Kumbe anafanya yote haya kunirusha roho yangu juu

Mohamedex121

JF-Expert Member
Jan 27, 2022
1,688
3,142
Habarini wakuu! Ni mimi tena kijana wenu jamiiforums! Msione kimya niko katika harakati za utafutaji ndio zinavyotuweka katika ubize si mnajua maisha yalivyo now ni kujihagaishwa ili mkono uwende kinywani.

Nisiwachoshe sana wakuu ngoja niende kwenye mada mara moja.

Kuna demu nilikuwa nae kwenye mahusiano kipindi niko chuo ila now mahusiano yamepungua baada ya kila mtu kurudi mtaani (masomo kuisha).

Nilikuwa nimeplan nimuoe na hili nilishamuweka wazi nadhani analijua hili pia, ila linapokuja suala la kuoa asa kipindi hiki ambacho sina chochote ninachomiliki zaidi ya gheto lenye godoro chini na biashara yangu ya umachinga apa mbezi mwisho ni mtihani kwakweli nikamuomba anipe muda wa kutafuta hela ili mambo yakae sawa maana now hali ngumu nimetoka kupoteza biashara yangu ya Studio hadi kuwa machinga Aisee nimedrop sana kimaisha.

Shida inakuja apa wakuu, baada ya kuwa Bize sana na biashara suala kumtext na kumpigia simu nilikuwa nafanya mara moja moja kwa wiki ila naona siku hizi amebadilika sana.

Nilimuomba awe anajishughulisha na biashara ili baadae tuje tusaidiane katika maisha ya ndoa ila mwenzangu yupo Bize sana na mambo ya dunia, suala la mitoko starehe kwake ni suala la kawaida sana. Kila siku namuona whatsapp akipiga picha akiwa sehemu za Bata wanakula sijui mnaita mabaga sijui mapiza na mazagazaga mengi, mara awa wish wanaume wengine happy birthday zao na anaweka picha zao huko whatsapp najaribu kuziview ila nimegundua anafanya yote ili kunirusha roho yangu juu au ana maana gani kufanya hivi au hajui kuwa kuna maisha ya baadae hizo pesa za kula Bata kwanini asiwekeze kipindi hiki ili baadae tuje tusaidiane. Huwa najiuliza sana ila sipati majibu.

Anyway wakuu #Natanguliza_shukhurani_wakuu. Kwa kunisikiliza masaibu yangu I hope mtanipa ushauri juu ya hili
 
I
75aa8356-e3b7-451f-9ea1-1c2fde8a4cae.jpg
 
Kila siku namuona whatsapp akipiga picha akiwa sehemu za Bata wanakula sijui mnaita mabaga sijui mapiza na mazagazaga mengi, mara awa wish wanaume...
Kiufupi
  • Sio mwanamke sahihi kwako
  • Hakupendi
  • Hajitambui
  • Tafuta atakayekupenda katika hali ngumu uliyonayo sasa, huyo ndiye mtu sahihi kwako.
Songa mbele sahau kama uliwahi kuwa naye.
 
Ni kweli kabisa ndio mimi nimejiweka kando na mahusiano hasa kipindi hiki, lakini mwenzangu yupo Bize na mambo ya kidunia hajui kuna kesho kwanini hizo pesa anazozichezea asiwekeze??
Hahahaha sasa wewe jomba mbona unaumia sana kama vile hela unampa wewe? Kimsingi kama ndo umemaliza chuo basi demu anayefaa kuwa mkeo labda ndo yuko form IV sasa hivi.

Huyo mliyelingana umri waachie wakubwa.. sio size yako. Wewe kwa sasa pigana kwanza uweze kujimudu basic needs. Usiwe na wasiwasi mkeo yuko form IV wazazi wanakutunzia.

Akimaliza chuo na yeye atamwacha boyfriend wake wa chuo na kuja kwako.
 
Hahahaha sasa wewe jomba mbona unaumia sana kama vile hela unampa wewe? Kimsingi kama ndo umemaliza chuo basi demu anayefaa kuwa mkeo labda ndo yuko form IV sasa hivi. Huyo mliyelingana umri waachie wakubwa.. sio size yako. Wewe kwa sasa pigana kwanza uweze kujimudu basic needs. Usiwe na wasiwasi mkeo yuko form IV wazazi wanakutunzia. Akimaliza chuo na yeye atamwacha boyfriend wake wa chuo na kuja kwako.
Wanawake siku hizi hawatabiriki unaweza kusema nimsubiri huyo wa form 4 mpaka amalize chuo anaweza kuwa kama huyu asiyekuwa na akili za maisha
 
Back
Top Bottom