St Lunatics
JF-Expert Member
- Aug 29, 2015
- 6,644
- 11,166
Juzi ijumaa nilikwenda kumtembelea dada yangu(mtoto wa baba mkuu) nilipofika nikawasalimu na kukaa sebuleni. Tukaanza kuongea mambo tofauti mara mtoto wa dada yangu akasema anataka kuongea na mimi, nikanyanyuka na tukatoka nje ya nyumba. Akaanza kuniambia kama kuna shughuli ya harusi ya shoga yake amesoma nae shule, na yeye hana hela ya mchango na kununua nguo za harusini. Nikamuuliza kiasi gani akasema 100,000 tu inatosha nikatia mkono mfukoni na nikampa 150,000 alinishukuru tukarudi ndani na kukaa. Nikiwa naomngea na dada yangu na mume wake mara nikasikia sms imeingia kwenye simu yangu kuangalia huyu dogo ndie alietuma hii sms ya kunishukuru tena kwa kumpa hela. Nikajibu usijali mara katuma nyengine ooh lakini hela nyingi ulionipa, nikamuangalia akanipa tabasamu nikamjibu zitakazo bakia zitakufaa kufanyia mambo mengine. Akanitumia sms nyengine akiniuliza kesho kama anaweza kuja nyumbani kwangu saa ngapi nitakuwepo nyumbani. Nimebaki kujiuliza hivi anamaanisha nini? Ameona kumpa ile hela kuna haja na yeye kunipa kitu? Manake nimempa hela kama mtoto wa dada yangu na sikuwa na lengo lolote kwake. Alituma kama sms 7 sikujibu tena, nilibaki kuaga na kuondoka zangu. Nikiwa njiani akanitumia sms nyengine akiniuliza kama nimemnunia, nilimjibu nipo na pirika kwa sasa nitakujibu baadae sijamjibu tena mpaka leo.