Tina
JF-Expert Member
- Jul 9, 2007
- 572
- 579
TAKUKURU sasa waingia bandari
.Vigogo wanaoomba kazi TPA wamulikwa
.Uongozi wa sasa nao hauko salama
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inachunguza nyendo za viongozi wa sasa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na baadhi ya waliomba nafasi katika mamlaka hiyo.
Habari za ndani ya TAKUKURU zimeeleza kwamba uchunguzi umeanza baada ya kuwapo taarifa za baadhi ya watu waliwahi kutuhumiwa ufisadi kuomba kazi TPA huku uongozi nao kuwa na maamuzi yenye utata kuhusu mamlaka hiyo.
"Kuna wanaowania nafasi za juu za TPA wakati walikotoka waliondoka kwa kashfa za ufisadi na sasa wanataka kurudi kuchota kwa hiyo wanawachunguza. Lakini pia wanafuatilia nyendo za viongozi wa sasa kutumia vibaya madaraka wakishirikiana na viongozi wa wizara," kinaeleza chanzo chetu.
Miongoni mwa wanaoomba nafasi katika TPA wamo watu waliowahi kushika nafasi za juu katika taasisi za umma na wengine wamo madarakani wanakotuhumiwa kujihusisha na ufisadi.
Ndani ya TPA kwenyewe hali si shwari baada ya kuelezwa kwamba kuna utata katika baadhi ya maamuzi ikiwamo kulazimisha kuingizwa kwa tozo la ufuatiliaji mizigo kwa mtandao (e-CTN) na uamuzi wa kuvuruga vitengo vya ununuzi kwa malengo yenye harufu chafu.
Tayari imefahamika kwamba TPA na uongozi wa wizara unajiandaa kupingana na uamuzi wa kisheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) ili kulazimisha kuanza kwa e-CTN.
Kuhusu suala la bozi za ununuzi, imeelezwa kwamba uongozi wa TPA chini ya Madeni Kipande, umefanya marekebisho kwa mara ya pili sasa ya kuvuruga vitengo vya ununuzi na kuwaingiza watu aliowahi kufanya nao kazi TANROADS.
Kipande aliokolewa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, aliyevunja bodi ya TPA iliyokua imeandaa mashikata dhidi yake ikitaka kumsimamisha kabla ya kuvunjwa kwa bodi hiyo.
Bodi hiyo iliandaa mashitaka ikiwamo matumizi mabaya ya madaraka, udhalilishaji wa kijinsia na kudharau maagizo ya bodi, tuhuma ambazo hazikujibiwa na badala yake bodi hiyo ikavunjwa.
Bodi hiyo iliyovunjwa iliundwa kwa mbwembwe baada ya kuvunjwa kwa bodi ya awali iliyosheheni watu wenye hadhi na uwezo katika sekta ya bandari na uchukuzi.
Hali hiyo ilimfikia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye hata hivyo, alikwama kukutana na wadau katika kikao alichoitisha kutokana na kuingiliana na shughuli nyingine za serikali.
SOURCE: Kulikoni Ijumaa, Desemba 6, 2012