Kulikoni mnafanya Msiba kama sherehe za kawaida?

Kulikoni mnafanya Msiba kama sherehe za kawaida?

Mwajiri dodoma!!!!!we umeajiriwa sector gani na umesomea nini na chuo gani au ndo wale wa muslim university.ila kwa nionavyo mhh hata muslim university hujapita.unajua great thinkers wana uwezo wa kumtambua mtu kama kasoma au la we inaonekana mfua nazi rufiji

Mimi nimesoma Mzumbe University. Ni mtaalamu wa Mambo ya Mawasiliano!!
Swali jingine???
 
Binadamu ni wa ajabu sana,
Utakuta mtu ni mgonjwa kweli yuko hoi hawamjulii hali wala hawamjali.

Mtu keshafariki unatoa gari la kifahari, mnachanga pesa za bia na vyakula vya gharama kubwa.
Ili tu waombolezaji wawaone mna utajiri au mali wakati mlishindwa hata kumpelekea maji alipokuwa
mgonjwa. Inasaidia nini???
 
Mimi nimesoma Mzumbe University. Ni mtaalamu wa Mambo ya Mawasiliano!!
Swali jingine???
Hebu tupe ID yako na password ya kuingia kwenye ARIS maana nyie kama kweli ulisoma mzumbe halafu una IQ ndogo kiasi hicho basi tutawauliza wslimu wako ulipataje digrii yako
 
Ebwana msiba ni sherehe tu kama sherehe za harusi,kuzaliwa na nyingine nyingi so their very right.
Let them do
 
Huwezi pata positive response huku. Watu wake ndo hivyo tena.......
 
Mleta uzi atakuwa Lizone kikwete maana alishawai kujitambulisha hapa ,hiyo ndo hali ya maisha ya kwetu usishangae sana ndo maisha bora kwa kila mtanzania .
 
kufa kufaana.
Na wengi tumemridhia yule mtoa roho kwamba kazi yake ni ulaji kwetu hivyo ameamua kuzidisha kuua ili walau kuwapa ulaji kila nyumba mara moja kwa mwaka.
.
 
Mimi nimesoma Mzumbe University. Ni mtaalamu wa Mambo ya Mawasiliano!!
Swali jingine???

Labda umesomea mambo ya umbea.

Hii tabia yenu ya kushinda vijiweni mkinywa gahwa na kashata ndio inapelekea muwe vibaka na kujiingiza kwenye vikundi vya kigaidi.
 
Mkuu Mandla,Bado unayo nafasi ya kutetea hoja yako lakin si kwa vigezo ulivyovitumia. Unadhani watu hao wangeonekana kuwa wana machungu sana kwa kusafiri na starlet na Raum kutoka Dar, Ungependa waende msibani wamevaa magunia au ungependa wanywe togwa na uji usio na sukari ndo waonekane wanamsikitikia marehemu.
 
Hii ni mada ya kipuuzi zaidi kuwahi kutokea hapa jf . Na ninaamini imetolewa na mtu mpuuzi sana ambaye hakutafakari lolote kabla ya kuandika. Tanzania kuna makabila zaidi ya mia moja kila kabla lina utaratibu wake ni si sawa kabisa kukosoa utamaduni wa kabila lingine ambao wewe haukuadhiri kitu. Ni sawa ni kuanza kuwalaumu wamasai kuwa kwann wanavaa kama wanavyo vaa.

Mghosi
 
Mimi nimesoma Mzumbe University. Ni mtaalamu wa Mambo ya Mawasiliano!!
Swali jingine???

Kwa kweli siamini kama wewe ni msomi wa mzumbe...! Hata form four wa shule ya kata angetafakari asingeandika upuuzi kama huu. Watu wanunue magari yao, wanazika ndugu yao kwa ngarama zao wewe unawashwa nini? Alafu umeshindwa kujua ecconomic status ya jamii flan inadetermine tabia zao? Au unataka watu wote wabebe maiti kwa pikipiki kama watu wa Mtwara??

Mghosi
 
Wanabodi habari ya leo,

Binafsi naomba kusema ni vyema kuwajali na kuwahifadhi wapendwa wetu waliotutoka kwa njia nzuri na ambazo ziko kihalali kulingana na mila, desturi, tamaduni na dini tunazoziamini. Lakini pia niseme ni masikitiko sana kuondokewa na mtu katika jamii yetu na kaya zetu, lakini hayo huwa ni mapenzi ya Mwenyenzi Mungu kikubwa ni kuwaombea wapumzike kwa amani waliko tangulia.

Sasa, naomba nishangae mambo yanayoendelea kwa wenzetu Wachaga, kwakweli misiba yao ni sherehe kubwa, majigambo, ufahari mkubwa hakika hii sidhani kama ni jambo zuri hasa kwa wale ambao wanakuwa wamempoteza ndugu yao.

Misiba inakuwa mpaka na Pombe na vinywaji vingine vikali? Ufahari wa magari ya bei kubwa? Yote haya ni kwa faida ya nani? Mfano ukikaa barabara ya Arusha - Moshi utastaajabu utitiri wa magari ya kifahari kwenda kwenye msiba Moshi, hivi hili linawasaidia kweli wafiwa?

Utakuta mtu anatoka msibani analalamika, hoo mimi sikupata bia au hoo mimi sijala nikashiba. Kweli kweli ndugu zangu mmefikia huku....Hakika inaumiza sana.

Nimeyaona ndio maana nimesema, nisichukiwe kwa kusema ukweli!!

SIO JAMBO JEMA AU LENYE AFYA.

Mandla.

Hizo ni tamaduni zao kama yalivyo makabila na mila zao ambazo unaweza kuzishangaa pia mf; kuna kabila fulani katika visiwa vya papua, ufilipino au tonga nadhani, huwa wanakaa na marehemu wao ndani kwa miaka mingi tu na kila baada ya muda fulani huwa wanawapamba kwa mavazi na mikufu mipya n.k
Wajaluo huwa wanafungulia mziki na mambo yanaendelea msibani kama kawaida.
Makabila mengi hapa yana utani mpaka wa kuzuia maiti isizikwe hadi faini fulani itolewe kwa watani.
Kuna watu wanazikwa na mikufu bangili na vito vya dhahabu wakati wengine wanazikwa na magari yao kwenye kaburi lenye ukubwa wa nyumba ndogo ya kuishi.
Nachojaribu kukueleza ni kuwa, mila zinatofautiana kati ya kabila na kabila na kile unachokishangaa kwa mwenzio, yeye ana vingi tu anavyoshangaa kwako.
Kwa hiyo take it easy and start living. Afadhali hata wao wako honest kudai bia au chakula kuliko wanafiki wanaojiliza msibani huku wakiwa na nyuso za huzuni huku wakiwa na chuki mioyoni na kuishia kusengenya pembeni kwa miaka mitano baada.
 
We mtoa mada;ukitaka mada yako ichangiwe na wengi njoo na mada za kusifia kabila hilo!sio unakuja na mada za sijui mapenzi hawajui au matambiko na mizimu au ukabila makazin au ujambazi wao au sijui nin na nin au wanawake kuwahi kuzeeka au shapeless na wana miguu.Yaaan watakutusi matusi yote hata usiyo yajua.pole
 
Kuna furaha 3 kubwa katika maisha ya mwanadamu, 1, kuzaliwa,2ndoa, 3, kufa sasa hizo zingine sijui kipaimara, hitma, arobaini na mengineyo ni mbwembwe tu, hayo matatu ndio kiboko, kwa hiyo siyo sifa wanafanya, we sema ukifa hutaona wala kusikia nadhani watakuwekea na matarumbeta kabisa..!!
 
We mtoa mada;ukitaka mada yako ichangiwe na wengi njoo na mada za kusifia kabila hilo!sio unakuja na mada za sijui mapenzi hawajui au matambiko na mizimu au ukabila makazin au ujambazi wao au sijui nin na nin au wanawake kuwahi kuzeeka au shapeless na wana miguu.Yaaan watakutusi matusi yote hata usiyo yajua.pole
We kikosikazi wa ccm,mboga ya nape hivi unajua wachaga ktk tasnia ya urembo(ma miss) wameshinda mara ngapi.unajua wakubwa wangapi wa nchi hii wameoa huko?unajua wamesoma na wanashikilia kiasi gani uchumi wa nchi hii?unajua wakwere,wazaramo na wadengereko wamefaidika kiasi gani kwa kuhamishwa jijini na waliobaki wanafaidikaje na hawa wachaga.basi jaribu kumtafuta mwanachuo anaesoma walau masters muombe ktk research yake iwe hivi!!!CONTRIBUTION OF CHAGA TRIBE IN THE ECONOMIC DEVELOPMENT OF TANZANIA,case study DSM REGION.am sure hutarudia kuwagilibu wachaga.
 
Kama ulivyosema tufanye maziko kwa taratibu za dini, mila na tamaduni zetu basi jua taratibu hizi zinatofautuana kutoka jamii hadi jamii

Kuna jamii msiba ni sherehe Kama sherehe nyingine. Mfano nchini Ghana msiba unaweza kuwa sherehe kubwa kuliko hata harusi sijui kwa wachaga inaweza kuwa wanachukulia Kama sherehe pia huwezi badili tamaduni za watu kisa wewe hufanyi hivyo. Au Kama wewe ni mkristo unataka sema waislam hawako sawa sababu hawaendi na wanawake kuzika

Lakini pia msiba ni sherehe, watu wanafurahia kuwahi kuwa na mpendwa wao duniani

Kama mtu ana gari nzuri kwake unataka akakodishe baya ndio aje nalo msibani! Unataka wote wanaohudhuria misiba wawe masikini ndio ufurahi! Au unadhani msiba wakihudhuria masikini ndio wafiwa wanafarijika. Ndio nyie mnaotaka viongozi watembelee magari mabaya ili mfurahi muone mko sawa nao wakati in reality hamko sawa
 
Back
Top Bottom