KULIKONI: TAKUKURU sasa waingia bandari


Tina

Tina

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2007
Messages
571
Likes
75
Points
45
Tina

Tina

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2007
571 75 45
TAKUKURU sasa waingia bandari

.Vigogo wanaoomba kazi TPA wamulikwa
.Uongozi wa sasa nao hauko salama

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inachunguza nyendo za viongozi wa sasa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na baadhi ya waliomba nafasi katika mamlaka hiyo.

Habari za ndani ya TAKUKURU zimeeleza kwamba uchunguzi umeanza baada ya kuwapo taarifa za baadhi ya watu waliwahi kutuhumiwa ufisadi kuomba kazi TPA huku uongozi nao kuwa na maamuzi yenye utata kuhusu mamlaka hiyo.

"Kuna wanaowania nafasi za juu za TPA wakati walikotoka waliondoka kwa kashfa za ufisadi na sasa wanataka kurudi kuchota kwa hiyo wanawachunguza. Lakini pia wanafuatilia nyendo za viongozi wa sasa kutumia vibaya madaraka wakishirikiana na viongozi wa wizara," kinaeleza chanzo chetu.

Miongoni mwa wanaoomba nafasi katika TPA wamo watu waliowahi kushika nafasi za juu katika taasisi za umma na wengine wamo madarakani wanakotuhumiwa kujihusisha na ufisadi.


Ndani ya TPA kwenyewe hali si shwari baada ya kuelezwa kwamba kuna utata katika baadhi ya maamuzi ikiwamo kulazimisha kuingizwa kwa tozo la ufuatiliaji mizigo kwa mtandao (e-CTN) na uamuzi wa kuvuruga vitengo vya ununuzi kwa malengo yenye harufu chafu.

Tayari imefahamika kwamba TPA na uongozi wa wizara unajiandaa kupingana na uamuzi wa kisheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) ili kulazimisha kuanza kwa e-CTN.

Kuhusu suala la bozi za ununuzi, imeelezwa kwamba uongozi wa TPA chini ya Madeni Kipande, umefanya marekebisho kwa mara ya pili sasa ya kuvuruga vitengo vya ununuzi na kuwaingiza watu aliowahi kufanya nao kazi TANROADS.

Kipande aliokolewa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, aliyevunja bodi ya TPA iliyokua imeandaa mashikata dhidi yake ikitaka kumsimamisha kabla ya kuvunjwa kwa bodi hiyo.

Bodi hiyo iliandaa mashitaka ikiwamo matumizi mabaya ya madaraka, udhalilishaji wa kijinsia na kudharau maagizo ya bodi, tuhuma ambazo hazikujibiwa na badala yake bodi hiyo ikavunjwa.

Bodi hiyo iliyovunjwa iliundwa kwa mbwembwe baada ya kuvunjwa kwa bodi ya awali iliyosheheni watu wenye hadhi na uwezo katika sekta ya bandari na uchukuzi.

Hali hiyo ilimfikia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye hata hivyo, alikwama kukutana na wadau katika kikao alichoitisha kutokana na kuingiliana na shughuli nyingine za serikali.

SOURCE: Kulikoni Ijumaa, Desemba 6, 2012
 
Tina

Tina

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2007
Messages
571
Likes
75
Points
45
Tina

Tina

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2007
571 75 45
KULIKONI NAONA KAMA WAMEOGOPA KUWEKA VITU VINGI, JE MUNAJUA KIINI CHA MH. MWAKYEMBE KUMLINDA KAIMU MKURUGENZU MKUU WA TPA BWANA MADENI KIPANDE KWA NGUVU ZAKE ZOTE BILA KUJALI SHERIA AMBAZO ANAZIFAHAMU VIZURI?. NAJUA KUNA WALOKUNYWA MAJI YA BENDERA WATATETEA LAKINI HAWANA UWEZO WA KUBADILI UKWELI AMBAO NI HUU:

Bwana Madeni Kipande aliyeletwa mwezi Agosti 2012 na Waziri wa Uchukuzi, Mh. Harisson Mwakyembe kama Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kwa mkwara wa “wiki mbili tu” ametimiza miezi kumi na tano sasa. Bwana Kipande hana uwezo hata chembe wa kuongoza taasisi nyeti na kubwa kama TPA yenye umuhimu mkubwa sio tu kwa maendeleo ya Tanzania bali hata kwa uchumi wa kanda ya maziwa makuu.

Inakera sana kuona kuwa Waziri Mwakyembe ambaye anajigamba kupiga vita rushwa na ufisadi wa mali ya umma alithubutu kumkingia kifua Kipande bila hata woga, huku moyoni mwake akijua kinaga ubaga kuwa “Waraka wa Ulanga” kuhusu Kipande ni ukweli mtupu. Kwa kweli inakera mno kuona kuwa Mh. Mwakyembe baada ya kupewa “Waraka wa Ulanga”; badala ya kumwajibisha Kipande aliishia kuivunja Bodi, bila shaka alifanya hivyo kwa kuzingatia maslahi yake binafsi.


·Mh Mwakyembe anayo ahadi ya Kipande kutumia Sh. 500 milioni za TPA kujenga nyumba ya wageni jimboni kwake, Matema beach.

·Kipande na Mwakyembe wanayo ndoto ya kugawana mamilioni ya pesa kupitia mfumo wa kukusanya taarifa za mizigo (ECTN), ambazo tayari zinapatikana bila hata malipo yoyote, hata hivyo SUMATRA waliupiga marufuku mfumo huu.

·Kipande na Mwakyembe wanaendelea na mkakati wa kifisadi kugawana kiasi cha sh 800 milioni kama fidia ya mapatano nje ya mahakama kati ya TPA na mkandarasi ambaye alishindwa kutimiza wajibu wake wa kujenga nyumba ya Meneja wa Bandari Tanga.


·Mwakyembe na Kipande hivi sasa wanatoa ajira kwa watoto wao, ndugu zao, jamaa zao na marafiki zao pasipo kificho tena kwa kukiuka taratibu za ajira pasipo woga na bila kuzingatia sheria na taaluma hata kidogo.


·Hivi sasa katika himaya ya Kipande na Mwakyembe, ajira kwa kuzingatia, ujimbo, udini na jinsia na bila kujali taaluma na weledi ndio kawaida. Imefikia hatua hivi sasa Kipande na Mwakyembe kuajiri watu katika ngazi za ukurugenzi, umeneja na maafisa waandamizi bila kujali muundo uliopo na taratibu za ushindani kabisa. Sio siri kuwa Bw Ali Pagali ambaye anafanya kazi kama Afisa Mkuu Utafiti Idara ya Mipango hana sifa ya kazi hiyo na ajira yake haikufuata taratibu kabisa.

·Kipande na Mwakyembe wanatoa marupurupu batili kwa viongozi wa wafanyakazi Bandarini (DOWUTA) yasiyo na tija kwa TPA ili kufumbia macho madhambi yanayoendelea ndani ya TPA. Mwakyembe amediriki hata kumteua Bwana Edmund Njowoka, kama mjumbe wa bodi ya TPA na hii imevunja sheria ya kuanzisha TPA kwa kuwa Njowoka ana mgongano wa kimaslahi wa kudumu na hatakiwi kabisa kuwa mjumbe wa bodi. Njowoka ni mfanyakazi wa TPA kama karani Bandari ya Mtwara na kwa uteuzi huu ni Bosi wa Kipande kama mjumbe wa Bodi; na wakati huo huo Kipande ni bosi wa Njowoka kama karani bandari ya Mtwara, huu kweli ni usanii uliopita mipaka!

·Kipande anawanyanyasa wafanyakazi na wengi wanakaa kimya kwa kuwa wanahofia kufukuzwa kazi. Kama inavyofahamika ajira ni za shida sana na madhara ya kufukuzwa kazi ni mabaya sana. Lakini unyanyasaji hivi sasa umekithiri. Baadhi ya wafanyakazi walisimamishwa kazi kwa ridhaa na utashi wa Kipande na Mwakyembe na tuhuma dhidi yao imeonekana kuwa ni uzushi. Wafanyakazi hawa hawajarudishwa kazini na wanaendelea kulipwa mishahara na marupurupu yao bila kufanya kazi, na kwa upande mwingine hii ni dhuluma dhidi ya haki zao za binadamu.

.Kipande na Mwakyembe pia wanatumia madaraka yao vibaya kwa kuwahamisha wafanyakazi bila kufuata muundo uliopo ili kuwakomoa kutokana na hulka zao za chuki binafsi. Baadhi ya wafanyakazi wamehamishiwa Makao Makuu, bandari za mwambao na zile za maziwa bila kufuata muundo uliopitishwa, kwa lengo la kuwakomoa na kuwanyanyasa pasipo sababu.

·Hivi karibuni Kipande na Mwakyembe wameshinikiza uhamisho wa Bi Beatrice Jairo, Afisa Mawasiliano na Bi Levina Msia, Afisa Mwasiliano Mwandamizi kwenda bandari za Nansio na Kasanga kinyume kabisa na taratibu za utumishi na haki za binadamu pia. Inawezekana vipi maafisa wa Mawasiliano kupelekwa kufanya kazi bandari ndogo ndogo za Nansio na Kasanga ambazo kimuundo wa utumishi hakuna vyeo hivyo. Pia mapato ya bandari hizo ni madogo mno hivyo kutokuhalalisha uwepo wa maafisa mawasiliano wakati wote na kwa kuzingatia kuwa majukumu yao katika bandari hizo hayahitajiki. Uamuzi wa Kipande na Mwakyembe ni utumiaji wa madaraka vibaya na hii ni itasababisha gharama kubwa zisizohitajika hasa kwa kuzingatia kuwa TPA inapashwa kufanya biashara kwa faida kubwa zaidi. Kwa uhamisho huu, walichokifanya Mwakyembe na Kipande ni uhujumu wa uchumi kwa kuwa haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma tena za walalahoi walipa kodi.

·Kwa hali yoyote ile kutofuata misingi ya utawala bora (lack of integrity), ufisadi, rushwa, uonevu, uzandiki, unyanyasaji, vitisho kwa wafanyakazi, matumizi mabaya ya madaraka, wizi wa pesa za umma na madhambi lukuki ambayo yamefanywa na Mwakyembe na Kipande katika kipindi hiki cha miezi kumi na tano "walipoiteka" TPA, haina budi mamlaka husika kuingilia kati ili kuokoa jahazi!
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,598
Likes
527
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,598 527 280
TAKUKURU wenyewe wala rushwa!
 
Tina

Tina

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2007
Messages
571
Likes
75
Points
45
Tina

Tina

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2007
571 75 45
TAKUKURU wenyewe wala rushwa!
Uko sahihi Mkuu, kuna kesi kibao zimepotea na hili ndilo tatizo na hakuna mtu wa kuwagusa. Wangekua wanachukuliwa hatua saa hizi wote wangeshika adabu. Tuna tatizo kubwa kama Taifa na tumepofushwa macho kiasi cha kutoyatizama mambo kwa HOJA na hapa utaona watu watakuja na majibu mepesi kwa maswali magumu. Watakuja watu wakisema, "AMENUNULIWA, ana WIVU WA KIKE, ANA CHUKI BINAFSI, AMEKOSA KAZI KILA SIKU BANDARI, SI MWENETU, ANATETEA MAFISADI" na kadhalika badala ya kuchambua hoja mstari kwa mstari na kuzijibu.
 
M

mtechnical

New Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
3
Likes
0
Points
0
M

mtechnical

New Member
Joined Dec 20, 2012
3 0 0
mwizi kapewa kazi ya kumkamata kibaka
 
Tina

Tina

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2007
Messages
571
Likes
75
Points
45
Tina

Tina

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2007
571 75 45
mwizi kapewa kazi ya kumkamata kibaka
Tusiache kupiga kelele!!! maana vibaka wakiiba wanafukuzana wenyewe, sasa mukiwaachia ndio wanaishia kugawana, dawa wakifukuzana na sisi tunawafuata na mapanga na mawe hadi mabondeni na kuwamaliza!! kelele ndio silaha ya kupunguza kama si kumaliza rushwa na ufisadi
 
Tina

Tina

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2007
Messages
571
Likes
75
Points
45
Tina

Tina

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2007
571 75 45
mwizi kapewa kazi ya kumkamata kibaka
Haya ndio majibu ya TAKUKURU na rushwa katika search engine je, kuna ufuatiliaji?:
About 36.300 results (0,32 seconds)

[h=2]Search Results[/h]
 1. [h=3]TAKUKURU YENYEWE INAJIUHUSISHA MOJ KWA MOJA NA ...[/h]sundayshomari.com/.../takukuru-yenyewe-inajiuhusis...‎Translate this page
  Aug 21, 2013 - "Ukiangalia kesi zilizoko mahakamani ambazo upelelezi wake bado ... wazi kuwa Takukuru ni miongoni mwa watu wanaopokea rushwa, ...


 2. [h=3]MICHUZI BLOG: TAKUKURU kujiunga IAACA kuwasaidia kujenga ...[/h]issamichuzi.blogspot.com/.../takukuru-kujiunga-iaaca-...‎Translate this page
  Mar 31, 2012 - Aidha Dr. Hoseah amekiri kuwa pamoja jitihada kubwa zilizofikiwa na TAKUKURU katika kupambana na rushwa bado rushwa ni changamoto ...


 3. [h=3]Rushwa anayoiona Sumaye: Takukuru mpo wapi? - Jamii Forums[/h]www.jamiiforums.com/.../334951-rushwa-anayoiona-...‎Translate this page
  Oct 8, 2012 - 20 posts - ‎14 authors
  Tume ya Kupamba na Kushiriki Rushwa Takukuru haina maana yoyote. ... na Kuilinda Rushwa Tanzania...eti mpaka leo bado wanachunguza ...Mbunge Musa Azzan Zungu akamatwa kwa tuhuma za Rushwa ...
  31 Oct 2012

  Bashe atumika kutoa rushwa Nzega - Takukuru mpo? - JamiiForums
  25 Sep 2010

  Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU - Page 6 - JamiiForums
  28 Oct 2009

  TAKUKURU na Siku ya Maadili Kitaifa - Jamii Forums
  10 Dec 2007

  More results from www.jamiiforums.com

 4. [h=3]Mbunge Zungu, wenzake bado wachunguzwa na Takukuru ...[/h]www.infocomtechnologies.com/.../mbunge-zungu-we...‎Translate this page
  Nov 20, 2012 - Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani hapa, imesema bado inakamilisha uchunguzi ili kuwafikisha mahakamani ...


 5. [h=3]takukuru kwa kushirikiana wadau wa mapambano dhidi ya rushwa ...[/h]


  kajunason.blogspot.com/.../takukuru-kwa-kus...‎Translate th


 

Forum statistics

Threads 1,252,239
Members 482,048
Posts 29,801,456