Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Mh Rais Magufuli alitoa tamko kuzuia mashindano ya kisiasa kwa nia njema kabisa atekeleze ilani ya chama chake kwa kuchapa kazi kama kauli mbiu ya chama chake inavyosisitiza"hapa kazi tu"
Lakini hakuzuia mikutano ya kisiasa kwa nia njema pia akitaka pasiwe na vurugu wala mwingiliano wa mikutano hiyo. Hivyo wabunge walipewa nafasi ya kuweza kunadi sera za vyama vyao na kuwaeleza wananchi waliowachagua kuwa nini wamefanya.kwenye majimbo yao tena kwa kufuata utaratibu.
Kumbe hata kwa wenzetu ambao huwa wanajinadi kuwa eti wanademokrasia iliyokomaa mshindi wa urais akishapatikana huwezi kumuona, mpinzani ananza kuzunguka nchi nzima kuanza kuleta upinzani katika kutekeleza ilani ya chama tawala.Mfano hata Usa hivi sasa ni D.Trump tu ameachiwa ulingo huo mpaka amalize muda wake.
Hapa nchini Tokea zuio la upinzani wa kisiasa na sio zuio la mikutano ya kisiasa litolewe vyama vya upinzani vinalalamika kuwa ndio sababu ya kuporomoka kisiasa na kukosa mvuto kwa wananchi.
Wanasahau kabisa kwamba zuio hilo lilikuwa na nia nzuri ya kuwapa wananchi fursa ya kufanya kazi zao kama uvuvi au kilimo na biashara,kuliko kusubiri helkopta kuanzia asubuhi hadi jioni.
Pia aliyepo madarakani ametumia fursa nzuri aliyopewa na wananchi kudhibiti ubadhirifu,rushwa ,kutekeleza miradi kama ujenzi wa vituo vya afya na na hospital,kujenga barabara na madaraja n.k hivyo amejijengea imani kubwa kwa wananchi.
Hivyo kuleta kisingizio ati wamezuiwa kufanya mikutano ndio sababu ya kuporomoka sidhani kama ni kweli.
Ukweli hauna chama,na mimi si mwana CCM ila nasema kweli tu.