Kumbe mtenda akitendewa husema ameonewa

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,444
Mzee mmoja kutoka makao makuu ya nchi alikuwa ombaomba maarufu sana hapa jijini.Alikuwa na mtindo(tuseme pozi) tofauti ya ushawishi.
Aliweza kukusindikiza kwa magoti mpaka utakapompatia chenji ulizo nazo mfukoni.Au alitambaa kama mtoto wakati wa kuomba fadhila.
Mara nyingine asubuhi uendapo kazini unamkuta amelala chali akinyosha juu mkono wenye kopo tupu.Unaporudi alasiri unamkuta katika hali ileile.
Hivyo itakuaminisha kwamba mzee wa watu hajatia kitu chochote tumboni, hivyo bila huruma hautasita hata kumchangia bila kuhisi pengine alikuwa msanii.
Mzee huyu alifanya shughuli yake kwa ufanisi wa hali ya juu kiasi cha kufungua fursa kwa wengine wa aina yake.Mambo yaligeuka baada ya vyombo vya habari
kuonyesha picha za nyumba,mifugo na mali alizowekeza huko kijijini kwakekutokana na "kazi" yake ya huku mjini.
Akawa ametangaza fursa. Vikongwe na maajuza kibao wakawa wanachangamkia tenda .Lakini kwa bahati mbaya kwenye msafara wa gorong'ondo hapakosekani gong'ole;
Akaibuka mzee kutoka ukanda wa Pwani akaja na staili mbovu ya kuudhi kupita kiasi.
Tofauti na yule mzee wetu wa Idodomya aliyeasisi dambwe lake kwenye mitaa ya Mnazi Mmoja, huyu wa Pwani alikuja na mtindo wa kushtukiza kwenye mitaa tofauti.
Leo Karikoo, kesho Ilala, mtondo Buguruni, Mtondo wa kesho unamkuta Sinza, mtondogoo unaweza kumkuta Posta. Kaila alipokutana na harufu ya pesa aliangua kilio.
"Baba nisaidie..." alisema kwa kitetemeshi akifuta kamasi na machozi."Nimeingia leo namtafuta mwanangu nikaambiwa alishakufa...Hapa nilipo sina hata sentano
...Tena sijala tangu juzi...Eeeeeh Mungu kwanini umeniumba na uzee wote huu?Leo itakuwa mgeni wa nani mie...Yaillahi na umaskini huu..."
Ukianza kumuelekeza ilipo wizara au taasisi inayoshughulika na wazee aina yake, ataangua kilio kikubwa zaidi.Utaona ni rahisi kumchangia pesa ya nauli
arudi kwao au atafute namna inayofaa kushughulika na tatizo lake kuliko kumfanya kuwa mgeni wako.
Siku moja watu walishuhudia mzee huyo akiumbuka mbele ya kijana mmoja."Wee mzee si nilikupa nauli toka juma lililopita?Huyo mwanao kafa tena?"
Mzee akataka kumtoroka lakini mama mmoja akapaza sauti kuwa hiyo ilikuwa ni kawaida yake. Alinaswa na kupigwa makofi mbele ya umma.
Binadamu yeyote hughabidhika sana anapofanywa mjinga. Nasikia hata mwizi anapoibiwa uchanganyikiwa na kuwa kama kichaa.Hi linadhihirisha kwamba mtenda
akitendewa anaona kama ameonewa. Anapoiba anajiona mjanja ila. Hivyo kinyume cha ujanja ni ujinga.
Lakini mtu mwadilifu anapodanganywa huumia zaidi.Huyu anazijua athari za uongo, anajua kwamba unapomfanyia mwenzake dhambi ya aina hiyo
unamsababishi maumivu ya kiasu gani? Pale anapofanyiwa yeye hujiuliza maswalimengi sana.Na majibu yake hueda yakawa makali maradufu.
Tumeshuhudia maradufu watu wanaokimbilia mipira ya gari maarufu kama matairi,mafuta na kiberiti mara tu wanaposikia kukamatwa kwa mwizi.
Kama nilivyosema watu wengi wa aina hii ni wacha Mungu.Ni wasikivu na wasamehevu.Wanashika amri za Mungu na kutenda kadiri wanavyopenda kutendewa.
Lakini wana bahati mbaya kudhani kuwa kila binadamu hufikiri kama au zaidi yao.
Kwa upande wao, wadanganyifu hudhani waliumbwa kuwa hivyo.Wanajisikia fahari wanapojipatia mali na heshima kutokana na fani hiyo.
 
Mnaotaka picha hio,
49906923_2012580138795940_5850712284915518550_n.jpg
maana hamjasema picha gani so mie nimewawekea yoyote tu
Uzi bila picha ni sawa na kuunga mkono juhudi huku ukiwa mpinzani
Tupia picha mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom