Kulipishwa na kukamatwa kwa ndege za Watanzania

Dreamnaire

Member
May 7, 2022
99
74
Kila ninapotafakari chanzo cha kushindwa kesi na kukamatwa mali za Watanzania, maswali ni mengi majibu ni machache. Je, ni kwa sababu wakati tunaingia mikataba na hizo kampuni tunaangalia upande wa faida tu bila kuona risk ya vipengele kwenye mkataba? Au ni kwa sababu vipengele vya kujitoa kwenye mkataba vinampendelea kampuni kuliko taifa?

Kwa mfano, tunaweza jilinganisha na Marekani kwenye kukatika umeme, kwanini tusijilinganishe na wao kwenye kuingia mikatabab ya nchi? Kwanini tusijilinganishe nao kwenye kushtakiwa kwa wahusika wenye kuingia hiyo mikataba tukianzia kwa Rais wa nchi?

Unavyozidi kulitafakari hili jambo maswali yanaongezeka, kwa nini? Inakuwaje kwamba Rais wa Marekani akifanya jambo kinyume na katiba, kinyume na sheria, Rais akiingia mkataba unaopelekea nchi kupata hasara anawajibika kwa kutoa maelezo na kujitetea? Maswali ni mengi.

Au kwenye katiba yetu hakuna kipengele au mwanya wa kuanzia ili kupata suluhu yenye kutupa mwanga au japo matumaini?

Vipi nyie wadau na wananchi wenzangu, kuna majibu mliopata ya kupata muafaka japo kwa kuanzia?
 
Hakuna uwajibikaji Tanzania viongozi ni waganga mkaa,wapo kimaslahi na si kiutumishi.
Ntafikiria kuwepo kiwango fulani cha kipato ili mtu awe kiongozi mfano GSM hawezi ihibia yanga au Mo simba ila tu baadhi ya mambo yake yataenda
 
Back
Top Bottom