Magnesium
JF-Expert Member
- Nov 9, 2014
- 317
- 185
Wakuu habari ya jioni? Nimekaa nikatafakari juu ya utendaji wa Mh. Rais Dr. JPM ndani ya mwezi mmoja na kuona mabadiliko makubwa bila hata ya usaidizi wa baraza la mawaziri na bado mambo yanaenda yakinyooka.. Kuanzia suala la Muhimbili, TRA, TANESCO na Bandari inaonekana wazi kabisa kazi iliyofanywa na Dr. JPM na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa ni kubwa.
Mpaka sasa sijaona pengo la kutokuwepo kwa baraza la mawaziri. Natamani Mh Rais asitangaze hilo baraza la mawaziri hadi mwakani. Peke yake atosha. Hao mawaziri wakiingia huenda wakaanza kuleta mlolongo mrefu wa utatuaji wa matatizo ya wananchi.
Kingine kinachonifurahisha ni Mh Rais kutosafiri nje ya nchi tangu ameapishwa. Inaonesha jinsi gani yuko makini na matatizo yetu zaidi kuliko ziara za nje. Kwa hili nampa Dr. JPM heko. Cha msingi Watanzania tumuungo mkono na kumtia moyo ikiwa na pamoja na kumuombea aendelee KUTUMBUA MAJIPU...