Kumbe P-Funk siye aliyetengeneza mdundo wa She Got a Gwan

kwa-muda

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,163
2,223
Ule mdundo kicks na drums kazigonga Soggy Doggy.
Gitaa kalipiga mzungu kichaa
na piano kaipiga jamaa mwingine kabisa.
Tena Pfunk alikuta soggy na mzungu kichaa washafanya yao akaiona kali akamwita jamaa aje aweke piano.
Sema credits zilienda kwake P-funk kama producer mkuu
 
Ngoma nyingi kafanya bizman Kama zeze..mtazamo n.k sijui kwanini majini alimbania jamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Majani nimemuelea kasema chief producer anaweza asitengeneze chochote zaidi ya kusema hapa mziki usimame hapa ianze verse hii au afanye na mastering. Katolea mfano wa band anasema band ikija studio wanakuwa washatengeneza midundo sometimes hata vyombo wanapiga wao lakini anayevinga na kuvimaster ndiye natambulika kama producer.
 
Daah Kumbe! sie wengine tunajuaga ni majani!.. halafu naskia yule jamaa mnene bizman ndo anafanyaga string pale bongo record??
 
She got a gwan, ngoma kali sana hii.
Maana ya neno "she got a gwan" ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Gwan ni neno la kijamaica linalomaanisha 'go on' ila mara nyingi hutumika kwenye sentensi fupi 'wa gwan' kumaanisha 'what is going on'.

Mpaka anafariki dunia, Mangwea hakuwahi kutoa tafsiri ya alivyolitumia yeye kwenye wimbo wake.. Japo ukiamua kutumia akili za kuunga unga, utaelewa mantiki yake ilikuwa ni kumaanisha 'she got one' - yaani huyo demu amekamilika kwenye kila idara..

Naweza nisiwe sahihi.
 
Beat nyingi mbona hatengenezi Majani, kuna Ludigo Bishota maarufu kama Professa Ludigo kafanya kazi kubwa mno, pia hao wengine wakiwemo.

Ndiyo hivyo ni mmiliki wa studio ndo maana sifa anabeba yeye
 
Gwan ni neno la kijamaica linalomaanisha 'go on' ila mara nyingi hutumika kwenye sentensi fupi 'wa gwan' kumaanisha 'what is going on'.

Mpaka anafariki dunia, Mangwea hakuwahi kutoa tafsiri ya alivyolitumia yeye kwenye wimbo wake.. Japo ukiamua kutumia akili za kuunga unga, utaelewa mantiki yake ilikuwa ni kumaanisha 'she got one' - yaani huyo demu amekamilika kwenye kila idara..

Naweza nisiwe sahihi.

She got a gwan mi nilidhani anamaanisha she got a gun kumbe nipo wrong sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom