Kumbe hata ajali ya meli zanzibar imesababishwa na chadema

Kataa ukubali lakini ajali ya Meli Zanziba imesababishwa na CHADEMA. Kwa umahiri wao wa kupeleka hoja zenye maslahi kwa nchi kumekifanya chama hiki kipendwe sana na wananchi na kuifanya CCM kuwa na wakati mgumu kwa wananchi na sasa kazi ni moja tu kwa CCM kuingamiza CHADEMA badala ya kutatua kero za wananchi kwa kuwa hawako radhi kuachia nchi. Nahili ni tatizo la kudumu kwa kuwa sasa hivi akili ndogo inaongoza akili kubwa. Nani anabisha kuwa ajali ya Zanzibar haijasababishwa na CHADEMA.


Ukitaka uhakika muulize Mhe Stella Manyanya.

Hilo nalo neno?! kumbe ndio maana hata Ana makinda alikuwa anasita kuahirisha kikao cha bunge akidhani CDM ndio imezamisha meli, duh they are running scared indeed!!!!
 
bt kwenye ajali kama hizi tuwe 2namshrikisha mungu zaid na sio vyama! Kwani huko ni kulaumiana pasipo sababu!
 
Hili suala halipaswi kujadiliwa hapa kwa sababu kesi iko MAHAKAMANI! Alhaj Kovu amemsomea mashtaka kapteni wa meli (ambaye kwa bahati nzuri alipona) mahakamanii Kisutu leo asubuhi. Kwa mujibu wa Katiba yetu tukufu, ni marufuku kujadili suala ambalo liko mahakamani!!!!
 
Kweli CHADEMA inahusika sababu hata Bahari jana ilikua imevaa Gwanda.
Halafu ilikuwa inaandamana bila kibali cha polisi na kibwagizo cha "peoplesss...............!" Sasa meli ikaingilia msafara polisi wakaifyatulia mabomu ya machozi abiria wakaparangana ikakosa balance
 
Halafu ilikuwa inaandamana bila kibali cha polisi na kibwagizo cha "peoplesss...............!" Sasa meli ikaingilia msafara polisi wakaifyatulia mabomu ya machozi abiria wakaparangana ikakosa balance

Hahahahahahaha......... Nasikia walishauriwa kutumia maji ya pilipili ili abiria wajirushe kwenye maji wenyewe. Lakini polisi hawakufanya hivyo.... Toba....!!!!!
 
Halafu ilikuwa inaandamana bila kibali cha polisi na kibwagizo cha "peoplesss...............!" Sasa meli ikaingilia msafara polisi wakaifyatulia mabomu ya machozi abiria wakaparangana ikakosa balance
Hilo la CHADEMA kuhusika halipingiki kabisaa,

Kwani meli ilipopata thoruba si ndio hao waliopanda juu ya meli na kuifanya ipinduke na mjue Kova anajiandaa kutuletea picha nyingine ya mwisilaam wa CHADEMA aliyekuwa mmoja waliopanda juu ya meli na kuifanya ipinduke akitubu msikitini.

Huku Manyanya na Nchemba wakiifanyia documentary Bungeni baadaye.

Poleni sana Watanzania wenzetu mliopoteza wapendwa wenu, Mungu awape nguvu kipindi hiki kigumu.
 
Nahisi kama wachangiaji wengi hamjamuelewa huyu mtoa maada, yule mama anaejiita Engineer akisoma hapa na hakika ataona aibu sana of course hata magamba wenzie.

Kwani kuna ubishi sikuhizi kila kitu CCM wanasingizia CDM, ukifanyika uzembe wa kwao, watasema CDM, mliosoma Fasihi, mweleweni mtoa maada, ana maana tofauti na mnavyo mfikiria, mi namuunga mkono, this why Riz1 amekuwa wa kwanza kutoa comment tena za kuomba hii iondolewe!
 
jifunze kuthamini muda wako, utani mpaka kwenye maisha ya watu. watu wanamachungu kwa kuwapoteza ndugu zao wewe unaleta utani. funguka...wanahusika au hawahusiki vipi.
 
Yaani wakuu mara nyingi huwa wanajamvi tunajikuta kumesahau kuchangia thread husika na kuanza kushambuliana wenyewe kwa wenyewe, ni vema tuchangie hoja ili kuleta manufaa na kutoa ufafanuzi pale tunapoweza kwa manufaa ya nchi hii. otherwise hayo hayatusaidii kwakweli
 
Back
Top Bottom