Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,853
- 930
JUHUDI ZA DKT. ALFRED KIMEA ZIMELETA MAHINDI BORA NA YA BEI RAFIKI KWA WAKAZI WA KOROGWE MJINI
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mhe. Dkt. Alfred Kimea, PhD wakati wa ziara yake jimboni alielezwa na wananchi juu ya changamoto ya ukosefu wa vyakula muhimu ikiwemo uhaba wa Mahindi na bei kuwa juu.
Mbunge huyo baada ya kupokea changamoto hiyo alifanya jitihada za kufikisha kilio hicho kwenye mamlaka husika na hatimaye tarehe 04 Aprili 2023 wananchi wa jimbo la Korogwe Mjini waliletewa Mahindi ya bei nafuu kutoka Serikalini.
"Mahindi hayo yatakuwa yakiuzwa kwa bei ya Shilingi 970 kwa Kilo Moja badala ya bei ya zaidi ya Shilingi 1500 ambayo iko sokoni sasa" - Amesema Mhe. Dkt. Alfred Kimea
Kwa upande wake mwingine, Mbunge wa Korogwe Mjini Mhe. Dkt. Alfred Kimea ametoa shukurani zake za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jambo hili kubwa kwa watu wa Korogwe Mjini.
Aidha, Mhe. Dkt. Alfred Kimea amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mh. Jokate Mwegelo, DAS (Katibu Tawala wa Wilaya) Mhe. Rahel Muhando pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji kwa jitihada zao za kutatua changamoto iliyokuwepo.
Aidha, Mhe. Dkt. Alfred Kimea amesema Ofisi yake imejipanga kujitolea kusaidia usafiri wa Mahindi yaliyonunuliwa na wananchi walioko katika maeneo ya mbali na vituo yanapotolewa Mahindi hayo hasa Kata za Kwamsisi, Mgombezi na Kwamndolwa.
Pia, Mhe. Dkt. Alfred Kimea amewaomba viongozi na watendaji wa Kata na Vijiji kuweza kuwaeleza wananchi kuhusu jambo hili ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kuwasaidia kupata huduma hii bila kadhia zozote.
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge
Mbunge Korogwe Mjini
Mhe. Dkt. Alfred James Kimea
Tarehe 04 Aprili, 2023