kumbe ccm nao huwa wansusia vikao!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kumbe ccm nao huwa wansusia vikao!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ms Judith, Apr 20, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mali za CCM zazua balaa Moshi

  na Grace Macha


  MGOGORO wa kugombea mali za Halmashauri ya Moshi zinazodaiwa kumilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana ulichukua sura mpya baada ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bernadette Kinabo, kususia ajenda hiyo na kutoka nje ya kikao cha baraza la madiwani.
  Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa nne asubuhi wakati wa kikao hicho maalumu na kuwalazimu madiwani wa CHADEMA kumchagua katibu wa muda wa kuendesha kikao hicho.
  Wakati hali ikiwa hivyo ndani ya halmashauri, nje ya eneo hilo na mitaa mbalimbali ya mji wa Moshi polisi waliweka ulinzi mkali na kufunga barabara kwa kile kilichoelezwa kuwa walihofia vurugu zingetokea.
  Kikao hicho awali kilikuwa kifanyike Machi 31 mwaka huu lakini kilishindikana baada ya Mkurugenzi huyo kukiahirisha kwa kile alichoeleza kuwa kungeweza kutokea kwa vurugu.
  Mkurugenzi huyo ambaye ni katibu wa kikao hicho alitoka wakati walipokuwa wakithibitisha ajenda za kikao hicho ambapo alitaka ajenga namba 7 iliyokuwa inahusu kujadili majengo ya manispaa hiyo yanayokaliwa na CCM isijadiliwe kwani tayari alikuwa na maagizo ya mahakama (court order).
  Kinabo alisema barua hiyo ya mahakama aliipokea siku iliyopita saa tisa alasiri, hivyo akataka kikao hicho kisijadili hoja hiyo, ambapo Meya wa manispaa hiyo, Jafar Michael, aliyekuwa akiendesha kikao hicho aliamua kusikiliza maoni ya madiwani.
  Mwanasheria wa halmashauri hiyo ambaye ni mgeni aliyetambulishwa kwenye kikao hicho, Deograsius Nyoni, aliwasomea madiwani ‘oder’ hiyo iliyoweka zuio la kuhamisha au kuharibu mali kwenye viwanja namba 54 Block BBB na namba 19 Block B, ambavyo vinakaliwa na CCM.
  Alisema shauri hilo linalosikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Stella Mgasha, lilifunguliwa Aprili 13 mwaka huu na bodi ya wadhamini wa CCM kupitia mwanasheria wao, Beth Minde, ambapo mshitakiwa pekee kwenye shauri hilo ni mkurugenzi wa halmashauri.
  Alifafanua kuwa CCM iliomba malalamiko yao kusikilizwa kwa shauri hilo kwa hati ya dharura ambapo mahakama iliyasikiliza Aprili 14, mwaka huu sasa 8 mchana lakini usikilizwaji huo ulifanyika kwa upande mmoja.
  Alisema kuwa maombi hayo ya CCM yaliyowasilishwa mahakamani yalilazimika kusikilizwa kwa haraka kuhofia maamuzi ya kikao cha baraza la madiwani wa Manispaa ya Moshi kilichokaa jana Aprili 20, huku mwanasheria akitaka kutojadiliwa kwa ‘oder’ hiyo ya mahakama.
  Mwanasheria huyo alifafanua kuwa ‘oder’ hiyo inaelekeza kutofanyika kwa shughuli yoyote kwenye viwanja hivyo ambavyo kesi ipo mahakamani.
  Baada ya maelezo hayo kutoka kwa mkurugenzi, madiwani walitakiwa wajadili kwa pamoja juu ya kuondolewa kwa hoja namba 7 kwenye kikao hicho, hali ambayo ilikuwa vigumu kwa madiwani wa CHADEMA kukubali maamuzi hayo ya mkurugenzi ya kuondolewa kwa hoja hiyo huku wakitaka badala ya kujadili ajenda hiyo basi wajadili ‘order’ iliyotolewa na mahakama ili waone namna watakavyokabiliana na kesi hiyo.
  Pia madiwani walihoji juu ya kutopatiwa ‘oder’ hiyo siku iliyopita kwani walikuwa kwenye kikao cha awali cha baraza la madiwani ambacho kilidumu mpaka saa 12 jioni kama kweli mkurugenzi alipata barua hiyo saa 9 alasiri.
  Baada ya kutoa maelezo ya kuondolewa kwa hoja namba 7, mkurugenzi huyo alisema kuwa yeye ndiye mtendaji wa serikali na anachotaka ni vikao hivyo vifuate utaratibu na hatimaye kunyanyuka na kutoka nje ya kikao.
  Baada ya mkurugenzi kutoka nje na kufuatiwa na wataalamu wa halmashauri na madiwani wa CCM, madiwani wa CHADEMA waliendelea kukaa ndani ya ukumbi huo wakijadiliana ni nini kifanyike ili waweze kuendelea na kikao.
  Baada ya kujadiliana walikubaliana kuahirisha kikao kwa muda ili wamwandikie barua mkuu wa mkoa aweze kuwapatia katibu atakayeweza kuendelea na kikao. Hata hivyo, baada ya saa mbili kupita waliingia kwenye ukumbi majira ya saa saba mchana na kuendelea na kikao.
  Meya huyo alisema baada ya kupitia kanuni za kudumu za halmashauri hiyo walibaini kuwa wanaweza kuendelea na kikao kwa kuchagua katibu wa muda baada ya kubaini kuwa hakuna kifungu kinachowazuia kumchagua katibu au kutomchagua.
  Alisema kuwa madiwani ndio wenye maamuzi ya kuweka hoja na kuiondoa na katika kikao cha baraza walitaka kupitisha maazimio ya kufuta maazimio ya awali yaliyotolewa ya kuwamilikisha CCM majengo ya halmashauri.
  Hoja iliyotakiwa kuondolewa ni ile ya kujadili viwanja viwili, kiwanja chenye namba 056038/94 ilipo ofisi ya wilaya ya CCM na namba 15686 ilipo ofisi ya UVCCM mkoa.
  “Lengo la Mkurugenzi kutoka nje ya kikao ni kutaka CHADEMA waonekane kuwa wana vurugu na sisi hili tutaliepuka, na baada ya hapo endapo akifanikiwa kwa kisngizio hicho basi baraza hili la CHADEMA livunjwe ...lakini CHADEMA kwa hili hatupo tayari,” alisisitiza Jafari.
  Katika kikao hicho ambacho walimchagua Diwani wa Kata ya Longuo B, Raymond Mboya, kuwa katibu wa muda, walipitisha maazimio matatu, ikiwemo madiwani kuwa sehemu ya kesi iliyofunguliwa na CCM dhidi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
  Diwani wa Kata ya Bondeni, Abdulrahman Sharif, alisema lengo ni kumdhibiti mkurugenzi kwa kuhofia kufikishwa mahakamani na kukubali kuwa mali hizo ni za CCM pamoja na kumtafuta wakili kwa ajili ya kesi hiyo.
  Azimio jingine walilolipitisha ni la kumpeleka mkurugenzi kwenye kamati ya maadili kwa kile walichoeleza kuwa ni kudharau kikao kwa kutoka na watendaji na kumuacha mweyekiti huku kikao kikiwa bado kinaendelea, ambacho kitakuwa na wajibu wa kupeleka mapendekezo kwa mwajiri wake au waziri mwenye dhamana kwa ajili ya utekelezaji.
  Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, alisema mkurugenzi huyo alitoka nje kwa hoja kuwa ‘order’ ya mahakama haipaswi kujadiliwa lakini maelezo hayo hayana hoja, kwa sababu kilichotaka kufanywa si kujadili ‘order’ bali kujadili jinsi ya kukabiliana na kesi hiyo.
  Ndesamburo alisema kulikuwa na haja ya kujadili juu ya kuweka wakili kwenye kesi hiyo ambayo walisema hawataki kutumika kwa mwanasheria wa halmashauri hiyo, ambaye ndiye kwanza wamemuona jana pamoja na kumuweka kando mkurugenzi kwenye suala hilo baada ya kuonekana kuwa na masilahi binafsi.
  Polisi wengi wenye silaha walionekana maeneo ya kuzunguka halmashauri hiyo huku Barabara ya Florida inayotumiwa kuingia kwenye jengo la mkuu wa mkoa, manispaa na kituo cha uwekezaji nchini (TIC) zikiwa zimefungwa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 8:30 mchana.
  Hali hiyo ilisababisha usumbufu kwa wananchi kutokana na kuwa barabara hiyo inatumika kuelekea maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na viunga vyake.
  Kwa upande wake, Kinabo akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake baadaye, alisema kuwa aliamua kutoka kwenye kikao hicho baada ya kuona hapewi nafasi ya kuongea pamoja na madiwani wa CHADEMA kuamua kujadili ‘oder’ ambayo kisheria hairuhusiwi kujadiliwa.


  http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=29940
   
 2. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  :a s 465:
   
Loading...