Kumbe kina Invisible tuko wengi.......!

Kumbe kina Invisible tuko wengi.......!

hiyo deja vu ndo nini ielezee basi,haya mazingaombwe kwa kweli,tuseme unakua umeitwa na Mungu au,Mtambuzi elaborate mo pls




Kuna wakati unakuwa mahali, halafu unahisi kwamba ulishakuwa mahali hapo kabla, na pengine ukiwa na watu wale wale. Lakini, kwa unavyojua, hujawahi kuwepo hapo, wala kuwa na watu hao.

Hali ya uzoefu huu kufahamika kitaalamu kama Déjà vu. Kama nilivyosema awali kwamba, unakuwa katika sehemu ngeni unashangaa kuona kama kwamba, ulishawahi kwenda sehemu hiyo huko nyuma.

Unaonana mtu kwa mara ya kwanza lakini unapata mawazo kama uliwahi kuonana naye huko nyuma. Hiyo ndiyo Déjà vu.

Neno Déjà vu, asili yake ni lugha ya kifaransa ikiwa na maana kwamba, Tayari nilishawahi kumuona au mahali hapa niliwahi kupaona kabla, ikiwa na maana kwamba mtu anakutana na kitu kipya katika mazingira mapya na anagundua kwamba aliwahi kukumbana na hicho kitu kabla, pengine katika mazingira hayo hayo.

Inasemekana kwamba, mambo haya ya Déjà vu ni ya kawaida. Kila watu saba katika kila kumi wanasema kwamba waliwahi kukumbana nayo angalau mara moja katika maisha yao.

Neno hili Déjà vu lilitumiwa kwa mara ya kwanza na Emile Boirac (1851-1917), ambaye alikuwa mtafiti wa Kifaransa wa mambo ya akili za ziada za watu. Kuna maelezo mengi ya uzoefu huu, kama ifuatavyo: Unakutana na picha kwa mara ya kwanza lakini unagundua kwamba uliwahi kuiona zamani.

Unafika mahali pageni na unagundua kwamba, mahali pale si pageni bali uliwahi kufika kabla. Lakini, kwa akili ya kawaida, unakumbuka kwamba hujawahi kufika hapo. Unaiona sinema mpya lakini unahisi kwamba uliwahi kuiona kabla. Na cha kushangaza ni kwamba unaweza hata kutabiri kitendo kitakachofuata na ikawa kweli, lakini hukumbuki na pengine hujawahi kuiona, kwani ni sinema mpya.

Unakumbana na hali fulani au unafika mahali fulani pageni lakini unagundua kwamba hali ile au mahali pale uliwahi kupaona katika ndoto zako huko nyuma.
Déjà vu pia inaweza ikaonekana katika unusaji, ladha ya chakula, mchanganyiko wa rangi, sauti ya juu au ya chini, kelele au kitu chochote ambacho kinafukua kumbukumbu ya mambo ya zamani.

Mtu mgeni aliye mbele yako uvaaji wake na namna anavyoongea anaweza kukukumbusha mtu uliyekuwa umekutana naye kabla. Baadhi ya watu wanasema kwamba hali hii ya kufanana inaweza kusababishwa na hali ya ubongo kwa wakati huo.

Watu wanaamini kwamba binadamu baada ya kufa roho yake inaingia katika mwili wa mwingine, wanasema kwamba kwa mujibu wa Déjà vu waliwahi kukumbana na hali kama hiyo zamani. Kunaweza kukawa na sababu na maelezo chungu nzima kuhusu Déjà vu.

Haya mambo unaweza kuogopa aisee!
 
Mtambuzi ...kwa 'waafrika' hili la invisibility linaweza kutengezwa pia. Mara kadhaa nimewahi kusikia kuna "wataalamu" wanaweza kutengeneza invisibility kwa ajili ya jambo fulani mahsusi.

Nilisimuliwa kisa hiki na vijana waliokuwa wananisaidia kujenga 'kibanda' changu.

Kuna siku baadhi ya hao vijana waliokuwa wakisimulia na wengine ambao hawakuwapo (jumla kama watano hivi) walikuwa wakifanya kazi fulani ya ujenzi mahali fualani hapa Dar. Siku hiyo walikuwa wakitegemea jioni 'bosi' wao angetokea 'site' ili awape pesa ya kujikimu (siku hiyo hawakuwa hata na nauli ya daladala ya kurudi majumbani kwao!). Kwa bahati mbaya, bosi siku hiyo hakutokea kama walivyo kubaliana/tegemea. Mahali site ilipo na maeneo wanapoishi vijana hao ni mbali na katika hali ya kawaida ni vigumu kutembea kwa miguu. Option pekee kwao ilikuwa ni kutumia daladala lakini hawana nauli!

Kwa bahati kumbe kati yao alikuwepo "mtaalamu"....basi akawaambia wenzake waende kituoni na wapande daladala wote watano na kazi ya "nauli" wamwachie yeye ila kwa sharti moja kubwa na la muhimu.....wakiwa ndani ya daladala (hao vijana wanne) wakae kimya bila kuongea chochote na mtu yoyote na hata baina yao. Mwanzo hawakumwamini wakijua kuwa pengine anatania tu - pengine ana pesa ambayo anaweza kuwalipia nauli wote - lakini walipoona 'mtaalamu' anasisitiza hayo masharti basi wakawaamua ngoja wampe the benefit of the doubt kwa kufuata masharti. Kwa mshangao mkubwa wale vijana wakaona mpaka wanafika kituo wanachoshuka konda amekusanya nauli kwa abiria wengine isipokua wao watano tu! Wakashuka na kutawanyika kila mmoja akipigwa na butwaa kwa yaliyotokea. Kuanzia siku hiyo wakaanza kumwogopa huyo mwenzao kwa maajabu aliyoyafanya
 
Last edited by a moderator:
Hee kumbe @INVICIBLE nae iko siku ataonekana!!!!!!!!!!!! Ngoja nisubirie!
 
Duh hii ishu ya Invisibility mkuu Mtambuzi nilikua siifahamu.
Lakini binafsi nafahamu kitu kinaitwa Deja Vu na Limbo. Mara nyingi sana nimesha-experience effect ya deja vu katika maisha yangu.
Deja Vu ni nini??
nishaiona juu.sorry kwa swali
 
hiyo deja vu ndo nini ielezee basi,haya mazingaombwe kwa kweli,tuseme unakua umeitwa na Mungu au,Mtambuzi elaborate mo pls


Naona mwenzangu jouneGwalu kanisaidia.........
 
Last edited by a moderator:
Deja Vu ni nini??
nishaiona juu.sorry kwa swali

Suprise said:
hiyo deja vu ndo nini ielezee basi,haya
mazingaombwe kwa kweli,tuseme unakua
umeitwa na Mungu au,Mtambuzi elaborate
mo pls

Kuna wakati unakuwa mahali, halafu unahisi
kwamba ulishakuwa mahali hapo kabla, na
pengine ukiwa na watu na mazingira yale yale. Lakini, kwa ujuavyo, hujawahi kuwepo hapo wala kuwa na watu hao.
Hali ya uzoefu huu kufahamika kitaalamu kama Déjà vu. Kama nilivyosema awali kwamba, unakuwa katika sehemu ngeni
unashangaa kuona kama kwamba, ulishawahi kwenda sehemu hiyo huko nyuma.
Unaonana mtu kwa mara ya kwanza lakini unapata mawazo kama uliwahi kuonana naye
huko nyuma. Hiyo ndiyo Déjà vu.
Neno Déjà vu, asili yake ni lugha ya kifaransa
ikiwa na maana kwamba, Tayari nilishawahi
kumuona au mahali hapa niliwahi kupaona
kabla, ikiwa na maana kwamba mtu anakutana na kitu kipya katika mazingira mapya na anagundua kwamba aliwahi kukumbana na hicho kitu kabla, pengine katika mazingira hayo hayo.
Inasemekana kwamba, mambo haya ya Déjà
vu ni ya kawaida. Kila watu saba katika kila
kumi wanasema kwamba waliwahi
kukumbana nayo angalau mara moja katika
maisha yao.
 
Umenifungua macho kuhusu Deja vu, this happens several times to me ila huwa nadhani labda ni hivi viroba tunavyokunywa!? kuna jamaa aliwahi ibiwa pesa bwenini tukiwa form five, zilitafutwa kila kona hazikupatikana, usiku nilivyolala it came to me like a dream nikawa namuona jamaa alivyoiba pesa na mtu aliyempa exactly asubuhi nikaamka na confidence kama what i saw was real nikawaambia jamaa wambane mshikaji niliyemuota na huyo mwingine aliyempa na kweli baada ya kumbana jamaa ali confess exactly kama nilivyoona, hadi tunamaliza shule jamaa wakawa wananiogopa, this happens to me so many times kwa kweli.

Sasa unangoja nini kuwa mjasiriamali?
 
Hii kali Mtambuzi haya sio mazingaombwe?
 
Last edited by a moderator:
houseparty.jpg


Peter wa Gloucestershire huko Uingereza alipatwa na jambo lenye kushangaza sana mwaka 1987. Akiwa katikati ya sherehe ya jamaa yake mmoja alishikwa na haja ndogo. Aliamua kwenda kujisaidia maliwatoni. Nyuma yake kulikuwa na mwanamke aliyekuwa anelekea huko huko maliwatoni {kumbuka sherehe ilikuwa nyumbani ambapo vyoo havikutengwa vya wanawake na wanaume}

Peter alijisaidia haraka na kutoka ili huyo bibie naye akajisaidie. Alimsalimia wakati anatoka chooni baada ya kujisaidia, lakini yule mwanamke hakuitikia. Kwa Peter halikuwa ni jambo la maana sana na hakulitilia manani. Alienda zake sebuleni ambako muziki na vinywaji vilikuwa vikiendelea. Alipofika hapo alienda kukaa kwenye meza ambapo rafiki zake walikuwepo.Alipokaa alichukua kinywaji chake na kuanza kuzungumza na hao rafiki zake. Lakini hao rafiki zake walionekana kumpuuzia. Kila aliposema wao hawakumjibu wala kumtazama, waliendelea tu na mazungumzo yao. Peter alijua wameamua kumfanyia mzaha, hivyo aliamua kunyamaza ili kujua lengo la ule mzaha wao.

Kwa kuwa alikuwa ameshikwa na hamu ya sigara, aliamua kuinuka na kumfuata bibi yake ili ampatie moto awashe sigara yake. Ajabu ni kwamba, alipofika pale kwa bibi yake na kumnyooshea mkono ili ampatie sigara aliyokuwa anavuta ili awashe yake, bibi yake hakuonekana kujali. Peter alinyoosha mkono karibu na bibi yake huyo, lakini bibie aliendelea kucheza bila dalili kwamba mbele yake alikuwa akiona mtu. Peter kuona hivyo alikasirika. Ni mzaha gani wakijinga, aliwaza! Rafiki zake pale mezani wamempuuzia na bibi yake tena anampuuzia, kwa nini? Aliamua kurudi chooni ili ajikague vema, huenda kuna kitu hawataki kumwambia kwamba amechemsha, hasa mavazi.

Peter anasimulia: Nikarudi chooni, kufika namkuta yule mwanamke bado anasubiri pale mlangoni labda akiamini kwamba, labda sijatoka humo. Nilipomuona bado anasubiri, nilikumbuka kwamba, nilipotoka nilimsalimu na hakuitikia. ‘Yule mwanamke aligeuka na kuniona. Aliponiona alishtuka sana,' ‘kumbe umeshatoka wala sikukuona, ningejikojolea nikiwa hapa hapa,' yule mwanamke alisema kwa mshangao'

Peter alisema alipoenda tena sebuleni rafiki zake na bibi yake walimuuliza alipokuwa muda wote huo. ‘chooni ndio ukae mwaka mzima?' Walimwambia. Anasema, alipowauliza kama ni kweli hawakumwona, walimwambia, hawakumwona. Aliwaeleza kilichotokea na wakabaki wameshangaa.

Je, wewe imeshakutokea hali kama hiyo? Kama bado au kama hujawahi kuisikia , haina maana kama haipo. Hiyo ni hali yenye kuwatokea watu kwa idadi ya kutosha. Tofauti iko kwenye kiwango tu. Wengine huwatokea kwa muda mfupi sana, kama sekunde tano au kumi na wengine hata dakika tano au zaidi, kama ilivyotokea kwa Peter.

Ni hali ambayo mtu anapoteza uwezo wake wa kuonwa na wengine. Mtu anaamini kwamba wengine wanamuona kama kawaida, wakati wala hawamuoni. Hawamuoni mwili na wala hawasikii sauti yake. Hali hii ambayo kitaalamu hufahamika kama invisibility, huwatokea wengi pengine hata ukiwemo wewe, bali inakuwa vigumu kung'amua kwa sababu unaweza kutafsiri kama dharau. Kwa mfano, kuna siku nilikuwa ninampa kondakta wa basi la daladala nauli, nikaona hapokei, bali anapokea za wengine tu. Kuona hivyo nilikasirika sana, na kuacha kumpa. Nilishuka kituo kinachofuata nikiwa nimenyoosha mkono ili achukue pesa zake, lakini wala hakunitazama, alikuwa anawadai wengine tu.

Kwa sababu naijua hii hali ya invisibility, sikushangaa sana, nilitabasamu. Kwa asiyeijua ataitafsiri kwa njia mbali mbali na hivyo hatajua ukweli. Kuna wakati mtu anakwenda hotelini, halafu anakuta wahudumu wote wanampita tu , hadi baada ya dakika fulani, kama vile wahudumu wanatoka usingizini ndio wanamwona na kumfuata. Mwingine anaweza hata kufoka, lakini wahudumu wanaonekana hawamjali , kumbe hawamwoni.

Hivi ni kitu gani kinatokea hadi mtu haonekani? Hilo ni swali ambalo bado halijapatiwa jibu. Lakini, huenda Wajapani watatoa jibu hivi karibuni, kwani wamegundua tayari.


Katika gazeti la Jitambue iliwahi kuandikwa. Hiyo habari ilikuwa katikati ya Jiji la D,salaam. Hebu itafute utuweke!
 
Mtambuzi, hakika unakumbusha zamani sana na makala zako hizi.
Kwenye gazeti la jitambue lililokuwa likimilikiwa na Bwana Munga Tehnani ndiko niliisoma makala hii kwa mara ya kwanza.
Nakutakia kila la kheri uendelee kutujuza mambo mbalimbali
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom