Kulingana na taarifa za Ewura

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Wakuu Kulingana na taarifa za Ewura, Mwaka 2020 tulitulimia mafuta ya wasitani wa lita bilioni 3,500,000,000
.
Ripoti ya matumizi ya mafuta mwaka 2021 bado haijawekwa katika mtandao.
.
Lakini ukijaribu kulinganisha mwaka 2018, 2019 na 2020 tofauti ni ndogo kwenye hizo lita bilioni 3.5.
.
Twende kwenye hesabu sasa.
.
Serikali inakusanya kodi kiasi cha Tsh 1243/= kwa kila lita moja.
.
Chukua;-
Lita 3,500,000,000 zidisha kwa Tsh 1243/= unapata Tsh 4,350,500,000,000/= (Trilioni 4 na Bilioni 350 na milioni 500)
.
Hayo ni mapato ya Serikali kupitia tozo mbalimbali kwa mwaka.

Maswali yangu wakuu;
.
1. Je sekta hii ya mafuta ina changia kwa asilimia ngapi katika mapato ya Serikali kama kodi kwa mwezi?
.
2. Je sekta ya usafirishaji, viwanda vinavyotumia mashine za mafuta na si umeme vinachangia kiasi gani mapato ya mwezi ya Serikali kama Kodi? (Naamanisha kodi ya biashara)
.
3. Je tukipoteza hizi trillion 4.3 kwa mwaka za mafuta shughuli za Serikali zitaathirika kiasi ganii?
.
4. Watalaamu wa Kodi kutoka TRA watusaidie.
.
Gharama za Maisha zimepanda kwa sababu ya kupanda kwa gharama za usafirishaji na kupanda kwa gharama za uzalishaji.
.
Matokeo yake mzunguko wa pesa utapungua kwa maana watu na makampuni ya uzalishaji kujibana kuogopa kupata hasara, kwa sababu inflation inapunguza uzalishaji na inapunguza ajira pia.
.
Kodi ya biasharaa na Kodi za watumishi (PAYE) inayo lipwa Serikali kutoka kwa makampuni haya ya usafirishaji na viwanda vya uzalishaji ni kiasi gani ukilinganisha na hii trilioni 4.3 inayokusanywa kwenye mafuta?
.
Je tumefanya tathimini ya kutosha kujua endapo uzalishaji utapungua na na Ajira kupungua Serikali itakosa kodi kiasi gani?
.
I humbly Submit 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom