everybody
JF-Expert Member
- Oct 30, 2010
- 337
- 103
Tatizo la malumbano yote haya ni majivuno tu hakuna kingine. Hata mimi sion tatizo kwa hao intern kuitwa madaktari (matabibu) wanafunzi. Wangekua wamemaliza uanafunzi wao wasingehitaji uangalizi wa mtu wa kuwafundisha kazi na wangeruhusiwa kwenda kutibu moja kwa moja. Hata mwongozo wa masomo yao unaonyesha kwamba, daktari anasoma mafunzo ya darasani kwa miaka mitano na baada ya hapo anaingia kwenye mafunzo ya vitendo (internship). Sasa malumbano yote yanatoka wapi. Hivi wewe daktari wa intern ukiitwa daktari mwanafunzi unapungua kitu gani? Majivuno kitu kibaya sana... Jitahidini kudai madai yenu ya msingi badala ya kung'ang'ania title ambazo bado hamjazipata.