Kulima mazo kama mahindi maeneo ya mjini

Cassava

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
282
36
Ndugu wana jamii forum, kuna sheria inayokataza kulima mazao sehemu za mijini mazao marefu kama mahindi. Sheria hiyo hutekelezwa na baadhi ya wakurugenzi wa miji michache hapa inchini, Iringa manispaa ikiwemo.

hata hivyo kwa uchunguzi niliokwishafanya, miji kama ya mwanza, dodoma, Morogoro Kigoma na Tabora huwa mahindi yanalimwa mjini.

Ninachojuwa ni kwamba, kwa wale wenye vi jieneo mjini wakilima mahindi huwa vinawasidia sana. lakini kwa mji wa IRINGa kulima mahindi ni issue, unamuliwa uyakate mwenyewe mara tu yafikapo kimo cha mbuzi na unashitakiwa hadi kulipishwa faini.

sasa wadau, maisha ya sasa, yanazidi kuwa magumu siku hadi siku,na mahindi yakilimwa hata eneo dogo yanaleta tija kwa huyo aliyelima.

Naweka hii mada kuuliza, wenye maeneo ya kulima hayo mahindi wafanyeje ili mkurugenzi huyo aweze kuwaelewa kwa kuwa hata miji mingine kama nilivyoitaja hapo juu wanalima na huvuna bila matatizo.

Hata hivyo ninaelewa kabisa mkurugenzi huyo anatekeleza kanuni na taratibu za kustawisha miji iwe katika hali ya usafi lakini tumbo nalo ndo hivo linahitaji.

Nawasilisha.
 
You do not need to compare how towns treat her citizens, bylaws do differ. In tz no single city, municipal councils or township allows farming.
 
Back
Top Bottom