Kumbe bajeti ni kiini macho tu?

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Leo asubuhi nilikuwa nikiangalia mahojiano ya mtangazaji wa tbc Gabriel Zakaria akiwahoji Aggrey Mwanri yule wasiri wa Tamisemi na dada Halima mdee kuhusu masuala ya Tamisemi.
Huyu Agrey alijaribu sana kuonyesha udhaifu wa halmashauri zetu na jinsi zinavyoboronga katika masuala yote ya kutuletea maendeleo, pamoja na ufujaji pesa mwingi unaoendelea katika halmashauri. Pia alieleza mikakati mingi waliyoiweka ili kuondoa wizi huo uliokithiri.
Alipopewa nafasi Mdee alimwambia wazi kabisa kwamba pamoja na madhaifu yaliyopo huk kwenye halmashauri, serikali inapeleka pesa kidogo sana za miradi ya maendeleo katika halmashauri tofauti na zile zilizopitishwa na Bunge, kiasi cha kufanya miradi mingi ya maendeleo ikwame kwani halmashauri hazipokei pesa kwa wakati na upewa pesa kidogo tofauti na zilizopangwa katika bajeti.
Nilifurahi na kushangaa kwa wakati mmoja, wakati Aggrey alipokubali bila kuuma meno kwamba ni kweli hali hiyo hutokea na ni kwa sababu sehemu kubwa ya bajeti ya maendeleo utegemea wanaoitwa wafadhili ( akasema yeye hawaiti wafadhili bali wahisani kwa sababu mfadhili ni mmoja tu "Mungu") na kwa bahati mbaya hawa wahisani uleta pesa kidogo au wanaleta wamechelewa au hawaleti kabisa na hivyo ukwamisha miradi ya kimaendeleo.
Mdee alidakiza hapo hapo kwamba kwa nini tukae tukitegemea wafadhili? Si ndio sababu CDM wanataka kupunguzwa kwa matumizi ili tupate namna ya kuanza kujitegemea kuliko kutegemea hao wafadhili?
Bwana Aggrey alisema ni kweli hata serikali yake inalifanyia kazi jambo hili.
Kitu nilibaki najiuliza maswali ni kwamba je hii bajeti tunasomewa kumbe karibu asilimia 60 inategemea tusaidiwe? na je kwa nini wabunge wengine wanaisifia kuwa ni bajeti safi itakayotuondoa katika matatizo wakati hatuna pesa za kuigharamia? Kweli bajeti ya kuombaomba ni bajeti itakayotukwamua kiuchumi?
Nashauri wale wote wanaoshangilia tarakimu za hesabu kuwa ni pesa zitakazotumika kutuletea maendeleo wafunge vinywa. Tumeingizwa mkenge, hii ni bajeti ya kisanii maana wahisani wasipotupa pesa hakuna litakalofanyika. Ni usanii moja kwa moja.
Hivi hakuna namna tunaweza kugharamia bajeti yetu wenyewe? Je, wahisani wakitunyima hela kwa sababu yoyote ile tutakimbilia wapi?

KAA LA MOTO
 
Wabunge wa CCM ndio wanaiangusha Serikali ya nchi hii mbaya kabisa. Kitendo cha makusudi cha kubeza ushauri kutoka upinzani ni cha kusikitisha sana..wabunge wamegeuka kuwa mawaziri kutetea bajeti..Nasema haiwezekani kabisa na si sahihi kutengeneza bajeti ya serikali ambayo matumizi ya KAWAIDA (kuendesha serikali) ni makubwa kulipo mapato ya ndani...matumizi trilioni 8 mapato trilioni 6!! Eti tunatarajia wahisani/mikopo tupate kama trilioni 6 kwa ajili ya MAENDELEO...Najiuliza Hapa tuna leadership kweli? Niwakumbushe uzuri wa bajeti si kuzingatia ilani ya chama au vipau mbele vya kitaifa bali ni utekelezaji wake.
 
Back
Top Bottom