Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Rais anasema amekuta uchafu mwingi serikalini. Ni lazima yeye na wasaidizi wake wajikite kwenye kuusafisha kwanza. Watu walikuwa wanahoji kwanini rais hasafiri kwenda nje na anawaachia wasaidizi wake, jibu ni uchafu mwingi katika kila sekta. Ina maana gani kusafiri kwenda nje wakati humu ndani mambo yanajiendea tu.
Kiongozi mkuu wa awamu ya nne alikuwa anapita angani na ndege kuelekea ughaibuni wakati ardhini yaani pale bandarini mafuta yanayoshuka kutoka melini yanachezewa na wenye fedha. Unaenda nje kuomba msaada wakati mianya ya rushwa ni mingi na hakuonekani juhudi yoyote ile ya kuiziba. Unaenda nje na kupewa tuzo wakati taasisi inayotakiwa kupambana na rushwa na yenyewe ni mzigo kwa taifa. Unaenda nje wakati kina mama wanalala chini pale Muhimbili.
Uchafu ni mwingi, uzembe ni mwingi. Tija ya taasisi nyingi na yenyewe ni ya kusuasua. Ni afadhali rais ameamua kuwa mkweli. Naamini rais atasafiri sana kwenda kuhudhuria vikao vya AU na UN, lakini wakati huo ukifika huu uchafu aliousema utakuwa umepungua.