Hypersonic
JF-Expert Member
- Apr 14, 2012
- 703
- 1,331
Wana wa Jamiiforums, Nawasalimu.
Sina uhakika kama hili linatokea kwangu tu au ni kwa kila mtu zaidi ya mara tatu au nne imetokea kwamba nikipiga tu simu kwa mtu tukajadili habari ya hela ambayo pengine natakiwa kuituma kwa njia ya simu pindi nikikata tu simu meseji inaingia kuwa tuma kwa namba hii.
Leo hii saa nne na dakika 21 nimepiga simu kuuliza nauli ya basi kutoka Musoma kwenda Arusha kwa njia zote mbili kwa maana ya Musoma via Serengeti na Musoma via Singida baada tu ya kukata simu saa 10:38 meseji kaingia kwamba hiyo hela tuma kwa Airtel 0698 338 2** Jina BEATRICE KAKUSA. Namba iliyotuma SMS 0697 160 5**. Ajabu mimi pia natumia airtel.
Siku ya jumanne tarehe 4/06/2024 saa nne dakika 35 niliongea na mama yangu ambaye yuko kijijini zilikuwa zinahitajika kutoa kiasi fulani cha hela kwa ajili ya kulipia kibali cha kuhamisha ngómbe toka kata moja kwenda nyingine, ambapo kwa kila ngómbe mmoja ilhitajika shilingi elfu 5.
Ile namaliza tu kuongea na mama saa 4 na dakika 40 meseji ikaingia hiyo hela tuma kwenye namba hii 06987234** jina litakuja Ester Kalinga namba iliyotuma sms 0616 894 5**.
Kutokana na hiyo mifano je niendelee kuamini kuwa hawa watu wabahatisha au Airtel ina watu wanasikiliza mawasiliano yetu na kuwapa matapeli taarifa? Hii tume ya kulinda taarifa ipo kweli na kazi zake ni zipi.