ON STAR TV LIVE: Demokrasia Tanzania na Nafasi ya Vyama vya Upinzani

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
JUMAPILI ya Leo 23.04.2012 Mjadala wetu tunauelekeza katika kutathimini Ukomavu wa Demokrasia na nafasi ya vyama vya Upinzani NCHINI katika kufanikisha hitajio la watanzania juu ya Utawala bora na uwajibikaji.

Wageni wallop Studio wataonyesha njia tu, tathimini na mawazo ya uchambuzi yanahitajika kutoka kwa washiriki kupitia forums, SMS na simu

Dar atakuwepo
Nd.Sam Ruhuza NCCR
Nd. Abdul Kambaya CUF

Mza
Jimmy Luhende TAASISI YA UTawala bora na Demokrasia
Shaman ITutu ADC
Grayson Nyakarungu CDM

Reflection point: matukio Bungeni wiki hii

Karibun kwa ma
Mjadala
 
Yahya tunashukuru sana ndugu yangu kwa Mada ya Leo, napenda kutoa rai yangu kwa serikali ya CCM kuwa wakubali kuwa mfumo wa utawala na uongozi tulio kuwa nao kwa takribani miaka 50 umeshindwa vibaya sana kwani hauna uwajibikaji wa moja kwa moja kwa wananchi hivyo hawatutendei haki sisi wananchi, watupe nafasi tujaribu mfumo mpya, naunga mkoni sera ya majimbo kwani itarejesha madaraka kwa wananchi na wananchi kuwajibisha viongozi wao moja kwa moja, na ni mfumo rahisi kusimamia rasilimali zetu.
 
mkuu Yahya,luhende hatambui kuwa kuhama chama ukiwa na wafuasi inamaanisha kuwa kundi la mtazamo mmoja linaweza kukubaliana kuhama?au anashindwa kutambua maana ya democrasia?au anadhani democrasia ni ya mtu mmoja mmoja pekee?tafadhali atuweke sawa!
 
huyu jama wa ADC anaongea uongoo asisingiziee katibaa maana amekua mwanachama wa CUF kama kiongozimuda wote huo alikua haoni huo upungufu anaouongelea sas na si tu janja ya wanasiasa wengi wakihisi maslahi yao yako shakani wanazusha visingizio vingi
 
Demokrasia ndani ya nchi yetu bado sana. Hadi pale tutakapopata mabadiliko makubwa ya kiuongozi! Siku ccm ikiangushwa, itakwenda kujipanga upya na wakirudi watakuwa ni chama cha wananchi na cha kidemokrasia. Tatizo lingine ni mfumo unaowaruhusu viongozi wa vyama kushika nafasi za uongozi serikalini. Hii inasababisha kushindwa kutenganisha siasa na uwajibikaji wa kiserikali. Chama kinashindwa kuiwajibisha serikali.
 
Binafsi naona Democrasia inakuwa kwa kwa kadri siku zinavyokwenda. Mfano kinachotokea leo bungeni ni ishara ya kukubalika kwa vyama vya upinzani kiasi kwamba ya wabunge hasa kutoka chama tawala wanauona MLANGO mwingine nje ya chama tawala, hii inawasukumu kutetea dhamira zao kuliko kuwa wanafiki. Kuhusu ADC tuwapongeze kwani bado vyama vya upinzani vinahitajika kwa taifa kubwa kama hili (japo sisi tuliowengi tungependa kuona vinaungana) Lakini kwa maelezo ya Kamishina wa ADC studioni Mwanza napata wasi wasi Aidha wameondoka CUF kwa jaziba hawajui wanachokisimamia au wametumwa kuvuruga upinzani uliopo sasa. Kwa maelezo yake amejipambanua pasinashaka kwamba wamekuja kuvishambulia vyama vya upinzani. Ndiyo maana wamekuja na bendera iliyosawa kabisa na vyama vilivyopo tofauti ni mpangilio wa rangi tu. Nasasa wanatafuta pale ilipo bendera inayofanana na chama chao wanatundika ya kwao. Tunawasiwasi mkubwa na ujio wa ADC,tusubiri tuone, time will tell.
 
Mkuu Yahya,
Kwanza nakupongeza sana kwa kuendesha kipindi live hapo Star TV, huku ukiwa interactive na Jamii Forums. Mimi niko hapa mjini Dodoma nikifuatilia kwa makini huu mjadala. Nimefarijika sana niliposikia jina la Jamii Forums likitajwa kwenye kipindi chako.

Natoa pongezi zangu za dhati kwako kwa uongozi mzima wa Star TV kwa kuwa ni kituo pekee cha Televisheni kilichotanguliza mbele zaidi maslahi ya taifa katika kujadili hoja bila upendeleo au kuegemea chama fulani.

Hongereni sana.

Pasco wa JF!.
 
Demokrasia bado iaminywa, na si kitu cha ajabu ukiona misimamo ya wabunge wa CCM inayoonekana kupingana na serikali inatekwa na kikao cha chama kinachoitwa 'Party caucus'
 
Yahya lazima tukubali kwamba Demokrasia ni process na bado vyama vetu hasa vya upinzani vanendeleakukuwa lakini pia vinachukuwa tàadhari dhidi ya mamluki na wavuruga vyama tunakumbuka NCCR.
Tukubali jukumu la la kujenga demokrasia ndani ya chama ni ya wananchama kuvikimbia vyama si solution.

Tofauti na ccm ni chama tawala wananchi wanachama wake wanatoka toka kutokana na kukiuka miiko ya uongozi.
 
Bila vyama vya upinzani thabiti serikali inalala,kwa madudu ya ripoti za kamati za bunge,ripoti ya CAG na madudu mengi. Nadhani tuelewa wazi kuwa kazi inayofanywa na chadema ndani na nje ya bunge si ya kubeza,na sasa tunaona serikali inavopaswa kuwawajibisha mafisadi,na wale waliokwapua mali zetu. Mwisho nashauri tufike hatua msajili afute vyama vya siasa visivo na uwakilishi bungeni,lengo la vyama si kuwa taasisi au kampuni au chama cha ushirika,tunahitaji chama cha kuwawakilisha wananchi ktk chombo cha
 
Yahya , tusiwe wanafiki chama chenye demokrasia ndani yake , Tanzania hakijaundwa!
Ccm , Chadema, Nccr , Cuf vyote havina demokrasia ya ndani.
Mif. Michache
Rejea issue ya ccm na RIP H.Kolimba
Cuf wamemtimua Mbunge kwenye chama lakini Mbunge husika yuko mjengoni.
Nccr imemtimua Mbunge ambae mjengoni anadunda kama kawaida.
Jiulize ni kitu gani kinachofanya hadi leo nchi hii isiwe na ridhaa na wagombea binafsi wasio na vyama.
Eti serikali ilipinga mahakamani mgombea binafsi serikali ya chama gani ? Tusiwe wanafiki ! Si isemwe Ccm haijakubali mgombea binafsi! Badala ya kusema serikali.
 
mada nzur sana, ni kwel kuna baadhi ya vyama vya siasa vinaongozwa na watu wachache na wanavimiliki, huyo jamaa wa ADC amenishangaza na katiba yao na jins wanavyosimamia nidhamu kitakufa mapema, CUF wanatoa maelezo ila in reality wanapotea kwenye siasa taratibu, kwa ufupi ni kwamba NCCR & CDM kwangu naona ni vyama vyenye maono vinahtaj kuepuka fitna za ccm tu.
 
Abdul Kambaya unaitetea cuf labda kwa kuwa ndipo unapopatia mkate wako. Kama uchaguzi ulikuwa umetawaliwa na udini, analiongeleaje suala la wao kuporomoka katika uchaguz wa ubunge na udiwani katika wilaya ya kondoa ambapo cuf ilikuwa ina nguvu sana na pia ni wilaya yenye waislam wengi? Cuf kondoa imekufa kabisa. Kiufupi, kinachoiua cuf ni kuwa, CUF NI MAALIM SEIF NA MAALIM SEIF NDO CUF. Cuf ni kampuni ya maalim. Na nionavyo mimi, cuf haitainuka tena. Imekumbwa na tufani
 
Yahya, kiukweli huyu Bwana wa ADC ametuchanganya sana, ameibua maswali mengi kuliko majibu. Naomba kumuuliza miongoni mwa marais wakali sana barani Afrika ni Rais Kagame wa Rwanda, anaipimaje nafasi ya Rwanda chini ya uongozi mkali wa Rais Kagame? Na maelezo ya chama chao kwamba ni bwelele tu. Hivi kweli kipo chama cha namna hiyo Duniani???
 
Mkuu Yahya,
Kwanza nakupongeza sana kwa kuendesha kipindi live hapo Star TV, huku ukiwa interactive na Jamii Forums. Mimi niko hapa mjini Dodoma nikifuatilia kwa makini huu mjadala. Nimefarijika sana niliposikia jina la Jamii Forums likitajwa kwenye kipindi chako.

Natoa pongezi zangu za dhati kwako kwa uongozi mzima wa Star TV kwa kuwa ni kituo pekee cha Televisheni kilichotanguliza mbele zaidi maslahi ya taifa katika kujadili hoja bila upendeleo au kuegemea chama fulani.

Hongereni sana.

Pasco wa JF!.

Yahya,mada iko poa kabisa,kinachoniuudhi ni huyo jamaa wa CUF anavyofikiri watu bado mbumbu wa akili anavyoipondea CDM eti mtu alitaka kugombea uenyekiti aliundiwa tume ya wazee,hajui kuwa CDM wako makini na kila kitu kinatathminiwa kabla.....yeye aumizwe kichwa kufikiria jinsi ya kujenga chama chake aachane na CDM ambayo speed yake ni kubwa mno hata yeye anajua...wao waangalie walipojikwaa baada ya kuamua kuingia ubia na CCM na kama hajui akae akijua 2015 CDM Zanzibar kama katiba bado itakuwa inaruhusu muungano.....
 
Nadhani ADC itakufa hivi karibuni kwa mujibu wa katiba yao ambayo nidhamu kwao si kitu muhimu! Hata ndani ya familia kuna utaratibu ambao imejiwekea kwa ustawi familia hiyo.
 
Niwapongeze kwa kuamua kujadili mustakabali wa taifa letu na demokrasia, demokrasia tuitafsiri kwa wigo mpana sio kama ndugu wa adc anavyo tafsiri na anaposema katiba za vyama kwenye midaharo ni lazima ataje chama na ibara inayosema hivyo sio kushambulia pasipo misingi mnawaacha watanzania hewani pasipo kuwaonyesha msingi wa mada.
 
Pamoja na kwamba demokrasia ni mchakato lakini lazima tukubali kuupokea na kuwajibika, mfano chama kinachotawala kinasita kukubali kwa dhati demokrasia na ndo maana hata pale vyama vya upinzani vinapotoa mwonozo wa uwajibikaji watu hukaa kama kamati kuokoana, leo hii tunashuhudia kushindwa kwa watawala wetu katika ulinzi wa mali ya Uma, lakini bado hakuna uwajibikaji hawataki kuachia madaka ama nyazifa hata pale walipokiri kushindwa, ona option B ya kukusanya sahihi watanzania tulitegemea kupata sahihi hata za bunge zima kumuajibisha waziri mkuu na serikari yake lakini wapi, hii ni kwa kua hoja ile imeletwa na wapinzani na hapa unapata picha kwanba laiti kama bunge lingekua na nusu ya wapinzani tungesonga mbele
 
Kuna kazi ya kufikia malego ya demokrasia ya kweli ndani ya vyama vya siasa, ni muhimu vitambue nini mtanzani anahitaji. Sasa kama kuna mfumo ulio mzuri ni vema vikaungana na sio kupigana vijembe kama hapo vinavyopigwa na kambaya wa cuf na itutu wa adc.
 
Back
Top Bottom