white wizard
JF-Expert Member
- May 18, 2011
- 8,618
- 13,891
Leo nimepita pale Mbagala Mzinga ambapo mabomba ya gesi ya Mtwara yanafikia baada ya kutoka bandari,wamejengea uzio ambao umepakwa rangi ya kijani na njao!utadhani ni ofisi ya CCM!ndio nikapata wasaha wa kumuuliza mfanyakazi mmoja,kulikoni wameamua kupaka rangi hiyo, akasema eti wameamua kupaka hivyo baada ya kupata maagizo toka juu,ili mheshimiwa atakapopita pale akienda kufungua kiwanda cha Bahresa apaone ili pa mvutie!
Japo nasikia ilileta mzozo wa ndani kwa ndani,kuwa inakuwaje itumike rangi ya chama fulani wakati huo ni mradi wa kitaifa?
Japo nasikia ilileta mzozo wa ndani kwa ndani,kuwa inakuwaje itumike rangi ya chama fulani wakati huo ni mradi wa kitaifa?