Leo,16th October 2015, tumefungua Kesi chini ya hati ya haraka sana (certificate of extreme urgency) shauri nambari 37 la mwaka 2015 katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Main Registry) tukiomba Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi ya kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi Tanzania na itamke iwapo wapiga kura na watu wengine wenye shauku wanaruhusiwa au la kukaa KWA UTULIVU umbali unaozidi meter 200 kutoka kituo cha kupigia kura/kufanya majumuisho ya kura.
Tumeiomba pia Mahakama Kuu itamke iwapo ni halali kwa Rais wa nchi kutoa matamko aliyoyatoa kwa namna ya katazo kwa wapiga kura/raia wenye shauku kukaa KWA UTULIVU umbali unaozidi meters 200 kutoka kituo cha kupigia kura/kufanya majumuisho.
Pia tumeiomba Mahakama Kuu itamke iwapo Rais ana mamlaka hayo kisheria kwa kuzingatia Sheria ya Uchaguzi Tanzania.
Tunasubiri taratibu za kiMahakama kuhusu shauri tajwa.