaka yote ya kuigawa Zbr katika mikowa baada ya kushauriana na rais wa Zbr.

Msimamo huu ni msimamo wa wengi ambao huwa wanasahau pia kuwa Zanzibar ni member/ partner mmoja wa muungano. Dhana ya kuwa Zanzibar ni sehemu ya muungano ni sawa. Sehemu nyengine ni ipi? member/partner mwengine wa Muungano ni yupi?

Hapa ndipo unapokuja utata na mazingaombwe ya muuungano wa TanZania.
 
..hata tukiunda serikali 3 bado ktk shughuli/sherehe zinazohusu Tanganyika au Zanzibar Raisi wa muungano atakuwa mgeni mwalikwa.

..lakini tusisahau kwamba Zanzibar ni ndogo mno kuwa ktk muungano wa shirikisho wenye serikali 3 na nchi kubwa kama Tanganyika.

..hiyo equal partneship itapatikana vipi wakati wa-Tanganyika tuko milioni 40 na wenzetu wa-Zanzibari wako milioni 1?
 
Lakini serikali ya Muungano inafanya kazi za serikali ya Tanganyika vilevile kama vile serikali ya UK inavyofanya kazi za serikali ya England.

l

Na ndio maana PM wa UK lazima atoke England tofauti na kwetu ambapo anaweza kutoka znz
 
Katiba ya Muungano inamtambua Rais wa Zanzibar kawa waziri asiye na wizara maalumu kwenye serikali ya JMT.
Haya ndio katika madharau ya hali ya juu. Na ni kwa sababu kama hizi ndio zinafanya muungano unakuwa kitu cha kipuuzi,kijinga..Hapa ni kuwa unaondoa thamani ya mshirika wa muungano halafu tunategemea tutapata Muungano wa maana.

Hili linaongeza katika zile zinazoitwa kero za Muungano. Mwisho wake kama ilivyofikia sasa Muungano wenyewe unakuwa ndio Kero.Muungano umekuwa mataputapu kwa Watanganyika na umekuwa maudhi kwa "wavisiwani".

Katiba inayotambua kiongozi mkuu wa mshirika mmoja wa Muungano kuwa ni waziri asiye na wizara maalum, huwezi kuiita katiba. Kama tutang'angania kuiita katiba basi tuseme ni Katiba mbovu, katiba ya kisanii, katiba ya mazingaombwe!

Ni afadhali kusikiliza masimulizi ya pwagu na pwaguzi au kusoma visa vya pimbi kulikoni katiba tuliyonayo leo.
Katiba inayolalamikiwa na kila mtu, isipokuwa mwanachama wa CCM,. katiba inayolalamikiwa na kila chama cha siasa ,isipokuwa CCM.

Katiba iliyopo kama hatutaibadilisha, itatuletea majanga ya kitaifa. Tukiingia uchaguzi mkuu bila ya Katiba ya watanzania. Nchi ya wadanganyika itakumbwa na tsunami.

Nani hajui kuwa katiba iliyopo ni Katiba ya CCM. na wameng'ang'ania kuwa kuibadili haitaki mwendo mdundo, pole pole kama mwendo wa jongoo mpaka itakapotuletea maafa ya kitaifa ndio tutaibadili fasta fasta!
 
Katika kuwasili uwanjani kwenye sherehe za muungano aman stadium zanzibar Rais wa muungano ameingia uwanjani kabla ya Rais wa Zanzibar. Kwa maana hii Rais wa muungano anatangulia uwanjani ili awe tiyari kumkaribisha "mdogo" wake atakapowasili uwanjani. Kwa wenye kuulewa huu muungano nielemisheni.



Jawabu ni ndogo tu mdogo wangu! Hata kwenye harusi Baba na mama hutangulia wakisubiri wenye harusi (Maarusi) wafike wa mwisho na kuanza sherehe!
 
ndo ujue huu muungano ulivyokuwa wa kipuuzi raisi wa Jamhuri ya Muungano ndiye anaetakiwa kuwa mkubwa lakini kwa sababu muungano huu ni wa kipuuzi Zanzibar imebaki kuwa nchi hivyo na raisi wao kuwa mkubwa katika nchi yake kwa kifupi Kikwete ni mualikwa

Umeona wapi mtu si nyumbani kwake akawa yeye awe mwenyeji? Hivyo baba zetu huwa wakubwa ndani ya nyumba zetu?
 
Hapo wanaadimisha mapinduzi ya mwaka 1963, wakati huo zanzibar ilikuwa nchi, na tanganyika ilikuwa nchi.
kwa maana hiyo leo JK amekaribishwa kama mgeni katika sherehe za mapinduzi.
Kinachonikera ni kwamba wazanzibari wanaadimisha sherehe za mapinduzi bila hata kumkumbuka mwanamapinduzi wa Kweli John Gideon Okello.

Mamluki huishia malipo tu! Na maea nyingi hawa huhesabiwa kama wauwaji wa kukodiwa.tu
 
Mkiambiwa Zanzibar ni nchi hamtaki. Huo ndio ushahidi wa wanachokisema wazanzibari kila siku.
 
Jawabu ni ndogo tu mdogo wangu! Hata kwenye harusi Baba na mama hutangulia wakisubiri wenye harusi (Maarusi) wafike wa mwisho na kuanza sherehe!

Laiti ungejua umri wangu usjngeniita "mdogo wangu".Pili mfano ulioutoa ni mwepesi mno kukidhi hoja nzito kama hii ya muungano.
 
Back
Top Bottom