Kumbe inawezekana

Kumbe inawezekana

iMind

Platinum Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
3,228
Reaction score
5,522
Tukiwa tuna karibia kumaliza mwaka, nashukuru mungu pamoja na malengo yangu mengi katika mwaka 2014 nimefanikiwa kutotoka nje ya ndoa.

Nilikuwa nachepuka na kuna kipindi nilifika kuwa na michepuko mi nne kwa wakati mmoja.

Baada ya mikwaruzano mingi na mama watoto ilifika mahali nikajihoji kupitia halmashauri ya kichwa changu. Je michepuko ni dili? Mwaka huu niliazimia kuweka pembeni michepuko na hadi sasa nashukuru mungu nimeweza ikiwa zimebaki siku chache kumaliza mwaka. Mara ya mwishi kuchepuka ilikuwa tarehe 20 Dec.

Kiukweli nilidhamiria na kuamua kujirekebisha. Nilikiwa na hali mbaya, migogoro isiyoisha, vile vile kutumia pesa nyingi kuchepuka. Nikajiuliza hivi wanawake wooote hawa nambao nilisha toka nao nimepata faida gani? Sana sana niliona hasara tu. Nilikuwa napoteza sehemu kubwa ya mapato yangu kuchepuka.

So niliamua kuachana na michepuko na kufanya yafuatayo.

1. Kuongea na mke wangu na kumuomba msamaha.

2. Kuwekeza kwa mke wangu. Kuhakikisha kuwa kila anacho hitaji anapata. Hasa katika mambi ya mavazi na urembo.

3. Kuzungumza na mke wangu kuhusu mambo ya 6x6. Kuvunja ukimwa na kuwa huru.

4.kuhakikisha kuwa mara nyingi ninapotoka nina toka na mke wangu.

5. Kujua udhaifu wa mke wangu na kujaribu kukubaliana na upungufu huo. Ikizingatiwa na mimi nina upungufu. Kuzungumza pamoja kuliwezesha kila.mmoja kutambua upungufu wake.

Mara ya kwanza nilikuwa kama na pretend vile, lakini slowly ikawa tabia na mwisho wa siku nikazoea.

Nikitoka kazini break ya kwanza home, kama nikinywaji nakunywa home au tunatika wote kwenda glosary ya karibu.

Nikisafiri kikazi zaidi wiki moja anakuja weekend especially kama sehemu yenyewe inafikika kwa ndege. Ni gharama kumlipia return ticket lakini kuna unafuu kuliko ku ji engage kwenye uhusiano wa nje.

Slowly nilianza kuzoea ma sasa nina mwaka mmoja sijachepuka.

Ninaandika siyo kujisifu bali kujaribu kuwajisha wanaume wenzangu kuwa it is possible.

Pengine inategemea na mke uliyenaye lakini ukweli ni kwamba nyama ni ile ile kinachotofautisha ni mapishi tu. Kikubwa ni utashi

Chukua hatua 2015.
 
Mara ya mwisho kuchepuka ni juzi??leo unaleta feedback?hongera!!ila nadhani upo mapumzikoni zaid...
 
Mara ya mwisho kuchepuka ni juzi??leo unaleta feedback?hongera!!ila nadhani upo mapumzikoni zaid...
Ana mwaka..meaning aliacha last yr 2014.

Hongera bwana iMind ...tulia msije mkauana ma magonjwa. Plus, maisha yanakuwa rahisi na ya furaha sana pale unappjifunza kuridhika na kuthamini kile ulichonacho. Ni kiasi tu cha kukifanya kiwe vile unavyopendelea.

GOOD LUCK!!
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana mkuu kwa kujitahidi kuzikimbia anasa. sasa bakia NJIA KUU, i hope haina 'foleni'
 
All the best may god protect your ways towards the destination!
 
mmmh hivi kumbe ndo mwafanyaga!!!!

haya hongera kwa uamuzi mzuri

Hapo kwe urembo na mavazi ndo nlipoona teh

Kama namuona vile mkeo anavyobadili mavitenge mares wigi
Heheeee roho yake kwaatuu!!!
 
Mmmmh mwanaume?umeachana na michepuko? aseee ww wa kipekee hongera...
 
mmmh hivi kumbe ndo mwafanyaga!!!!

haya hongera kwa uamuzi mzuri

Hapo kwe urembo na mavazi ndo nlipoona teh

Kama namuona vile mkeo anavyobadili mavitenge mares wigi
Heheeee roho yake kwaatuu!!!

Hadi nkatamani kuwa mkewe....:becky:
 
Hivyo eeh? Ngoja na mimi nijaribu nione kama ntaweza..
Cc Honey Faith
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom