Kumbe Lissu anajitambua kama 'Msaliti wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania'?

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
Ni kwa maneno na kauli yake mwenyewe Lissu!,kupitia mahojiano na na Clouds360.

Kwamba masaa mawili kabla ya shambulio lake huko Dodoma,amemtuhumu aliyekuwa Rais wa awamu ya tano. Marehemu John Pombe Magufuli (R.I.P). kwa kusema kwamba alitamka kwenye hotuba yake.

"Wasaliti Wa Nchi Yetu, Wanafaa kupigwa Risasi,Askari Wanajua Huwa Tunafanyaje"...Lissu.

Sasa kama Lissu anadai, Magufuli alikuwa akiongelea kuhusu "wasaliti". Iweje yeye Lissu ahusishe kauli ya Usaliti na Shambulio lake?

Je, ni kweli sasa, kupitia kauli yake Lissu mwenyewe, kwamba anakubali yeye ni msaliti katika nchi hii?

Pili: Lissu mpaka leo ameendelea kumficha, Shahidi namba moja kwenye lile shambulio!

Dereva wa Lissu amefichwa mpaka leo,na Lissu anapozunguka kote,hakuna kipengele hata kimoja anapozungumzia kuhusu kutoweka kwa dereva wake,na mahali alipo mpaka sasa!

Tuunganishe "Dots" tusipelekane wote kama misukule!

Hatupendi watu kushambuliwa nchi hii,na wala haikuanzia utawala wa awamu ya Tano tu.

Hata Awamu ya nne,kina Dokta Ulimboka walishambuliwa na kutupwa huko Mabwepande.

Kuna waandishi wa habari kama Saed Kubenea walimwagiwa tindikali usoni.

Kuna yule Mhariri na mwandishi Mwingine nguli mpaka leo hana jicho moja.

Kuna kiongozi wa UPDP , Peter Mziray(R.I.P).
Aliuliwa nyumbani kwake jijini Dar es salaam.
Hiyo yote ilikuwa awamu ya Nne.lakini hayo hayasemwi,badala yake limezuka genge linalopigana na kaburi la Magufuli 24×7!

Ni kwa faida ya nani?
Kwa malipo gani?
Kwa malengo gani?

Hata Magufuli,aliwahi kulishwa sumu na akaponea chupuchupu huko awali.

IMG-20230204-WA0007.jpg


Je! LISSU!
Alojihisi vipi kwamba yeye ndie msaliti alietajwa?
Ni usaliti gani aliokuwa akiufanya kisirisiri?
 
Sasa angalia upande wa pili wa coin, President Magufuli kutamka maneno hayo ni sahihi kuhusiana na usaliti? Elewa matamko kama haya yanachochea vigilate, pia juilize why hadi leo police hawatoa ripoti ya awali kuhusu uchunguzi wao, hata vitu simple kama, silaha iliyotumika/ zilizotumika, risasi ngapi zilifwatuliwa kwenye ile crime scene, CCTV ripoti, statements za guards, na je police walifungua docket ya attempted murder?,... pithole country
 
Usaliti kokote pale haufai

Ikitokea tu umesalitiwa na mke akagawa uroda kwingine na ukabahatika kujua, ni ama zake! Sembuse mtu anayeharibia maisha mamilioni ya watu kwa tamaa tu ya kitu kidogo?

Serikali ya kuvumilia watu aina hiyo haipo na haitazaliwa!

Sjasema mtu fulani ni msaliti
 
Sasa angalia upande wa pili wa coin,President Magufuli kutamka maneno hayo ni sahihi kuhusiana na usaliti?elewa matamko kama haya yanachochea vigilate...
Wewe unatarajia Police wakuletee taarifa ya uchunguzi na upelelezi wao humu mitandaoni?

Magufuli kama amiri jeshi, anaweza kutoa kauli kukemea usaliti.

Lakini iweje Lissu ajihisi hotuba ile ilimlenga yeye?

Kuna usaliti gani anaoujua aliudanya, hadi kuhisi alikuwa akilengwa yeye?
 
Lisu ameendelea kudai kwamba hayati Magufuli aliagiza msaliti hasitahili kuishi na baada ya muda mfupi Lisu akashambuliwa kwa risasi Dodoma, je kumbe Lisu alikuwa anajijua ni msaliti wa nchi?, maana Magufuli hakutaja jina la mtu alitaja msaliti. Kwa nini Clouds FM hawakumuuliza dereva wake amemficha wapi?

Kwa nini Clouds hawakumuuliza sababu za Acacia kufutwa Tanzania na hawakushitaki MIGA?

Kwa nini Clouds hawakumuuliza kama alipigwa na Magufuli na sasa hivi ni miaka miwili Magufuli hayupo kwa nini uchunguzi haufanyiki sasa hivi?

Nb: watoto wa Mbowe na Lisu wote ni raia wa Marekani.
 
Wewe unatarajia Police wakuletee taarifa ya uchunguzi na upelelezi wao humu mitandaoni...
Ndio maana nchi hii inahitaji katiba mpya, Botswana president pamoja na uamiri wake wa jeshi, hawezi kuingiza jeshi mitaani bila bunge kuidhinisha!,hivyo hivyo kwa Namibia na SA,

kuwa amri jeshi mkuu sio kigezo cha kutamka reckless statement kama hiyo kutoka kwa president magufuli, social networks ni sehemu ya mawasiliano kwa dunia ya sasa, technology inakwenda mbele,sisi tupo tumesimama, president magufuli alikua dictator
 
Magufuli alisema msaliti wa nchi hatakiwi kuishi na baada ya masaa machache nikapigwa risasi ~~~~~ Lisu.

Kumbe anajijua kabisa ni msaliti
 
Magufuli alisema msaliti wa nchi hatakiwi kuishi na baada ya masaa machache nikapigwa risasi ~~~~~ Lisu.

Kumbe anajijua kabisa ni msaliti
 
Ndio maana nchi hii inahitaji katiba mpya, Botswana president pamoja na uamiri wake wa jeshi, hawezi kuingiza jeshi mitaani bila bunge kuidhinisha!,hivyo hivyo kwa Namibia na SA...
But the country needed him.
 
Umepatia patia sana bro!
Jiwe alitangaza wazi wazi ktk VITA YAKE YA KUCHUMA ATAKAYE MUWEKEA TUTA NI MSALITI!
Lisu aliweka tuta la shaba ambalo jiwe asinge toboa!
 
Ushahidi wa mazingira kwa sababu mpaka leo upelelezi haujafanyika.
Wewe unatarajia Police wakuletee taarifa ya uchunguzi na upelelezi wao humu mitandaoni?

Magufuli kama amiri jeshi, anaweza kutoa kauli kukemea usaliti.

Lakini iweje Lissu ajihisi hotuba ile ilimlenga yeye?

Kuna usaliti gani anaoujua aliudanya, hadi kuhisi alikuwa akilengwa yeye?
 
..Samia alimuita Mbowe Gaidi na akampeleka mahakamani.

..Ushahidi dhidi ya Mbowe uliwasilishwa na kila aliyefuatilia alijua nani mkweli.

..Kama Magufuli alikuwa na ushahidi kwamba Lissu ni msaliti alipaswa kumfikisha mahakamani.

..Maadam hakumfikisha mahakamani basi ni sahihi kusema kwamba madai ya usaliti yalikuwa ya uongo.
 
Back
Top Bottom