Umri wa Kustaafu kwa Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya; Sheria za nchi zinafuatwa?

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,178
2,000
Fahamu kwamba kwa mujibu wa sheria ya uongozi wa mikoa (The Regional Administration Act) Sura ya 97, Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ni maofisa (watumishi) wa Umma (Kifungu cha 3 na kifungu cha 4 (2)).
Screen Shot 2021-05-16 at 8.12.06 AM.png

Stahiki na mafao yao ma-RC na ma-DC zimeelezwa katika Sehemu ya 6 ya Sheria ya the Political Service Retirement Benefits Act CAP 225 R.E 2015 hususani kifungu cha 24 (1). Sheria hii inaeleza kuwa Mkuu wa mkoa atapata Mafao stahiki baada ya kustaafu kwa lazima kwa umri unaojulikana (miaka 60) au katika umri wowote chini ya miaka 60 kwa kuondolewa katika ofisi hiyo (Utenguzi) kama kabla ya uteuzi hakuwa mtumishi wa umma (kama kina Mulongo na Makonda).

Kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya Kustaafu kwa watumishi wa Umma (The Public Service Retirement Benefits Act CAP 371 R.E 2015), imeelezwa kuwa kustaafu kwa hiyari kwa mtumishi wa umma ni kuanzia miaka 55 na kustaafu kwa lazima ni pale mtumishi afikapo miaka 60 isipokuwa kwa majaji wa Mahakama Kuu (kina Biswalo) na majaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambao wao kwa mujibu wa ibara ya 110 na 120 ya katiba wanatakiwa kukoma utumishi wanapofika miaka 60 au zaidi (majaji wa mahakama kuu) na miaka 65 au zaidi (majaji wa mahakama ya Rufaa) ikiwa Rais ataona kuwa inafaa kwao kuendelea na utumishi wa umma. Hawa umri wao wa kustaafu kwa hiyari na kwa lazima utafuata vile Katiba ya nchi inavyoeleza.
Screen Shot 2021-05-16 at 9.07.39 AM.png

Uzoefu (Experience and Practice) unaonesha Sheria hizi zimekuwa hazifuatwi na watawala na kama zinafuatwa basi inakuwa sio kwa uwazi yaani bila umma kuhabarishwa pale kunapokuwa na nyongeza ya kuendelea kubaki ofisini kwa Mkuu wa Mkoa au wa Wilaya mwenye umri wa kustaafu kwa lazima (kama wanakuwa wamewaongezea muda) hivyo kupelekea ugumu wa kujua kama Serikali inaheshimu sheria au la na kuiwajibisha. Jambo hili pia limekuwa linaleta mkanganyiko pale taarifa za Uteuzi zinapotolewa kwa umma na kueleza kuwa baadhi ya teuzi zimefanywa kwa ajili ya kuziba nafasi za Wakuu wa Mikoa waliostaafu bila ya kutaja kama kustaafu kwao ni kwa hiyari au kwa lazima baada ya kufika umri wa kustaafu. Mkanganyiko umekuwa unapoteza hata uelewa wa wananchi ambapo ukiuliza umri wa kustaafu kwa ma-RC na ma-DC wengi hawajui jambo ambalo sio zuri.

Mfano taarifa ya teuzi za Wakuu wa Mikoa zilizofanywa tarehe 15 Mei 2021 na Mheshimiwa Rais Samia inaonesha Anna Mghwira amestaafu (huyu ana umri wa miaka 62 - amezaliwa 23 Januari 1959 ) wakati huohuo taarifa inaeleza kuwa Makongoro Nyerere ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara (Huyu ana umri wa miaka 62 kwani amezaliwa 30 Januari 1959 ambapo tayari umepita umri wa kustaafu kwa lazima (miaka 60). Pia taarifa inaeleza kustaafu kwa wakuu wa mikoa wengine kama Joachim Wangabo na Idd Hassan Kimanta ila haielezi kama kustaafu kwao ni kwa hiyari au kwa lazima.

Huenda mazoea yamejenga tabia kiasi sasa hatufuati Sheria bali mazoea; Mzee Yusufu Makamba aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM kutoka Ukuu wa Mkoa akiwa na umri wa Miaka 69, wapo na wengine waliohudumu wakiwa wazee sana kama kama kina Balele, Mashishanga nk

Ni wakati sasa Serikali ikaanza kuzingatia sheria zilizopo ama sivyo kunakuwa hakuna maana ya kuwa na bunge kwa ajili ya kutunga Sheria zisizoheshimiwa. Kama tunaona ni vyema kuwa na ma-RC na ma-DC wasio na ukomo wa umri wa Kustaafu basi tuweke hivyo katika Sheria ili jambo liwe linafanyika kisheria. Utawala wa Sheria (The Rule of Law) ni pamoja na Serikali kuonesha mfano wa kuheshimu Sheria. Wanaomshauri mheshimiwa Rais wamshauri vyema na wasimpotoshe kuhusu hizi Sheria maana mwishowe tutarudi kulekule kwenye uvunjaji wa Katiba.​

Screen Shot 2021-05-16 at 12.46.11 PM.png
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,191
2,000
Vijana hawana ajira wazee wanaendelea kupeana shavu endlessly kinyume cha sheria halafu wanakuja kukebehi "jiajirini". Funny!
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,140
2,000
Akili yangu inaniambia Mama Mghwira ametolewa tu kafara ili kubalance mambo baada ya kumsimamisha yule jambazi Ole Sabaya.
 

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,178
2,000
Akili yangu inaniambia Mama Mghwira ametolewa tu kafara ili kubalance mambo baada ya kumsimamisha yule jambazi Ole Sabaya.
Kama ni kustaafu ilipaswa iwe miaka miwili iliyopita. Kutuambia kuwa amestaafu ilhali ana umri sawa na wa Makongoro Nyerer aliyeteuliwa kwa nafasi hiyohiyo kunaonesha jambo fulani halipo sawa.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,140
2,000
Kusema amestaafu huku ana umri sawa na wa makongoro aliyeteuliwa kunaonesha jambo fulani halio sawa. Kama ni kustaafu ilipaswa iwe miaka miwili iliyopita.
Rais amejigeuza tu kuwa Pilato! Amemtoa kafara Mama Mghwira ili kupunguza msuguano kwa Mataga ambao hawakufurahishwa na kitendo cha Taga mwenzao Ole Sabaya kusimamishwa UDC, na huku ikijulikana wazi hakuwa akimheshimu huyo RC wake.
 

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,178
2,000
Vijana hawana ajira wazee wanaendelea kupeana shavu endlessly kinyume cha sheria halafu wanakuja kukebehi "jiajirini". Funny!
Kigwangala anasema vijana tufikiri nje ya box na kujiajiri hapohapo anahonga baiskeli wajumbe ili aendelee kula kodi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom