Machali umekaririwa mara kadhaa kwenye vyombo vya habari ukidai kwamba kama Mbatia angevuliwa uenyekiti basi ulikuwa tayari kuhama chama. Pia umekaririwa mara kadhaa ukidai kwamba huwezi kubaki ndani ya NCCR Mageuzi endapo Kafulila angefanikiwa kuwa mwenyekiti wa chama.
Je, upo NCCR Mageuzi kwa sababu ya Mbatia ama kwa sababu ya sera na itikadi zake?
Je, kutokuwa tayari kuongozwa na Kafulila ni dalili za majivuno, ni dharau ama kutokujua unachokifanya?
Je, kuvuliwa uanachama kwa Kafulila ni katika jitihada za kuona kwamba nafasi ya uenyekiti wa Mbatia inalindwa kwa gharama zozote?
Je, hakukuwa na adhabu nyingine ya kumpa Kafulila zaidi ya kumvua uanachama?