Kumbe Muungano ukivunjwa Zanzibar wana maili 10 tu kutoka nchi kavu

Mimi sioni tatizo hata kama zingekuwa chini ya maili 10. Kuna nchi inaitwa LESOTHO iko katikati ya Afrika ya kusini kama ilivyo Dodoma kwa Tanzania lakini ni nchi huru na inayotambuliwa kimataifa haina hata hizo maili 10 pande zote. Mbona Marekani ni nchi tajiri duniani lakini haina madini na migodi mingi kama Tanganyika? Tanganyika inaweza kuwa na kilometa nyingi za maji ya bahari na maziwa lakini ikawa masikini kuliko Zanzibar. Hata sasa angalia Tanganyika ina mito, mabwawa, maziwa bahari na vyanzo vingi vya maji lakini wananchi wake wanashida kubwa ya maji na umeme kuliko hata nchi zilizopo jangwani kama Libya na nchi nyingine za kiarabu. Ukubwa wa kichwa sio wingi wa akili mkuu. Unaweza kukuta ndani kimejaa matope tu kama baadhi ya ving'ang'anizi wanaoendesha bunge la katiba!

Wkati mwingine unatakiwa kufanya utafiti kidogo kabla ya kusema. Marekani ina migodi mikubwa na madini mengi na kwa wingi sana kuliko Tanzania.
 
Back
Top Bottom