twende kazi
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 1,520
- 461
Wana MMU mambo vipi?
Kuna nyakati nilipata mkasa mmoja wa kusikitisha sana.Ni kuhusu mrembo mmoja ambaye nilifukuzia takribani miezi sita bila majibu ya kueleweka lakini siku ya siku alikuja kunasa kiulaini sana mpaka nikaogopa.Yani alikuwa anajiachia huyo na outing nyingi za hapa na pale.
Nikajiona nimependwa kumbe nilikuwa natumika kumrusha roho njemba yake ya zamani ambayo ilimpenda sana na waliachana sababu manzi alikuwa na dharau mchizi hakuwa na kazi na kuna siku jamaa alimpiga kwa sababu iyo iyo na ndo ikawa mwisho.Yote haya mimi sikupata kuyajua.Nilikuwa napitishwa mbele ya jamaa mimi pasipokutambua.
Siku ya siku jamaa akanitolea uvivu mbele ya yule binti kwenye mgahawa flani hivi akaanzisha fujo ya maana sana mtu mzima nikahisi kama nimefumaniwa vile bahati nzuri hakuweza kudhuru mtu ila alivunja chupa na kutupa chini kwa hasira.Jamaa alitoa shits sana nikamtuliza nikamuuliza kulikoni mkuu hakunijibu kitu kwa dakika kadhaa alilia kama mtoto mdogo vile kisha akaondoka kiukweli nilimuonea huruma sana.
Kikubwa kwenye maneno mbovu yake alikuwa analalamika bora demu angemuacha kuliko kummimina kwa sababu mfukoni hana kitu ila jamaa alionekana ni mstaarabu na mwenye malengo na binti alikuwa na upendo nae tatizo lilikuwa ni iyo migogoro isiyokuwa na kichwa wala miguu.Na binti yeye alikuwa anasema yeye aliniona wa nini wenzake wanawaza watanipata lini.Hii kauli ndo iliniboa sana na kuona kabisa huyu manzi alikuwa na roho ya kisasi na sio upendo wa dhati.
Uamuzi nilioufanya nikampiga chini yule binti na kumwambia alikurupuka sana kuja kwangu alipaswa kuwa mvumilivu kwa jamaa na maisha yaendelee.Jamaa naye nilimtafuta nikataka kuwapatanisha ila juhudi zangu zikashindikana.Ninatamani warudiane mbele ya safari.Ila nimejifunza kitu.