Kumbe freemasons ni watu poa sana!

Mimi nachotaka kujua nikwamba watu waliochukuliwa na freemason wanakwenda wapi?

Nikiunganisha na kanumba na sharo
Wapo mkuu na duniani huwa wanarudi sana tu ila huwa wanaonekana kwa watu wachache, then wanarudi kuzimu maana hawana tena uhuru, kuna kipindi taarifa fulani zilikuwa zinavuma fulani kaonekana sehemu fulani sijui ananunua vocha, sijui anafanya vile ndio kuonekana kwao then wanapotea, sio kwamba ni kiki mkuu, lisemwalo lipo kumbuka, duniani huja kwa kazi maalum ambayo haina faida binafsi tena kwao bali kwa utawala waliouchagua enzi za uhuru wao walipokuwa wakitumika kwa faida ya utajiri na mafanikio ya muda mfupi. Kwa habari ya kazi wanazofanya nafikiri hapo tuparuke kwanza
, ila naimani umepata mwanga fulani.
 
Hivi mkuu si bible inasema kabla hawajafanikiwa kuuteka ulimwengu wote si ndo hapo mwana wa Adamu atarudi kuwatwaa watakatifu?au huu mpango kazi wao wa kutawala ulimwengu wote ni kabla ya Yesu kurudi?
Inaonekana una details baadhi mkuu wala hujakosea, Mungu wa haki (yeye asiye na kikao na wanadamu) hataruhusu watoto wake aliowagharamia kwa gharama kubwa ya kafara ya damu ya mwanae mpendwa wakumbwe na janga la utawala huo dhalimu na ni kwa sababu ya hao watakatifu wake ndio maana anazuia (maana yeye ndie anazuia mipango yao mingi isitimie kwa sababu ya watoto wake anaowapenda ambao bado wapo duniani ,Maana huyu Mungu wa haki anahuruma sana na maisha ya mwanadamu anaweza kuponya au kuzuia mabaya yasilipate jiji zima la Dar es salaam kwa sababu ya mtoto wake mmoja au wawili tu waaminifu) sasa wakishaondolewa hao watakatifu wake hana tena sababu ya kumfanya azuie na kama isingekuwa kuzuia kwake walikuwa wameshaazimia kuiteka mapema haraka iwezekanavyo,usione hii nchi au bara au dunia nzima tupo salama ukafikiri ni amani, huenda kuna kakikundi ka watu waaminifu wasiozidi hata mia moja ndio sababu ya amani ya raia zaidi ya million 60, lakini sababu ya upofu wa roho kakikundi haka kadogo kanaonewa na kupingwa na kuteswa vikali, maana ndio sababu ya amani na haki hii kiduchu iliyobaki kwenye Dunia au nchi lakini baada ya unyakuo (sijasema kurudi mara ya pili), namaanisha unyakuo kwanza atakapochukua walio wake, na wengine kuuwawa pasipo haki (kudhulumiwa uhai wao kabla ya siku zao), watakapoisha tu kuonekana katika uso wa nchi, wale watakao baki "watajiponya kwa gharama zao wenyewe," namaanisha ataondoa nguvu zake za kuwazuia hawa mabwana na ndipo watakuwa na mamlaka kamili, ni kipindi cha kuogofya sana hicho usiombe kikukute. Ndio maana ni bora kuwa mwaminifu mpaka kufa hata kama ni kwa kuonewa, kuliko kutetea maisha yako halafu kikukute hicho kipindi, maana ndio kipindi watu watakitafuta kifo hawatakiona, watatafuta mauti, mauti nayo itawakimbia, kwa hiyo mateso yapo maumivu yapo,vilio vitajaa kila kona lakini no kufa, ni mateso mwendo mmoja, (Ndio maana ya yale maneno "yeyote atakaye kuyaponya maisha yake katika ulimwengu huu wa sasa atayapoteza, na yeye atakaye yapoteza maisha yake kwa ajili ya jina langu katika ulimwengu huu wa sasa atayapata hata uzima wa milele"), Maana itafika kipindi patabana kote, hutaweza kuuza wala kununua, hutapata huduma yoyote ile ya kibinadamu, kibenki, au kiserikali isipokuwa umemsujudia Master kwanza, ndio kipindi imani za watu zitapimwa na kujaribiwa kama mtu anavyopepeta ngano, ndio itajulikana wenye dini au wenye imani kina nani watasimama, maana kuna watu wameshika dini kama vile ndio Mungu wao, lakini hawana imani ya kile wanachokitetea, sasa ndio itajulikana, kati ya waabudu halisi na wazugaji, hapa hakuna wa kumtetea au kumsemea mwenzake hata mchungaji wako au imamu au mzee wako wa kanisa na yeye ban itamhusu hakutakuwa na msimamo wa pamoja eti sisi dhehebu fulani tunaamua kufa kwa njaa au kukosa huduma muhimu ili tusimsujudie Master, wengine waoga na ni viongozi wa juu, akiona mtoto wake hajala siku mbili roho inamuuma, akifikiri uhai wa mtoto wake ni bora kuliko utii kwanza kwa Mungu, (jifunze kwa Ibrahim), ndio utajua amri ya Mwenyezi Ina thamani kuliko uhai wa mtoto unaempenda, maana alikuwa tayari hata kuyaangamiza maisha ya mwanae mpendwa kwa mikono yake mwenyewe, kwa ajiri ya amri ya Mwenyezi, ndipo Mungu alipomheshimu zaidi na kumjalia uzao kama mchanga wa bahari, ki ukweli kumlingana Bwana inahitaji kujikana nafsi na kuubeba msalaba wako mwenyewe halafu unamfata kila aendako, kuwa tayari kwa lolote kwa chochote kwa ajili ya jina lake halafu uone kama utapoteza chochote, sio porojo tu baada ya kushiba ugali ,hutapoteza kitu maana upendo wake kwa wanadamu aliowaumba haupimiki na anahuruma sana kuliko sisi tunavyohurumia familia zetu na wapendwa wetu, ila ana wivu sana anapoona ibada yake inaibiwa na kupelekwa pengine. Atakaevumilia mpaka mwisho ndie atakae okolewa, Amri ni moja haigeuki kuwa mwaminifu mpaka kufa ( sio mpaka uzidiwe au uzimie au uteseke au ukatwe mguu au mkono ni mpaka kufa).
 
Na Mwana wa Adam alikuja ulimwenguni humu mara mbili mara ya kwanza kuukomboa ulimwengu na mara ya pili atakuja kuuhukumu ulimwengu pamoja na mungu wa dunia hii(Master). Kwa hiyo hizi vurugu zote ni kabla hajarudi mara ya pili, maana akiisharudi hakuna maisha tena duniani ni either Jehanum or heaven and after that zitaumbwa mbingu mpya na nchi mpya ambayo haki yakaa ndani yake ndipo andiko litatimia "wenye haki watairithi nchi", sio nchi hii ya sasa ni ile mpya idumuyo milele, maana sharti ni moja kila lililotabiriwa na manabii na waonaji wa Bwana lazima litimie, kama neno lisemavyo mbingu na nchi ya kwanza iliwekwa akiba kuangamizwa kwa maji (siku za nuhu), lakini hizi za sasa zimewekwa akiba kwa ajili ya moto usiozimika.
 
Among the top secret society in the world hiyo ni mojawapo. Sasa nashangaa haya machapisho mnayabuni kutoka wapi
Hamna siri ya kuanzia watu wawili siri ni ya nafsi na Muumba wake ila ukiisha zungumza hatuiti tena siri, sema tofauti itakuja kwenye level ya kamba yako ku access hizo information
 
Nasikia HUWA hamsajiri member maskini?
Nafikiri umasikini ni nadharia pana sana sijajua unamaanisha umasikini upi, maana hata ukipungukiwa maarifa unakuwa masikini wa fikra, na ndio maana mganga wa kienyeji anakaa kwenye kajumba ka nyasi lakini anamtengenezea mtu dawa ya kwenda kutengeneza mabilioni, sio kwamba ni mjinga hajitambui anaelewa nini anafanya, watu wa rohoni wanaelewa jinsi gani fedha au majumba au magari ambavyo hayana thamani katika ulimwengu wao, maana kwao chenye thamani ni nguvu na uwezo, akiwa na hivyo tu vilivyobaki vya mwilini kuvipata ni kugusa tu, ila nachojua yeyote anaweza sajiliwa/kujiunga ilimradi ibada kwa Master tu na sadaka zitolewe kwa wakati na kulinda kiapo na mkataba alioingia, maana mpaka kuna mikataba wanasainishwa tena yenye masharti magumu (ingawa sio wote), ndio maana saa hizi wanatafuta watu wa aina zote, ila sio kwa matangazo kama ninavyoona sehemu nyingi, sijui mabango kwenye nguzo za umeme/matangazo sijui namba zetu utupigie ukiona hivyo ujue hao matapeli hakuna freemason hata mmoja hapo huwezi kuungwa freemason bila kupelekwa na mtu ambaye tayari yupo kule na mara nyingi lazima awe anakujua wewe ni mtu wa namna gani, namaanisha huenda akawa rafiki yako uliesoma nae ila kwa sasa maisha yake sio ya kitoto, au hata ndugu yako, au business partner, naomba niishie hapa maana sifundishi jinsi ya kujiunga ila nakuelekeza ogopa matapeli mjini, kuzimu huwa haijinadi kwa matangazo ya hivyo na hawasajiliwi kwa kujaza form sijui wapi ni unapelekwa mzima mzima na mara nyingi hutajua, wanakujaga kutambua tayari wameshanasa, ingawa wengine huwa wanajua kabisa ila most huwa inawakuta tu tayari yumo na hakuna namna ya kutoka.
 
Wabongo kwa kutunga na kubunibuni mambo utawaweza.
Sawa mkuu, kama shetani ni mwigizaji siku sawa, lakini ni kama yule yule basi tambua hata kama hujaambiwa zipo kafara hutolewa Master hanaga kitu cha bure, vyote vinalipiwaga kwake tena kwa gharama kubwa ya nafsi za watu wasio na hatia, ambazo hazikuwa zimemshika vizuri Mungu wa haki, asiye na kikao na wanadamu.
 
Hamna siri ya kuanzia watu wawili siri ni ya nafsi na Muumba wake ila ukiisha zungumza hatuiti tena siri, sema tofauti itakuja kwenye level ya kamba yako ku access hizo information

Nimekupata mkuu
Nimeelewa zaidi sasa hata sababu ya baadhi ya wachungaji kuwa walivyo
Inaelekea wewe ni mpakwa mafuta wa Bwana mkuu,nishushie upako!
 
Halafu wakulu kumbukeni vyama vya waabudu shetani sio freemason tu, vipo vyama kama 11, kama sijasahau ila kama viliongezwa au kupunguzwa hivi karibuni sifahamu ila kuna hiki cha hawa mafia waliovaa ngozi ya kidini ila ndani ni majitu ya kutisha na duniani huonekana kama wachamungu hatari lakini kumbe ndio devil worshipers wa viwango vya lami
,"Jesuits"
, jina lisikuchanganye ukadhani kuna uzima hapo maana hata nabii wa mchongo hawezi kufungua kanisa akaliita kuzimuni church hatapata watu atajiita kajina kazuri kakutia moyo na matumaini lakini hakuna kila kitu, mfano Arise and shine ministry, ila ni mfano tu ndugu zangu mtajijua mkichukulia serious
,mi nimesema mfano tu sasa wewe jiongeze mwenyewe lakini mimi nimetolea mfano "halisi
" ili uelewe, ila tuachane na hayo kwanza, hata hivyo uzi unahusu freemason tu au "nasema uongo ndugu zangu" in the late voice
.
 
Aisee inatisha,!!!. Vipi kuzimu kupo ki mazingira kama ya duniani au kunaonekana vipi na hao ndugu zetu waliochukuliwa wanalala na kuishi kama maisha ya duniani?
 
Aisee inatisha,!!!. Vipi kuzimu kupo ki mazingira kama ya duniani au kunaonekana vipi na hao ndugu zetu waliochukuliwa wanalala na kuishi kama maisha ya duniani?
Muonekano wake ni wa ajabu na wa kitofauti sana na dunia yetu, ukibahatika kupaona ndio utaelewa Dunia yetu kumbe inapendeza na ni nzuri inavutia hata kwa kutazama tu ukiachilia mbali kuishi, ukiona Nuru ya jua, mwezi, wanyama, viumbe hai, maporomoko ya maji,mimea hai, miti,milima ,mabonde vyote hivi kwa pamoja huonesha na kueleza upendo wa Mungu kwa wanadamu, na ukarimu wake kwa viumbe alivyoviumba kwa jinsi vinavyopendeza hata kwa kutazama ndio maana ya lile neno" Bwana Mungu akaona na tazama ni vyema sana " hii ni kumaanisha hata Mungu mwenyewe baada ya kuumba aliona nafsini mwake kweli nimeumba kitu kizuri, lakini kule hapakutengenezwa Mungu akiwa anafurahi

Ilikuwa ni baada ya vita kuu mbinguni Ndio mmoja wa wale wakuu wa mbele, Kerubi afunikaye , nyota ya asubuhi, mbeba Nuru/Light bearer (Lucifer) aliposhushwa,(kutupwa) kama umeme mpaka pande za mwisho za shimo, na jeshi lote lililokuwa upande wake na huko ndio kukawa makao yao mapya hakuna uumbaji wowote wakufurahisha huko, anga lake muda wote ni kama lina mawingu mazito meusi meusi, hakuna nuru kama vile ya jua ila mwanga upo sasa sijajua huwa unatoka wapi, mazingira yake ni kama utusi utusi, hakuna miti, hakuna uzuri kama wa duniani, pamoja na kuwa dunia imechoka, lakini ukilinganisha na kuzimu inavutia bado, lakini kingine cha kushangaza hakuna mchana wala usiku, na ndio maana ukiwa unaenda lazima uwe kama unashuka chini ya dunia, maana ni shimoni, na ukiwa unarudi duniani ni kama unapanda kutoka shimoni maana Dunia ipo juu na kuzimu ipo chini, sasa usiniulize kiaje, juu ya Dunia ni wapi na chini ni wapi, we elewa tu, maana ndio pako hivyo maana mi mwenyewe mpaka leo sijawahi kuelewa kwanini ipo hivyo na inawezekanaje, lakini ndio hivyo ukistaajabu ya kuzimu utayaona ya rohoni. Na kuna malango hapa duniani ambayo Ndio hutumika kuingia au kutokea, mf: matundu ya vyoo, makusanyiko ya maji mengi(bahari, ziwa), visima visivyokauka, mito mikubwa, makaburini, njia panda,kwa wale magwiji hata katikati ya chumba, chumba chochote pale katikati yake sasa ni njia hiyo ila ikumbukwe njia nyingine ni za magwiji tu ya kichawi, kurutu wa kawaida hawezi
, mf hii ya katikati ya chumba. Halafu kuna zile njia maarufu kumbukeni lisemwalo lipo, pale bagamoyo road, kama unaenda... Au basi tu hata hivyo sio sehemu ya mada.

Wengi hawafahamu hata unaposema kuzimu unamaanisha nini, kwenye kiebrania, hutumia neno Sheol kueleza sehemu yenye giza zito lisilo penyeka kirahisi ambapo dead souls huenda, wagiriki wao walitumia neno abyss kumaanisha bottomless pit, yaani shimo kisilo na mwisho lenye giza, lakini kwa jina lake halisi kwa lugha ya wahenga wa kule, panafahamika kama Sheole Mapkzye (inasomwa hivyo hivyo usiweke uzungu wako), tafsiri yake ni mahala pa ufu, au sehemu ambayo vitu vimekufa au vinaendelea kufa, kwa hiyo unaposema kuzimu sehemu yoyote ile jua unaongelea mahali pa ufu, ninaposema ufu haimaanishi hakuna nafsi zinazoishi kule, maana kufa sio kupotea wala kulala, wala kupumzika (pumziko ni kwa watakatifu tu ila ukifa na midhambi yako hakuna kupumzika ndio unaanza maisha mengine ya kuogofya sana, hayaelezeki ndugu zangu acheni dhambi, acheni dhambi nawaambia kwa mara nyingine kule nafsi zinateswa katika viwango vya juu sana vya kuogofya 🥲
, inasikitisha lakini tuendelee kwanza na usidanganywe eti ndugu zako watatoa sadaka kwenye misa uombewe utoke, huo ni utapeli, ogopa matapeli, ukiingia umeingia mageti yake yana minyororo mikubwa na walinzi wakali juu, usidanganywe huwa hatoki mtu kule, kwa kuombewa msamaha na watu wa duniani, matendo yako siku za uhai wako ndio yataamua), ni maisha kabisa mengine huku ukiwa umetengwa na Mwenyezi (Muumba wako) milele, maana kitendo cha kutengwa na Mungu aliye hai ndio kinaitwa kifo, ni kama vile umtenge samaki na maji, au mmea na ardhi, vivyo hivyo mwanadamu aliumbwa ili amtegemee na kumtumikia Muumba wake kama vile maji yalivyo mazingira ya asili ya samaki, akitoka njee ya hapo, hata ikitokea hajafa basi ataishi maisha magumu kupindukia, ndivyo ilivyo kwa mtu, mazingira yake ya asili ni Muumba wake (Mwenyezi) , ikitokea kwa namna yoyote ile akatengwa na mazingira yake ya asili huyo tunahesabu amekufa na kupotea, hata kama bado anatembea ni suala la muda tu atakauka, maana hata samaki ukimtoa majini hafi hapo hapo kuna ka muda katapita akijutupatupa baadae kwishnei,

Ingawa kuzimu siyo sehemu moja tu kubwa ukumbuke, imegawanyika mara tatu, nafikiri tukipata muda tutaendelea katika hizi sehemu kuu tatu ambazo kwa pamoja ndio zinaunda hicho unachokiita kuzimu, maana kuna watu wanafikiri ukishaingia kuzimu hapo hapo utamwona kanumba, sharo millionaire, Lucifer, majeshi ya mapepo, ndugu zako waliokufa, hapana sio hivyo imegawanyika mara tatu ndugu zangu, ipo sehemu ya waliohai ambayo ndio hao wanaoenda na kurudi, lakini ipo sehemu ambapo wafu wote wenye dhambi huenda huko huwa hatoki mtu, halafu ipo sehemu ambapo enzi ya Lucifer ndio imekaa (sijasema Lucifer amekaa nimesema enzi yake, maana yeye mwenyewe yupo kazini duniani) huko ndio kuna yale mapepo mabaya kabisa, na hayajawahi kufunguliwa huko tangu yatupwe na kama yale yakiachiliwa hata dk moja duniani, hatutaiita tena dunia, ila kipindi cha mwisho yatafunguliwa yote sijui itakuwaje kwa watakaokuwepo.

Naomba niishie hapa kwanza siku tukipata muda tutaziangalia kwa undani moja baada ya nyingine na majina yake na kazi zake zote ila hapo juu tu ni dondoo chache kuhusu kuzimu.
 
Heshima kwako mkuu
 
Tunashukuru kaka, na tunasubili kwa hamu hiyo mada...
 
Dah mwamba ulipotaja malango ya kuendea kuzimu na makaburini kunahusika ni kweli

Siku usik moja nililala usingizi kama kawaida,sasa mida ya usiku mnene nlianza kuota lakn sio kuota ni kama nlikuwa nashusika moja kwa moja lakin kwa ufahamu usiokuwa sawa,nlioona naanguka kutoka juu sana naelekea chini na maeneo yale kutoka juu nlikuwa nayajua a to z yaan hakukuwa na errors zozote.Eneo lenyew ni la shule ambayo nlisoma sekondar lakn lilipakana na makamburi.Basi vile nilikuwa nashuka (ilikuwa kama nimebebwa na mtu hivi Mgongoni lakn nlikuwa simuoni)spidi kali sana hadi upepo nilikuwa naufeel machoni na nyumba naziona na kuzitambua vzr kbs.Bwana nkajua tunaangua tunaenda kujibamiza laaahh vile tunakaribia makaburi yale tukalenga kaburi moja lakn badala yake likageuka duara jeusi tiii,na tukapenya katikat ya duara hilo.Muda wote huo tunadrop mi najiskia ok hata hofu sina na hata sijui ilikuwaje lkn sasa wakat tunaendelea kushuka( mle ndani tulikuwa tunshuka straight vilevile lakn ilikuwa ni kama tunapita kwenye pipe fulan).Nisiseme uongo tulufika mahali nkagundua mwendo ulipungua na mahali oale ni kama ilikuwa emptpy space ila giza lilikuwa la ajabu sana.Giza lili kuwa ni kama rangi nyeusi tii bile ilivo.Na hapo aisee nkahisi hali ambayo sjawahi kuhisi kwa kiwango kile.UPWEKE aisee ni upweke ambao hauelezeki yaan emptness,au void naifeel toka ndan ya moyo wangu..nilisikia sauti tofauti tofauti za watu wanalia,nlisika wanawake watoto na wanaume na wengine wanaita jina la Yesu.I was shocked nilitamka YESU WANGU NAOMBA NISAIDIE.Hapo ndio nkajihisi tumeanza kuascend kuja juu hata kabla hatujaibuka nkashtuka nmeloa jasho nahema ovyo ovyo.
The choosen one nisaidie ndg hapo ww unaonaje hili suala.Huwa natafakari sana sipati majibu ni nani alinichukua na kunitisha route ile
 
Uwe unakula na kunywa maji kabla ya kulala. Hayo ni mawenge ya kawaida ukilala na njaa.
 
Hawa ma chalartan wamejaa wengi mno nowadays. Kitu kingine kinacho watambulisha kuwa ni mbwa mwitu ni "Jiunganishe na madhabahu ya mtume au nabii" au mungu wa madhabahu so and so Amefanya.
Mkuu, upi utofauti kati ya hawa secrets society na Occultism?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…