Kumbe bado wanawake wanafuata asili katika kupenda…………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe bado wanawake wanafuata asili katika kupenda…………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, May 8, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  hadzabe-3.jpg 1284852638Yfm7Uk.jpg
  Katika utafiti wa hivi karibuni, watafiti wamegundua kwamba, wanawake wanawapenda wanaume wasio waoga na mashujaa kuliko wale waoga. Ushujaa wa wanaume ni kigezo kikubwa kwa wanawake kuwapenda marafiki wa kiume wa muda mrefu na muda mfupi. Hii inamaanisha kwamba katika urafiki wa kawaida na wa kimapenzi na wa kindoa, wema au ukarimu ulionekana kwamba ni kigezo cha kawaida.

  Tukirudi kwa mababau zetu wa kale walioishi mapangoni, wanawake waliwapenda wanaume shujaa ambao wangeweza kujitoa muhanga kuwalinda wao na watoto wao. Mwanaume ambaye alikuwa na uwezo wa kujitoa muhanga alionekana kuwa na uwezo wa kuwinda bila hofu na kuzama porini kutafuta chakula kwa jili ya familia.

  Bila shaka ushujaa huo kwa wakati huo ulikuwa na maana ya mwanaume kuwa na uwezo wa kuifanya familia ijihisi salama. Kwa maana hiyo, fedha ambayo ndiyo inayotamalaki hivi sasa, ndicho chombo kinachowafanya wengi kuamini kwamba kuwa na fedha inamaanisha wako salama. Kwa hiyo mwanaume mwenye nazo ananekana kama ndiye anayeweza kuilinda familia. Kwa hiyo ukikuta wanawake wanavutiwa na wanaume wenye fedha, usishangae, kwani bado wanafuata ule wito wa asili wa haja ya mwanamke kuhakikishiwa usalama wake.
   
 2. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa hizo pesa zikikata inakuwaje?
  Bado wazee hatuwawezi! kwani ushujaa wao katika kutafuta ni kumudu kuwalinda wenzi wao na familia kwa ujumla, Mwanaume mwenye uwezo wa kulima kwa ajili ya kupata chakula cha kulisha familia yake. kingine kuuza kwa ajili ya kusomesha watoto.
  Siku hizi vibarua venyewe vya kihindi anakuajili asubuhi, jioni anakumwaga, maisha ya kubangaiza mjini..........lol!
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Michael Scofield ..................Nakubaliana kuhusu wanaume wa zamani na utafutaji....................Kule vijijini wanume wenye wanawake wengi ni wale wanaume hodari kwa kilimo na utafutaji..........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umeonaeee!
  Siku hizi kila kitu pesa, mapenzi=pesa, pesa ikikata hakuna mapenzi.
   
 5. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Siku hizi tofauti na zamani wanawake wa siku hizi kama huna hela hakuna ndoa ila zamani hata kama huna hela unaoa vizuri tuu na mnalima pamoja kutafuta chakula cha familia.
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  I prefer the later. . .
  Kushirikiana ndio mpango mzima.
   
 7. Justin Dimee

  Justin Dimee JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 1,148
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Wanawake wa saivi sio kabisa kama ukichek global pulisher habr ya jana kuna sijui ndo kamiss cjui cha wapi yan eti kana miaka 19 but hakaoni hata haya kanaenda kutoka na kigogo eti kisa ana pesa yan wanawake sio siri wanapenda vya mteremko sana yan duh eti kime pangishiwa nyumba ya milion 7 duh hawa wanake wa kileo duh mtu uwe makini kuwa chek ahse huyu mdada mi alinishangaza umri mdogo alafu ana nguvu let say za kutafuta hela but kwakuwa anapenda vya mteremko simple way aka ona ajibane kwa uyo kigogo hataka kigogo ndo ka mfuata but nayeye angalie mbele aone wata kuwa ni wangi huyo kigogo kawa fanyia ivyo mmh wanawake acheni mikumboo bana.
   
 8. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Maisha yamebadilika ndo maana watu nao wanabadilika ili kuendana na mazingira..kwa maisha ya sasa kuendesha maisha bila hela ni sawa na kusukuma gari lisilokua na magurudumu..
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Purple ........Ndio maana nilisema kinachotafutwa na wanawake ni kuhakikishiwa usalama.............Siku hizi hatuwindi wanyama kama sehemu ya chakula, bali fedha imechukua nafasi katika kujihakikishia usalama wetu........ Kila kitu siku hizi ni pesa na ndio maana wanawake kwa dhana ile ile ya kujihakikishia usalama wanavutiwa na wanume wenye nazo........ Sio kwa sababu ya tamaa......La hasha, ni kutaka kuwa na uhakika na maisha yake na familia yake baadae, kama akikosa sifa ya fedha ataangalia mwanaume mwenye ujasiri wa kuthubutu na mchakarikaji, hapo anajua kwamba kwa kushirikiana mbeleni maisha yatakuwa mazuri na salama................
  Ikitokea kwa mfano kaolewa na mwanaume mzigo au siku hizi tunawaita "Dead alive" Jukumu la kutafuta hulishika mwenyewe kwa sababu hamna jinsi na mara nyingi hufanikiwa kuzikamata kwa sababu anafanya hivyo kwa nia na dhamira ya kujihakikishia usalama.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  very true...
   
 11. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Pesa ndo kila kitu....hata njiwa huwezi kumla bila ya pesa.
   
 12. b

  bia JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh naacha pombe
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  za asubuhi mkuu
   
 14. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  New times requires new approaches but traits remains the same.
   
 15. J

  JOJEETA Senior Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli but cku hizi cio wanawake2 hata wanaume wapo,,,utakuta janaume linasema"natafuta jimama lenye pesa zake linilee".so mi naona issue hii cio wanawake tuu bali wanaume pia
   
 16. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Ni kweli, unajua kwa mvivu siku zote njaa ni sehemu ya maisha. Lakini, jasiri hata kama kaajiriwa na muhindi kama anavyosema Scofield bado atakuwa na shamba; na si ajabu jioni atakuwa anafua hata vyuma.

  So hata kibarua kikiota nyasi; bado ugali wa kila siku utapatikana, wagonjwa watapata matibabu n.k
   
 17. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pesa si kila kitu bali security. Kuna watu wana fedha na wake zao wanatumia pesa zao kuwahonga wawatakao. Hivyo kama tutaongelea mapenzi ya kweli, nadhani wanawake wana sababu mbali mbali za kupenda. Wapo watu maskini wameoa wanawake wema na wapo watu matajiri wameoa matatizo. Kimsingi, suala la pesa si la wanawake wote bali wale wanaotoka kwenye mila zinazoabudia pesa ambao hapa kwa mfano siwezi kuwataja kuogopa kuchafua hewa. Wapo ndugu zetu ambao mke hata kama mume ana pesa kiasi gani asipompiga ni dalili tosha kuwa mwanaume hafai. Ukienda kule Ethiopia kuna makabila ambapo wanawake hupenda wanaume warefu. Hata ndugu zetu hapa Tanzania kule AR wana mila hii. Kama wewe ni pimbi hata uwe milionea watakushit tu.
   
Loading...