Elections 2015 Kulinda kura: Wakili Peter Kibatala afungua kesi Mahakama Kuu

amilyroley

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
621
1,199
Tayari wakili jembe na nguli Peter Kibatala akiambatana na wanasheria nguli wa Ukawa Prof Safari, Mallya na Tundu Lissu asubuhi ya leo amefungua kesi mahakama kuu kuishitaki NEC kwa ukiukwaji wa sheria juu ya wananchi kukaa mita mia mbili na kulinda kura.

Kesi imefunguliwa under certificate of urgency nadhani kama sijakosea kwa kiswahili ni 'hati ya dharura' ili isikilizwe na tafsiri itoke kabla ya uchaguzi.Tayari jalada lishapelekwa kwa pilato na wanasheria nguli wa Ukawa wamejipanga kwa hoja za nguvu na ushahidi wa kutosha.

Pia jopo la wanasheria nguli wa UKAWA wameiomba mahakama kuu ya Tanzania kutoa tafsiri ya kisheria juu ya matamshi ya rais wa nchi kuwa alitumia mamlaka gani kuvaa kazi za tume.

Peter Kibatala said:
Leo,16th October 2015, tumefungua Kesi chini ya hati ya haraka sana (certificate of extreme urgency) shauri nambari 37 la mwaka 2015 katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Main Registry) tukiomba Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi ya kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi Tanzania na itamke iwapo wapiga kura na watu wengine wenye shauku wanaruhusiwa au la kukaa KWA UTULIVU umbali unaozidi meter 200 kutoka kituo cha kupigia kura/kufanya majumuisho ya kura.

Tumeiomba pia Mahakama Kuu itamke iwapo ni halali kwa Rais wa nchi kutoa matamko aliyoyatoa kwa namna ya katazo kwa wapiga kura/raia wenye shauku kukaa KWA UTULIVU umbali unaozidi meters 200 kutoka kituo cha kupigia kura/kufanya majumuisho.

Pia tumeiomba Mahakama Kuu itamke iwapo Rais ana mamlaka hayo kisheria kwa kuzingatia Sheria ya Uchaguzi Tanzania.

Tunasubiri taratibu za kiMahakama kuhusu shauri tajwa
.
 
Kiambatanisho cha uzi
 

Attachments

  • 1444987005542.jpg
    1444987005542.jpg
    29.7 KB · Views: 12,783
kila la kheri my learned brother,I hope High Court watatoa tafsiri liberally kuhakikisha haki inapatikana
 
Tayari wakili jembe na nguli Peter Kibatala asubuhi ya leo amefungua kesi mahakama kuu kuishitaki NEC kwa ukiukwaji wa sheria juu ya wananchi kukaa mita mia mbili na kulinda kura. Tayari jalada lishapelekwa kwa pilato na wanasheria nguli wa Ukawa wamejipanga kwa hoja za nguvu na ushahidi wa kutosha.


dah nahisi mtu anaweza kurogwa hapa manake kila mwanya wa goli la mkono ukitokeza mnaziba....dah msidhani wanafurahi?
 
Nice move,ila pia wafanye utaratibu wa kumlima Kikwete kwa wawakilishi wa nchi za Ulaya,International Observers na ICC kwa kitendo chake cha kuingilia NEC huku akipotosha idadi ya wapiga kura na kutoa vitisho vya kutumia mabavu/kuvunja amani!!!
 
kila la kheri my learned brother,I hope High Court watatoa tafsiri liberally kuhakikisha haki inapatikana

Mkuu wala liberal approach haihitajiki kwani kifungu kipo wazi kabisa kuwa kukaa mita mia mbili toka sehemu ya kupigia kura sio kosa. Ila haisemi mkiwa hapo muwe kwa ajili ya kulinda kura. Kwa hiyo watu wakae mita hizo mia mbili ila polisi wakija wasiseme tupo hapa tunalinda kura hata kama mioyoni mwao lengo ni kulinda kura.
 

Similar Discussions

36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom