Kulikoni Nembo ya BAVICHA!

Kulikoni Nembo ya BAVICHA!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,200
Reaction score
7,568
Kwa wale wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kuwa mnamo tarehe 27 february 2013, BAVICHA walitangaza mchakato wa kutafuta Nembo yao.Tangazo lao lilikuwa limewekwa hapa jukwaani na mdau mmoja likiwa na kichwa cha habari "BAVICHA YAANZISHA SHINDANO LA KUPATA NEMBO YAKE".Sasa nilichokuwa napenda kufahamu; hivi zoezi hilo liliishia wapi au haya mambo ya Video yashaanza kuathiri shughuli za chama na wadau kujikuta wakipoteza "concetration" kwenye mambo ya msingi?
 
Kuna haja gani BAVICHA kuwa na nembo yake. Baba awe na nembo (CDM)'; Mwana / Binti awe na nembo; na je Mama naye akihitaji nembo??? Sioni haja ya nembo kwa kila mwanafamilia. CDM ni familia moja hivyo nembo ya chama inafaa kutumiwa na wanafamilia wote.
 
Mbona wewe unajina lako na baba yako ana jina lake?
 
Kuna haja gani BAVICHA kuwa na nembo yake. Baba awe na nembo (CDM)'; Mwana / Binti awe na nembo; na je Mama naye akihitaji nembo??? Sioni haja ya nembo kwa kila mwanafamilia. CDM ni familia moja hivyo nembo ya chama inafaa kutumiwa na wanafamilia wote.
Tanzania ni moja lakini tuna nembo ya taifa, nembo ya Ikulu, Nembo ya halmashauri ya jiji la Dar es salaam, Nembo ya Halmashauri ya Ilala N.K. Unasema je hapo? Je! hili linaifanya Tanzania kutokuwa moja!
 
Siasa za matukio...
Siasa huathiri trend ya matukio na matukio huathiri siasa na hali hiyo ni hali isiyoepukika katika maisha ya kila siku.Cha msingi tu ni kujaribu ku "regulate" na kudhibiti hali ya mambo.
 
Back
Top Bottom