Kulikoni ndoa za siku hizi?

Kulikoni ndoa za siku hizi?

Maisha pesa

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2015
Posts
681
Reaction score
632
Vijana wengi wanatamani kuoa na wasichana wengi wanatamani kuolewa. Mimi ni miongoni mwa vijana wanaojiandaa kuoa na hivyo niko katika kipindi cha kuyatafakari maisha ya ndoa.

Jambo moja ambalo limenishangaza ni wimbi la kuachana wanandoa. Asilimia kubwa ya marafiki na jamaa zangu walionitangulia kwenye ndoa hawako pamoja leo hii. Siyo wadada wala wakaka ukija kusikia eti walishaachana. Tena wapo waliokuwa wanapendana sana kiasi kwamba niliamini ni kifo tu kingewatenganisha lakini leo hii nasikitika kusikia wameachana.

Tatizo ni nini wakuu? Zamani watu walikuwa wanaachana lakini siyo sana kama siku hizi make ilikuwa ni aibu kuachika na baadhi ya makabila mtoto wa kike alikuwa anaambiwa akiachika asirudi tena kwao, kwa lengo la kumfanya aiheshimu ndoa yake na awe mvumilivu.

Baadhi ya watu wazima wameniambia kuna tatizo la feminism, wanawake wengi hasa wenye vipato wanapenda kushindana na wanaume hawajishushi kama wanawake wazamani ambao hata wakipigwa walikuwa wanavumilia tu.

Pia michepuko ya wanaume ni tangu zamani lakini siku hizi mwanaume akichepuka na mwanamke naye anataka kuchepuka ili alipize mwishoe ni kuachana tu.

Kingine watu wamepungukiwa na uvumilivu, juzi nimepigana sana kuokoa ndoa ya mdogo wangu ambaye alitaka kumuacha mkewe waliyezaa naye watoto wawili ili aoe kabinti ka Chuo Kikuu bila sababu zinazoeleweka lakini mwishoe nikabaini huyu amemchoka shemeji tu. Wanawake nao mwanaume akichoka mathalani hana hela tena au kaishiwa nguvu za kiume wanaanza visa mwishoe wanakimbia.

Nini sababu nyingine zinachangia? Karibu mtoe maoni tuwaandae vijana kabla hawajaingia kwenye ndoa takatifu.
 
Binafsi i don't believe in marriage japo nipo kwenye ndoa ila anytime ntaiacha maana ninayokutana nayo ni makubwa na si swala la uvumilivu no mimi nimevumilia kwa miaka minne unaenda wa tano ila mtu ndo kama anakuona unajipendekeza na huna pa kwenda, nadhani kiburi cha pesa na hulka ya mtu binafsi kuwa na wanawake wengi pia vinachangia ndoa nyingi kuvunjika,mwanamke unaweza ukavumilia na kujaribu kumrekebisha ila mwanaume anakuona km unampanda kichwani na kumfatilia mambo yake so hapo ndo kuna tatizo
 
Hizi ndoa hizi
Pamoja na kusoma sana humu na kusikia kuwa ndo za siku hizi majanga ila bado mimi nahitaji ndoa yakinishinda ntaondoka.
Inafikia hadi hatua mtu aliyeolewa anakwambia kabisa mwaya mdogo wangu usiolewe ndoa ngumu ingekuwa mimi wewe nazaa katoto kangu kamoja natulia.
Hapo unabaki tu kumshangaa.
Si kila mtu atapata ndoa yenye matatizo japo nyingi za siku hizi kila mtu analalamika.
Kuwa mke kuna raha yake ila usivumilie mpaka ifikie hatua unatolewa jicho eti unailinda ndoa yako.Maji yakizidi unga tafuta mbadala wa maisha yako.
Maisha yenyewe mafupi uje teseka kwasababu ya mtoto wa mwingine.
 
Mkuu kinachofanya ndoa ziwe ngumu siku hizi ni watu kuingia kwenye ndoa bila kuelewa wanakuwa humo kwa sababu gani? Sasa hivi ukisema uulize mtu kwanini amefunga ndoa ni wachache sana watakaokupa majibu ya kuridhisha nilichokiona kwa muda niliokaa kwenye ndoa ni yafuatayo
1. Wanandoa wanajua ni furaha siku zote hakuna nyakati za huzuni, hasira na maumivu
2. Wanafuata mapenzi kwenye ndoa na sio kujenga familia nzuri
3. Hawaelewi kuwa mtu unaeenda kuishi naye ana mapungufu na anaweza kukosea na unapaswa kusamehe over and over bila kuweka kinyongo
4. Watu wanategeana kufanya majukumu yao mfano kuhudumia familia, na kuheshimiana
5. Watu wanakata tamaa mapema sana linapotokea tatizo hawakai kusolve au kufight ndoa iendelee kuwepo
Hayo ndo niliyoyaona na nimeyafanyia kazi kwa kiasi kikubwa nyumba ina amani na ninaimani nitazeeka na mzee tukiwa pamoja in one piece.
 
mi naona maisha ya ndoa ni mazuri km mtaishi kwa upendo ila kwa sasa zipo familia hali mbaya yaan baba analala kivyake mama kivyake na hakuna kupika kisa baba hajaacha chakula yani bwai ni bwai na zp familia baba akipata pesa mama anachukua anaweka kapuni ndo maan unakuja wasoweza vumilia wanakunywa sumu wanakufa
 
nani anataka kuishi na Malaya aje aletewe miwaya ndani!! wacha waachane tu.

na usiseme wanawake wanalipiza, sema wanaenda kutafuta furaha yao. unafikiri ni maboksi hawana hisia au wana mioyo ya chuma? aishi maisha yake kumlilia MTU ambaye hamjali? acha tu watafute furaha nao.

ukisema tu ndoa ina miaka thelathini wala hunivutii, hadi nijue ni ndoa kweli ama vepee! sio sifa kusema tu ndoa INA muda mrefu wakati wahusika hawafurahii, mnafurahia nyie watazamaji!
 
2. Wanafuata mapenzi kwenye ndoa na sio kujenga familia nzuri
. ninaimani nitazeeka na mzee tukiwa pamoja in one piece.
lol duh

sasa mapenzi watoe wapi??

au ndo wale una mwenzi wa kulea naye watoto ambaye ndo unaishi naye na mwenzi mwingine huko nje wa kuufurahisha moyo??
 
Binafisi nikweli ndoa za zamani zili dumu nikisema mazingira ya kipindi iko yali luhusu,unakuta mwanamke tangu aolewe anashikwa kiuno na mmewe pekee ila nambie saivi hali ilivo.kwa wanaume sasa ndio usiseme.Kipindi iki ndoa zina changamoto kupita kiasi.

Kiukweli tuache kufalijiana ndoa za kweli ndio zinaishia.

Wanao sema ndoa raha waulize wamepitia matatizo mangapi bado wakaiona ndoa ni raha.

Kwa ufupi naamini miaka ijayo mtu mwenye akili timamu(ukiacha hawa wanao funga ndoa kuepuka dhambi ya zinaa) atakae kua kwenye ndoa atashangaza sana.
 
Mkuu kinachofanya ndoa ziwe ngumu siku hizi ni watu kuingia kwenye ndoa bila kuelewa wanakuwa humo kwa sababu gani? Sasa hivi ukisema uulize mtu kwanini amefunga ndoa ni wachache sana watakaokupa majibu ya kuridhisha nilichokiona kwa muda niliokaa kwenye ndoa ni yafuatayo
1. Wanandoa wanajua ni furaha siku zote hakuna nyakati za huzuni, hasira na maumivu
2. Wanafuata mapenzi kwenye ndoa na sio kujenga familia nzuri
3. Hawaelewi kuwa mtu unaeenda kuishi naye ana mapungufu na anaweza kukosea na unapaswa kusamehe over and over bila kuweka kinyongo
4. Watu wanategeana kufanya majukumu yao mfano kuhudumia familia, na kuheshimiana
5. Watu wanakata tamaa mapema sana linapotokea tatizo hawakai kusolve au kufight ndoa iendelee kuwepo
Hayo ndo niliyoyaona na nimeyafanyia kazi kwa kiasi kikubwa nyumba ina amani na ninaimani nitazeeka na mzee tukiwa pamoja in one piece.
Mungu azidi kuwasimamia mpendwa.
 
NDOA za siku hiz tunavumiliana tuu tukichokana Tuna Achana Ndoa zilukuwa zile za Ma Babu zetu na Bibi zetu sio hiz za kuoa au kuolewa kama fashion tuu
1475414176026.jpg
 
Ndoa ni tendo la kiimani hivyo wanandoa inawapasa kumtanguliza Mungu mbele ili aweze kuilinda ndoa yao. Vijana wa siku hizi wakimaliza kuoana hawamuhusishi tena Mungu wao,, Hawaendi Misikitini wala Makanisani. Hawasali pamaoja! Sala ndio nguzo pekee ya ndoa! Muwekeni Mungu wenu mbele nanyi mtaishi miaka mingi kwa raha daima!

Pia vijana waache kuhusisha maisha ya ndoa na mambo ya social networks.. Social networks ndio chanzo kikubwa cha kuvuruga ndoa nyingi! Wana ndoa wanapotaka kuiga mambo ya watu wengine wanayoyaona kwenye social network ndio tatizo linapoanzia hapo. Mdada anaona mwenzake kila siku katolewa outing na mumewe naye anataka mumewe amfanyie vivyo hivyo bila kujali mpangilio wao wa kimaisha yeye na mwenza wake!
 
Ndoa ni Taasisi inayojitegemea alafu unapata cheti hata kabla ya mtihani.

Binafsi i don't believe in marriage japo nipo kwenye ndoa ila anytime ntaiacha maana ninayokutana nayo ni makubwa na si swala la uvumilivu no mimi nimevumilia kwa miaka minne unaenda wa tano ila mtu ndo kama anakuona unajipendekeza na huna pa kwenda, nadhani kiburi cha pesa na hulka ya mtu binafsi kuwa na wanawake wengi pia vinachangia ndoa nyingi kuvunjika,mwanamke unaweza ukavumilia na kujaribu kumrekebisha ila mwanaume anakuona km unampanda kichwani na kumfatilia mambo yake so hapo ndo kuna tatizo
Duh pole sana lakini ndo mitihani ya ndoa
 
Mkuu kinachofanya ndoa ziwe ngumu siku hizi ni watu kuingia kwenye ndoa bila kuelewa wanakuwa humo kwa sababu gani? Sasa hivi ukisema uulize mtu kwanini amefunga ndoa ni wachache sana watakaokupa majibu ya kuridhisha nilichokiona kwa muda niliokaa kwenye ndoa ni yafuatayo
1. Wanandoa wanajua ni furaha siku zote hakuna nyakati za huzuni, hasira na maumivu
2. Wanafuata mapenzi kwenye ndoa na sio kujenga familia nzuri
3. Hawaelewi kuwa mtu unaeenda kuishi naye ana mapungufu na anaweza kukosea na unapaswa kusamehe over and over bila kuweka kinyongo
4. Watu wanategeana kufanya majukumu yao mfano kuhudumia familia, na kuheshimiana
5. Watu wanakata tamaa mapema sana linapotokea tatizo hawakai kusolve au kufight ndoa iendelee kuwepo
Hayo ndo niliyoyaona na nimeyafanyia kazi kwa kiasi kikubwa nyumba ina amani na ninaimani nitazeeka na mzee tukiwa pamoja in one piece.
Hongera mkuu vijana wengi inatupasa kufuata ushauri huu
 
Back
Top Bottom