Katika ajali ya ndege Iliyotokea juzi CCM imeonesha kwanini ni Chama Tawala mpaka leo na kwanini CHADEMA imeshindwa hata kupaka rangi ofisi zake

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,220
9,647
Ndugu zangu katika Ajali ya Ndege Iliyotokea Juzi imeonyesha Kwanini CCM imeendelea kuaminiwa na watanzania katika kila uchaguzi mpaka leo hii, CCM imeonyesha sababu za wananchi Kuendelea kuwa na Imani nayo,CCM imeonyesha sababu ya watanzania kuipigania na kuilinda kwa nguvu zao zote na kwa gharama zote kuhakikisha CCM Inaendelea kuwepo madarakani

Wakati CCM imeonyesha kuguswa ,kuumizwa,kuhuzunishwa,kusikitishwa na ajari hii iliyochukua uhai wa watanzania wenzetu ,Wao CHADEMA wameonekana kukifanya suala hili kuwa la kisiasa na mtaji wao katika kipindi hiki Cha majonzi, wakati CCM imejikita katika kuunganisha Taifa na watanzania wote, kuwaombea majeruhi kupona haraka, kufika eneo la tukio kutoa msaada wa kibinadamu kwa wahanga, Wao CHADEMA ni Kama imekuwa furaha kwao, Ni Kama wamepata Cha kuongea, Ni Kama walitamani wapoteze wote maisha ili wapate vya kuongea wiki nzima,Ni Kama walikuwa wanasubiri vya kupost kwenye kurasa zao, Ni Kama walikuwa Kama mafisi wanaosubiri mkono udondoke waokote, hawakufurahishwa na habari za uokoaji wa abiria takribani 26

Chadema imekuwa na Tabia Kama za mchawi anayeweza kuuwa hata mwanaye, Hawafurahishwi Wala kupenda kusikia habari za Rais wetu kuagiza kupewa ajira kwa kijana Majaliwa, wao Ni kupinga pinga kila kitu, wakati CCM inahangaika na wahanga kuwasaidia, wao wanahangaika kuitisha mikutano na waandishi wa Habari kuropoka utoto na ujinga

Cha kusikitisha Ni kuwa CHADEMA Tangia kisajiliwe kwake miaka ya 90 mwanzoni lakini mpaka Leo kimeshindwa hata kupaka tu Rangi katika ofisi zao, wameshindwa hata kubadilisha madirisha ili yaweze kupitisha hewa vizuri wanapokuwa wamerundikana mule ndani,wameshindwa hata kubadilisha milango ikawa na muonekano mzuri, Hata pa kuweka Bendera tu wameshindwa kupaweka katika muonekano mzuri, kimekuwa Ni chama Cha kitapeli na Cha matukio, kinabaki Ni chama Cha kutafuna Ruzuku na kila aina ya Senti inayoingia katika mifuko yao

Ndio sababu hakina dira Wala muelekeo, hakieleweki kinasimamia Nini na Hakina wakukipa muelekeo kwa kuwa wanaopaswa kuonyesha njia nao pia walishapoteza Ramani na Dira hivyo wamebaki wanaburuzana tu kwa kila mtu kujifanya anaijuwa njia huku ikionekana wazi kinaelekea korongoni ambako hakitaweza kujinasua.

Hongera Sana kwa CCM na serikali ya CCM kwa namna ilivyohangaika tangia kutokea kwa ajari hii mpaka Leo hii, ninampongeza Sana Rais wangu mama Samia kwa maelekezo yake na naamini uchunguzi ukikamilika utawekwa hadharani ili kubaini chanzo Cha ajari hii

Kazi iendeleee,mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Amini Amini nawambia ipo siku ccm itaondoka madarakani na hiyo siku haipo mbali tuombeana afya njema tu.
Hakuna chama chenye uwezo wa kuitoa CCM madarakani maana wananchi Wana Imani kubwa Sana na CCM na kuvipuuza vyama vya upinzani
 
Ndugu zangu katika Ajari ya Ndege Iliyotokea Juzi imeonyesha Kwanini CCM imeendelea kuaminiwa na watanzania katika kila uchaguzi mpaka leo hii, CCM imeonyesha sababu za wananchi Kuendelea kuwa na Imani nayo,CCM imeonyesha sababu ya watanzania kuipigania na kuilinda kwa nguvu zao zote na kwa gharama zote kuhakikisha CCM Inaendelea kuwepo madarakani



Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Back
Top Bottom