Kulogea/kulogewa yai viza

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,791
Reaction score
830,941
Yai viza ni kitu kisichofaa kimekufa kinanuka hakina uhai...yai viza hutumiwa sana na wachawi wenye roho mbaya kuharibu maisha ya mtu..ni mojawapo wapo ya uchawi mbaya kabisa kulogewa nao.

Mara nyingi hunuizua maneno kama haya ....kama hili yai lisivyo na uhai ....kama hili yai lisivyo na faida...kama hili yai linavyonuka...

Kisha baada ya manuizi hayo hupasuliwa njia panda ili litawanyike pande nane za uso wa dunia ili kila utakapoenda utakalofanya lisifanikiwe na uchukiwe na kukimbiwa na kila mtu....hata ulikuwa una mafanikio kiasi gani ghafla hujikuta unaanguka na nuksi balaa na mikosi kukuandama

NB: Sifundishi uchawi bali najaribu kuelezea ubaya wa kitu fulani kama hiki ili siku ikitokea kuna mtu kakuudhi usimfanyie jambo baya kama hili bali mwachie Mungu kwakuwa yeye ndio mwamuzi wa haki.

Na wewe kama kuna mtu kajaribu kukufanyia hivi Usijaribu kwenda kwa waganga wa kienyeji kwakuwa huko unaenda kutafuta balaa zaidi la viapo na maagano ambavyo unaweza kuja kushindwa kuvitengua.

Mwachie Mungu kwakuwa hata juju liweje huwa lina kikomo cha kuishi na kufanya kazi expire date.
 
Unafundisha shule gan mwalimu?
 
Mkuu hii ina mahusiano yoyote kati ya curse, spell cast, black magic au sorcerer!?

Je muathirika wa uchawi anaweza kujifanyia self delivarance via psychic powers!?
 
Mkuu hii ina mahusiano yoyote kati ya curse, spell cast, black magic au sorcerer!?

Je muathirika wa uchawi anaweza kujifanyia self delivarance via psychic powers!?
This man he don't have logic to answer your question.

Swissme
 
Mkuu hii ina mahusiano yoyote kati ya curse, spell cast, black magic au sorcerer!?

Je muathirika wa uchawi anaweza kujifanyia self delivarance via psychic powers!?

At least we can call it black magic. Muathirika hawezi kujifanyia self deliverance via psychic powers kwakuwa huu ni uchawi kamili ambao uko kinyume kabisa na psychic powers au supper natural powers .

Haiwezi pia cuser (laana)kwakuwa laana hutamkwa waziwazi tena mbele ya mtu husika, kimsingi laana si uchawi. Haiwezi pia spell cast, hili jibu lake lipo kwenye ile post ya kiapo cha damu. Spell cast haina mambo mengi na inaenda moja kwa moja kwa mlengwa, spell cast na laana huwa havihusishi third part.

Hii yaweza kuwa black magic au sorcerer kwakuwa

1. Ni lazima awepo mganga/mchawi wa kukutengenezea hilo scud
2.haifanyiki waziwazi bali kwa kificho na kwenye maeneo maalum kama njia panda nk
3.kwa kiasi kikubwa hii haifanyiki mchana bali usiku mwingi au alfajiri
 
Hiviii haiwezekani uchawi ukamfanya mtu kuwa tajiri tukaondokana na umasikini badala ya kuwafanyia watu mabaya.....
 
Hiviii haiwezekani uchawi ukamfanya mtu kuwa tajiri tukaondokana na umasikini badala ya kuwafanyia watu mabaya.....

Uchawi ni pepo na roho ya kuharibu hivyo hauwezi kutengeneza
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…