Kulikoni huko NEC Dodoma

Kulikoni huko NEC Dodoma

Panda Kapesi

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Posts
345
Reaction score
220
Kimya mshindo jamani. Toka asubuhi source zetu za ndani za Dom hamjatujuza nini kinaendelea na uvuaji wa magamba huko ndani......au mmebanwa?
tunasubiri kwa hamu mtujuze!
 
nahisi magamba yamegoma kuvuliwa ndo maaana hakuna kilicho jiri mpaka sasa
 
gamba likikaa sana linakuwa sehemu ya mwili na ukilazimisha kulivua unapoteza maisha.
 
mo2.jpg


mo1.jpg


Yanayojilia Dodoma ni msukule. Picha hizo za huyo mjumbe ambaye ni Mbunge wa Singida kukimbia kikao kwenda kupooza nerves kwa kumeza moshi wa tobacco kutelemshia na kikombe cha tangawizi baada ya kubugia kashata ni dalili tosha yaliyomo kikaoni vurugu tupu, kukamiana, maana ngoma ilnayolia sana ni dalili ya kupasuka punde.
 
mo2.jpg


mo1.jpg


Yanayojilia Dodoma ni msukule. Picha hizo za huyo mjumbe ambaye ni Mbunge wa Singida kukimbia kikao kwenda kupooza nerves kwa kumeza moshi wa tobacco kutelemshia na kikombe cha tangawizi baada ya kubugia kashata ni dalili tosha yaliyomo kikaoni vurugu tupu, kukamiana, maana ngoma ilnayolia sana ni dalili ya kupasuka punde.

Huyu naye mjumbe wa NEC?
 
uteuzi wa makatibu 10 wa CCM wa wilaya . Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye walioteuliwa kuwa ni: Makatibu wa wilaya wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo: -
1. Ndg. Zainabu Mlawa,
2. Ndg. Paulo Mwita,
3. Ndg. Magdalena Ndwete,
4. Ndg. Ramadhani Sevingi,
5. Ndg. Odilia Maholeo,
6. Ndg. Omari Zuberi Mbwana
7. Ndg. Raymond Mangwala,
8. Ndg. Yahya Saleh Issa, 9. Ndg. Ame Omar Mkadam
10. Ndg. Langael Akyoo

Pia Kamati Kuu ya CCM imetengua uteuzi wa Makatibu watatu wa wilaya na kuwapangia kazi nyingine. Makatibu hao ni:-
1. Ndg. Zubeda Mbarouk aliyekuwa Kwimba
2. Ndg. Mussa Wenema aliyekuwa Kilindi
3. Ndg. Mkongea Ally Pira aliyekuwa Wilaya ya Magharibi. Kamati Kuu ya Halimashauri Kuu ya Taifa inafanyika tarehe 21 na 22/11/2011 na kufuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachofanyika tarehe 23 na 24/11/2011. Kikao hicho na vingine vinafanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Baada ya kumalizika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa tarehe 25 hadi 27/11/2011 kutafanyika Semina ya Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi wa ngazi ya Kitaifa hadi Wilaya. Katika semina hiyo watakaoshiriki ni Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, Sekretarieti za Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (UWT, UVCCM na WAZAZI), Makatibu wa CCM wa Mikoa na Wilaya zote nchini.
Nilikuwa nawajuza.
 
Back
Top Bottom