Wakati Polisi wanatafakari vifo mbalimbali vya wenzao vinavyotokana na vipigo kutoka kwa watu wanaosemekana wana hasira kali,Leo majira ya saa tatu asubuhi katika mataa ya chang'ombe wameshikana mashati na Mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi pale Mwanajeshi huyo aliposhuka na kuanza kuongoza Magari ili gari alilopanda liweze kupita.Trafiki wapatao wanne walifanikiwa kumdhibiti na Mwanajeshi alifanikiwa kuponyoka na kudandia gari iliyokuwa mbele na kutokomea.
MY NOTE:
Kwa nini Majeshi yetu na hasa hawa askari wa vyeo vya chini wanaonyesha mfano mbaya kwa Raia?.