Pole kaka yangu Mh. Mbatia. NCCR-Mageuzi na upweke wa Kafulila na Machali

Deogratius Kisandu

Verified Member
Dec 2, 2012
1,335
2,000
POLE KAKA YANGU Mh. Mbatia. NCCR-Mageuzi na UPWEKE WA KAFULILA na MACHALI.

Safari ya kisiasa ina ugumu sana hasa kama unafanya kazi na wachuma pesa na sio Wazalendo. Najua fika uliwasaidia sana David na Moses ukawapa maisha mpaka wakawa Wabunge na tambua hawahawa ndio walikufarakanisha na tambua hawahawa ndio wamekimbia chama tena kipindi ambacho bado afya yako haijakaa sawa.

Nimeamini kweli umdhaniae ndiye Kumbe siye yaani anakupenda tu wakati WA faraja au akiwa na shida ya ubunge lakini akikosa hana habali na wewe. Maana pia utakimbiwa na Kiongozi mwingine.

Pole kaka angu James na hizo ndizo Siasa za Malimbukeni WA Tanzania wasio jali UTU WA MTU Bali maslahi tu. Mungu akupe afya ili upone, ugonjwa wako unatibika soma Biblia yote kitabu cha Tobiti na utajitibu mwenyewe naamini Padre Tomy anajua hicho kitabu vizuri sana atakusaidia.

Maisha sio hivyo tu, na hisi sana UKAWA hawana habari na wewe kabisa hata kukujulia hali kama ilivyo kwa Mh.Lema huko gerezani kutembelewa mpaka waone haya ndio waende. Mungu ni mwema kwa kila MTU. Hata Mimi Deogratius Kisandu nilipopata ajali kwenye uchaguzi mdogo WA udiwani Sengerema mwaka 2013 hakuna aliyethamini mwili wangu zaidi ya ajali kupotoshwa na kuzushiwa ugaidi na ujambazi, huwezi amini nimeumilia maumivu mpaka Mungu akasema sasa basi utapona kwa nguvu za Roho Mtakatifu.

Mungu akutie nguvu na akupe afya nzuri wewe na familia yako ili urudi kwa kasi kulijenga Taifa. Wasaaalaaam

Deogratius Kisandu.
31. 12. 2016
 

Mndali ndanyelakakomu

JF-Expert Member
Dec 14, 2016
12,963
2,000
Mkuu chama sio ukoo ukaogopa kuhama sasa kama hawajali wengne yeye watamjali vp Siku zote ukiona kambi inakimbiwa jiulize nn kinawakimbiza?
 

Nyakageni

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
14,811
2,000
Kisandu una stress mbaya sana. Nakushauri rudi Kahama pale shule yako ya zamani ya Sr. Irene ukafanye kazi. Mara uponde ukatoliki mara uponde vyama vya siasa. Si utulie tu au uhamie CCM??
 

IBRAHIM KAUKI

JF-Expert Member
Jan 14, 2014
544
250
Kisandu una stress mbaya sana. Nakushauri rudi Kahama pale shule yako ya zamani ya Sr. Irene ukafanye kazi. Mara uponde ukatoliki mara uponde vyama vya siasa. Si utulie tu au uhamie CCM??
mbna yypo ccm?
huyu anatakiwa apelekwe mirembe akafanyiwe check up ya kichaa cha mbwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom