Kulikuwa na haja ya kumtimua Kafulila NCCR? Mh. Moses Machali Live on Star TV

Kitendo cha kumfukuza bwana Kafulila ni kupunguza nguvu ya Upinzani. Je, hamuoni kuwa mnadhoofisha nguvu ya upinzani bungeni ilhali Mh aliomba mumsamehe?
 
Je, haoni kuwa kufukuzana si chanzo cha kusolve matatizo bali kutengeneza matatizo?

Je, anakubali kuwa Kafulila bado ana nguvu kwan tumeona wanazomewa huko Kigoma wanavyoenda kusafisha upepo?
 
Ushauri kwa huyo Machali:

Yahya hebu mwambie huyo apunguze sauti kwani anamtolea nani mimate yake hapo au kuna ugomvi? And by the way yuko pointless sana katika mambo anayoyatoa hapo..
 
Kwangu mimi mmoja aliyechangua kukivuruga NCCR ni Machali... na cha kushangaza baada ya kutimuliwa kwa Kafulila jamaa kaukwaa ukatibu uenezi!!

Naomba kumuuliza kwanini anatumia nguvu nyingi kumlaumu Kafulila wakati kimsingi hata yeye anaonekana ana matatizo mengi ya ubinafsi na hasira zisizo na tija.
 
No research no right to speak.
Order ya mahakama!!
NCCR wasichukue hatua zaidi ya hiyo ya kumvua uanachama!!
 
Ushauri kwa huyo Machali:

Yahya hebu mwambie huyo apunguze sauti kwani anamtolea nani mimate yake hapo au kuna ugomvi? And by the way yuko pointless sana katika mambo anayoyatoa hapo..
Dogo anaongea kwa jazba sana...
 
Yahya,

Machali angetuambia na kesi ya msingi aliyofungua Kafulila ni nini?

Ndio itafaaa kujua manatiki ya order ya mahakama.
 
Yahya Mohamed, Naomba kuuliza swali:

Ni kosa gani kubwa aliliofanya Kafulila mpaka akafukuzwa chama?
 
Mnadai moja kati ya tuhuma zilizopelekea kumfukuza Kafulila ni kuita chama 'CCM'.

Je, kuna makosa gani kama mtu kaona hizo ishara za chama kuwa kibaraka wa CCM, na njia pekee aliyoiona ni kusema kusudi chama kibadili mwelekeo wake huo wa ki-CCM CCM?
 
Haya swali lako limesomwa!
SWALI KWA MH MACHALI:

Kabaa ya kufukuzwa Mh Kafulila, ulinukuliwa na gazeti moja linalotoka Kila Jumatano (MwanaHalisi) Ukimtuhumu Kafulila Kwamba anataka kumpindua Mwenyekiti Mbatia. Na tayari Kafulila amevuliwa madaraka aliyokuwa nayo na Kukabidhiwa wewe (Katibu mwenezi wa Chama).

Je, hiyo sio fitna ya Kisiasa? Je, huoni pia ni kikwazo cha kukijenga chama hasa kutokana na kambi ya Kafulila kuona wewe ni moja ya chanzo cha mgogoro huo?


NAAMINI NDUGU YAHYA UTALISOMA SWALI LANGU HILI
 
Inaonekana Mh.Machali anamchukia sana Kafulila,sijui kwanini,au kwa sabb ana mashiko kuliko wewe?naona unatokwa povu tu hapo!
 
Machali atupe msimamo wake kuhusu katiba mpya na msimamo wake maana hakutoka ndani ya bunge wakati chadema wanatoka bungeni kupinga muswaada wa katiba mpya?
 
Machali unadhalilisha utu wako kwa kumuita James Mbatia kuwa ni taasisi!

Hapana, uenyekikiti wake ndo wenye taasisi! Pia naomba kujua kuwa baada ya kumtimua David na Mbatia atachunguzwa au ndo ataenziwa au anaogopwa?

Pia naomba Machali utoe msimamo kwa Mbatia kumfungulia kesi Halima Mdee mpinzani mwenzake huko ni kujenga upinzani au kuutetea u CCM?
 
Watanzania hatujazoea maauzimu magumu kama hayo, tumezoea mtu akikosa anaamishiwa pengine.

SWALI LANGU:

Katika kumfukuza kafulila katiba ya NCCR Mageuzi imeeleza nini kuhusu hilo? Pia mhe Machali atueleze vipi Mhe kabwe anahusika na mgogoro huu.


MAONI YANGU:

Dawa pekee ya migogoro hii ni katiba mpya ya kuruhusu mgombe binafsi
 
Kama mmeambiwa msichukue uamuzi wowote, sasa kwanini mmeandika barua kwenda ofisi ya spika?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom