BINAGI BLOG-BMG
Member
- Mar 12, 2016
- 73
- 33
Kabago anatambulika kama mmoja wa watu waliowezesha hiphop nchini kusonga mbele tangu akiwa mkoani Arusha na hata alipohamia Mwanza, akiwa kama msanii na mtangazaji wa redio (kwa sasa Passion Fm Mwanza).
Atakumbukwa namna alivyosaidia kwenye harakati za kimaendeleo Jijini Mwanza kupitia kazi zake za muziki na hata namna wimbo wa tatizo la umeme ulivyoleta nafuu kwa wakazi wa Jiji la Mwanza.
Kama hiyo haitoshi, mchango wake redioni ni mkubwa kwa wasanii mbalimbali hususani wanaochipukia ambapo wengi wao ambao sasa ni wanavuma akiwemo Baraka Da Prince na Young Killer, wamepitia mikononi mwake.
Kumbe bado yupo, nina hamu ya kusikiliza huo wimbo wake mpya ili kujua ikiwa bado makali yake yapo.