BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,766
- 23,230
Hongera kwa kujifunza
Mkuu kama nilivyoeleza hapo awali kwenye paragraph ya mwanzo binti alionekana kuwa na dharau na jamaa na dizaini kama alitaka kumtawala , mchizi akaona asiwe mnyonge ilibidi siku moja amtie mbata na hapo ndo ikawa mwisho wao.Na kwa ghafla sana akanikubalia ombi langu lililodumu yapata miezi 6 tena kwa kasi ya ajabu sana.Kumbe lengo lake amkomoe jamaa.Nilihuzunika sana baada ya kuja kupata ukweli huu.
Cha msingi ni kuangalia kama wewe unampenda na yeye anakupenda. Swala la kuangalia alimfanyia nini fulani sio hoja kwa sababu mtu hufanyiwa kadiri ya matendo yake mwenyewe. Kama jamaa alikuwa na dharau na wewe huna unategemea nini? Watu hatufanani shilingi kwa shilingi tunatofautiana na utofauti wetu ndiyo unatufanya huyu kumpenda yule na yule kumchukia huyu. Inawezekana alichonacho huyu yule hana ndiyo dunia. Kumwacha mpenzi kwa makosa aliyomfanyia mtu mwingine na wala sio wewe ni uchanga wa mapenzi. Ulimuonea bure mpenzi wako. Kama kule alikereka na akaamua kutafuta kivuli kwako na wewe ukakata mti ni ukatili usio kifani.