Kwa mara ya kwanza msiba mzito umeisha salama bila kuwepo na habari za udaku. Tulizoea huko nyuma magazeti mengi yalizoea kufanya udaku kwa kukuza story ili yauze nakala nyingi hususani kwenye misiba ya watu mashuhuri!
Ingekuwa zamani msiba wa mkapa usingeisha salama bila habari za magazeti udaku kuweka habari mifano mwa hizi!!
Msiba wa mkapa Vuta Ni kuvute😋😋
Mazishi ya mkapa wingu zito😋😋
Mauza uza yatawala msibani
Kuku afunga njia msibani
Joka kubwa laonekana lupaso
mabomu yazua tafrani msibani
Mganga atinga msibani na ungo
mwewe washiliki mazishi masasi
"Tuliliona Hilo kwa baba wa taifa, Tuliona Hilo kwenye msiba wa Juma Alli Juma, Tuliona Hivyo kwenye msiba wa kanumba na wengine kibao!"