KULIMBIKIZA VYEO: Rais Magufuli ateua mtu mmoja vyeo viwili na mikoa miwili tofauti

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,636
29,511
Rais alisema hawezi mrundikia mtu mmoja vyeo lakini kwa huyu naona kabahatika au wenye weledi CCM wameisha?

Anaitwa Samwel Warioba Gunzar. Kwa ukurugenz kapewa Lindi DC na kwa uDAS kile cheo cha akina Mtela Mwampamba kapewa Wilaya huko Manyara.

Naamini bado wengine watapata uteuzi humu ndani maana kuna makosa ambayo yatafanya nafasi ziwe wazi.

1. Dk Leonard Masule huyu aliteuliwa kuwa DC Ilemela ila kwenye uteuzi huu wa Wakurugenzi inaonesha amepangiwa Dodoma

2. Justin Joseph Monko huyu aliteuliwa kuwa DAS MUSOMA ila kwenye uteuzi huu wa Wakurugenzi inaonesha amepangiwa Liwale

3. Haji Yusuph Godigodi huyu aliteuliwa kuwa DAS KIGOMA ila kwenye uteuzi huu wa Wakurugenzi inaonesha amepangiwa Kyerwa

4. Joel Mwakibibi huyu aliteuliwa kuwa DAS BIHARAMULO ila kwenye uteuzi huu wa Wakurugenzi inaonesha amepangiwa Kigoma

5. Msongwe huyu aliteuliwa kuwa DAS MISENYI ila kwenye uteuzi huu wa Wakurugenzi inaonesha amepangiwa Kasulu

Kweli Zilongwa mbali, Zitendwa mbali!

1467894696936.jpg

1467894719314.jpg
 
Aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma pia ameapishwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Ilemela hii imekaaje?
 
Mkurugenzi wa manispaa Dodoma ameteuliwa kimakosa pia. Jina lake limeondolewa tayari.
 
Unajua kwa spidi tunayoenda nayo sometimes tunajikuta tumepitiliza vituo sometimes tunaamua kukatisha ruti!!
Kama hajaapishwa bado basi namshauri asiende kwenye hafla ya kuapishwa!yasije yakamkuta yaliyomkuta yule mwenzie aliyetolewa ukumbini kama kibaka.
 
Alisema hataki kuwalimbikizia watu madaraka nini sasa hiki?
Au teuzi zinafanywa na mtu mwingine, hashirikishi wasaidizi wake hadi ajikute anampa mtu mmoja nafasi mbili?
 
kwani haraka ya nini? si alisema ajira zimesitishwa? au tunakimbilia nchi ya viwanda
 
Si alisema hakuna atakaepata cheo mara mbili, hyo ya juu ni uDAS na hyo ya chini ndo ukurugenzi daaah nmechoka aseee na wasaidizi wake
View attachment 363867View attachment 363869
Sasa huyu samweli wanonta gunza atawezaje kufanya kazi Lindi na Mbulu kwa wakati mmoja? Dah! au ndio ameandaliwa viatu vya mwendo kasi Lindi to mbulu Mbulu to Lindi daily?
 
Back
Top Bottom