Kumbe Kuna Rais wa kiAfrica anayemfunika JK kwa kuwa Titiles nyingi!

kwani askari wanaakili tofauti wajemeni? Mi naona kama wote wanafanana na kwa bahti mbaya afrika mashariki ukiondoa kenya, wengine wote ni wajeshi na ndiyo maana maendeleo afrika mashariki ni hadithi kwa kweli

Duh, hii sasa kali!...
 
Duh!huyo jamaa ni kiboko, interview nzima imejaa neno ambalo wala haliendani na maswali yenyewe, hamna mtu humo.
 
"HIS EXCELLENCY SHEIKH PROFESSOR ALHAJI DR. YAHYA A.J.J. JAMMEH , President of the Republic of The Gambia and Commander-In-Chief of the Armed Forces"

Jamaa katisha kwa kuwa na jina refu kuliko hata wasomi wenyewe waliokaa vyuoni wakaumiza akili anastahili kuitwa TZ na kupewa nishani ya majina na DR. Jkey
 
Sizijui siasa za Gambia, kwa hili naomba kusaidiwa, ila niajabu kwa karne hii nchi kuwa na kiongozi kama huyo na cha ajabu zaidi ni hizo asilimia alizopata katika uchaguzi asilimia 98, najua katika Afrika tuna tatizo la kutokuwa na uchaguzi huru na wa haki ila asilimia 98, na Rais mwenyewe huyo basi Africa and Africans have long way to go.....
 
Luteni Kanali DR. Jakaya Khalfan Mrisho Kikwete - Rais wa Tanganyika, Tanzania na Amiri Jeshi mkuu.
 
Hawa ndiyo viongozi wetu, vilaza. Inanikumbusha: His Excellency President for Life,Field Marshal Alhaji Dr. Idi Amin Dada, VC,DSO, MC CBE(Conqueror of the British Empire).
 
hapana cheo cha Rais wetu ni zaidi, ni Mh.Mwenyekiti Rais Amiri Jeshi Luten Kanali Dr Jakaya Mrisho Kikwete.
 
duuh! kuna mapresident vilaza kwelikweli sasa sijui wananchi wake watakuaje?
 
Kajamaa kaliingia madarakani kakiwa kakijana ka miaka 27 kakiipindua serikali lakini sasa kanaonekana kamelewa.madaraka. Mwezi uliopita nilikutana na jamaa wa Gambia akaniambia serikali ya Jammeh ilifanya siri siku ya uvhaguzi hadi ikabaki.wiki moja ndio ikatangazwa siku ya kupiga kura na hivyo wapinzani kuruhusiwa kufanya kampeni kwa wiki moja tu!
 
Kajamaa kaliingia madarakani kakiwa kakijana ka miaka 27 kakiipindua serikali lakini sasa kanaonekana kamelewa.madaraka. Mwezi uliopita nilikutana na jamaa wa Gambia akaniambia serikali ya Jammeh ilifanya siri siku ya uvhaguzi hadi ikabaki.wiki moja ndio ikatangazwa siku ya kupiga kura na hivyo wapinzani kuruhusiwa kufanya kampeni kwa wiki moja tu!

Mkuu, Inawezekana ikaqa kweli maana jamaa alisema kwa maendeleo aliyoyaleta Gambia, haoni sababu za kuangaika kupiga kampeni. Na Wananchi wa Gambia watakuwa wapumbavu iwapo hawatomchagua. Aisee! Jamaa anajiamini sana.
 
Back
Top Bottom