pilipili usiyoitafuna yakuwashia nini?!! kauli zingine tuziangalie la sivyo zitatuweka matatani.
Akihojiwa na the Daily Nation, Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono hatua za kijeshi za Kenya huko Somalia ili kujilinda dhidi ya Al-Shabaab. Source: JF twitter.
Hii maana yake unapomuunga mkono adui wa rafiki yako maana yake automatically unakuwa adui wa adui wa rafiki yako pia. Hivyo, kwa maana nyingine indirectly tumetangaza vita na Al-Shabaab.
Pengne pia kauli hii ya Rais imekuja ili ku-support kauli ya Kova kuhusu kufuta maandamano yaliyokuwa yafanyike kupinga kulipwa DOWANS. Anyway, mbinu za kisiasa ni nyingi.
Mbona nasikia Waingereza wanatutuhumu kuwa tuna wahost Al Shabbab?
Ni kituko cha aina yake yaani Watanzania wanatishwa na Al Shabaaby na serikali inakubali? Kwa maana nyingine ni kwamba Serikali ya Tanzania ilikubaliana na serikali ya Kenya wapeleke majeshi huko Somalia.
Lengo hapa ni kuwapa furusu Al shabaab kuingia nchini tena wanaweza kusaidiwa na serikali ili kuwatisha Watanzania. Hii ni nini maana yake, ni kuwa Serikali ya Tanzania inajua mahali na sehemu ambapo imewahifadhi Al Shabaaby hapa nchini. Serikali itakuwa tayari kuwasaidia Al shaababy kutekeleza mashambulizi yao.
Watanzania kuweni macho, CCM ni Al Shaababy ya Tanzania. Ukweli unajieleza wenyewe kuhusu viongozi wa Serikali kukumbatia makundi ya kihalifu ili kubaka demokrasia nchini.
Hii ni hatari sana.
Na wewe nawe akili yako imekupeleka huko kumuunga mkono raisi kwamba Alshabaab ni tishio kwa Tanzania pia.Wewe vipi, kwa hiyo ulitaka rais aunge mkono Al-shaabab? Jamani, mambo gani haya. Ushabiki gani huu. Tanzania tujihadhari na watu wa aina hii ambao hawana uzalendo. Sote tuunge mkono kauli hiyo ya Rais. wote tuwe walinzi popote pale tunapotembea. Inawezekana kabisa Al-Shaabab wakawa na vibaraka nchini, wote hao tuwaumbue, tuwe kitu kimoja katika hili bila kujali tofauti zetu za kichama, kidini na hata kijamii
Tukumbuke wanaoathirika sana na matukio haya ni wazee, watoto, walemavu na wanawake. Tusifike huko. Aidha ni lazima tuwekane wazi kwamba GAIDI hachagui wewe ni adui yake au la, lengo lake ni kutimiza azma yao popote pale. JK tunaungana na wewe kulinda nchi yetu kwa gharama yoyote.
Mungu Ibariki Tanzania, tuepushe na wenye wivu na amani yetu
kuna kipindi alikuja Rais wa Somali..pengine ana msupport mwenzake...
Raisi gani huyo mbona sina kumbukumbu.Amekuja mara mbili. Kuna wakati alipewa msaada wa mahindi!
Mkuu unaona mbali!Ni kituko cha aina yake yaani Watanzania wanatishwa na Al Shabaaby na serikali inakubali? Kwa maana nyingine ni kwamba Serikali ya Tanzania ilikubaliana na serikali ya Kenya wapeleke majeshi huko Somalia.
Lengo hapa ni kuwapa furusu Al shabaab kuingia nchini tena wanaweza kusaidiwa na serikali ili kuwatisha Watanzania. Hii ni nini maana yake, ni kuwa Serikali ya Tanzania inajua mahali na sehemu ambapo imewahifadhi Al Shabaaby hapa nchini. Serikali itakuwa tayari kuwasaidia Al shaababy kutekeleza mashambulizi yao.
Watanzania kuweni macho, CCM ni Al Shaababy ya Tanzania. Ukweli unajieleza wenyewe kuhusu viongozi wa Serikali kukumbatia makundi ya kihalifu ili kubaka demokrasia nchini.
Hii ni hatari sana.